Ushauri kwa Serikali: Nashauri Serikali iwanyang'anye passport za kusafiria wale wote waliotukana, kudhihaki na kumsema vibaya Rais wetu

Mtu akiwa nje ya nchi akamtukana Raisi kuna compromise vipi National Interest or National Security? Watu wana maoni tofauti na mitazamo tofauti ya ki sera na kiuongozi, kukosoana kwenye dunia hii ya sasa hakukwepeki!!
 
Kama una uchungu si ukjifungie huko leba,

We unataka mtazamo wako kila mmoja awe ka.a wewe..!
 
Mtu akiwa nje ya nchi akamtukana Raisi kuna compromise vipi National Interest or National Security? Watu wana maoni tofauti na mitazamo tofauti ya ki sera na kiuongozi, kukosoana kwenye dunia hii ya sasa hakukwepeki!!
Mkuu naomba uwaze mara mbili mfano wewe umeenda kwa Trump. Then unaanza kumwambia Trump habari za kiongozi aliyepo madarakani huku ukimtusi Rais huyo, huoni kama unavujisha usalama wa taifa mkuu. Hahuoni kama unahamishia ikulu ya Tanzania Marekani.

Na unavyokwenda huko wewe unadhani lengo lako linakua ni lipi? kama sio kuomba, msaada hao beberu wakusaidie kumtoa huyo madarakani kwa interest zako wewe mwenyewe?
 
we nikikuita ni mjinga nafikiri unastahili huwezi kuwa na mawazo mufilisi kama haya hata kujipendekeza kumezidi kipimo
 
Piece of written masturbation! For how long you been flicking that bean?!
 
Huwezi ukampora mtu passport bila kufwata sheria ,haitauwa kirahis kama unavyofikir wewe
 
Kwa kweli una muda was kupoteza kuandika huo utumbo.wanyang'anywe passpot ili iweje.passport ni mtu,taasisi au ni Mali ya watz wote?kila mtu Ana uhuru wa kutoa mawazo yake na huo uhuru uko kikatiba ili mradi tu haivunji hiyo katiba.
 
Kumbuka passport sio kadi ya kliniki kusema kuwa watu wanapewa bure.
Passport zinanunuliwa kwa pesa 150K,JMT imedhamini raia wake kupitia passport.
Na hiyo serikali inayotukana viongozi wa upinzani na wananchi wenye kutofautiana nao kiwawazo tuwanyang'anye nini??
Nakushauri mleta mada weka jina lako halisi viti maalumu bado kuna nafasi za kumwaga.
 
Sawa, hebu twende taratibu. Nadhani kupinga kilicho kibaya kwenye ngazi ya kimataifa sio kosa na wala sio kudhalilisha. Inawezekana nafasi ya kukipinga mkiwa ndani ya Nchi haiwezekani tena, lazima utumie njia mbadala.

Sasa chukulia mfano mtu kama Tundu Lissu alivyonyanyaswa, amefunguliwa kesi za ajabu ajabu, za uchochezi wakataka na kumpima mkojo juu [emoji16]. Amepigwa risasi ndani ya makazi ya wabunge, waligoma kumtibu mpaka Bunge lipate ruhusa kutoka kwa Rais, polisi hawajafanya uchunguzi wanasema mpaka victim mwenyewe arudi nchini (maana nyingine ni kwamba angekufa kusingekuwa na uchunguzi), walizuia maombi kwaajili yake, wamekamata watu waliovaa Tshirt za "Pray for Lissu", wamezuia watu wasitoe damu hospitalini,,,haya yote amefanyiwa yeye unategemea akiwa huko nje atamuongelea vipi Raisi wa Nchi na vile yeye ndiye mhanga wa matendo ya Serikali??


Alafu chukulia mfano mwingine - unaongozwa na Serikali ambayo haifuati utawala wa sheria, watu wanabambikiziwa kesi za uongo, wenye mawazo mbadala wanaonewa na kunyanyaswa, watu wanawekwa mahabusu miaka zaidi ya saba kesi zao haziamuliwi (Masheikh), wafanyabiashara wananyanyaswa kwa kunyangwa mali zao (wa bureau de change Arusha) au kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi ili tu kukwapua mali zao kwa nguvu, wabunge wanafutwa uanachama alafu spika hawaondoi bungeni kama sheria inavyotamka wazi, chaguzi haziwi huru (mfano chaguzi za serikali za mitaa), alafu Serikali hiyo hiyo ikaondoa haki ya mtu binafsi au taasisi kuishitaki kwenye Mahakama ya Afrika (African Court on Human and Peoples' Rights). Unategemea watu watakimbilia wapi kuomba msaada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…