habarini!!
wazo hili linakuja baada ya utafiti wa muda mrefu wa shule kadhaa ZA SEKONDARI!
hawa walimu wa kike walio katika umri wa makumi na ishirini wana tabu sana huko mashuleni.......
1. Hawatulii vituoni kwani wengi wao wanakuwa kwenye kuhangaika na maisha ya kutafuta wenza na kula ujana.....leo ameomba ruhusa ya kwenda Arusha, kesho Mwanza; keshokutwa Dar, mtondogoo Mtwara. Maonyo wala ripoti hazisaidii.....chuchu zimesimama bwana!
2. Wasema ovyo, viburi kwa wakuu wao na wamejaa ushindani wa wao kwa wao unaoleta mabifu yasiyo na maana maeneo ya kazi na kudororesha upataji wa elimu wa watoto wetu.
3. Wengi wao wanavaa viguo vifupivifupi vinavyoacha maeneo yao nyeti nje kabisa, mfano mbaya kabisa kwa watoto wetu!
4. Shughuli za uzazi. hili ni tatizo.....Yaani kwenye shule yenye walimu wa kike kuanzia 4 hadi 8 ni balaa. nitatoa mfano wa shule flani hivi yenye walimu 5: mwaka 2017 walimu wawili walipata likizo ya uzazi, waliporudi wao wawili wengine wakafuata 2018 na baadae mwingine 2018 hiyohiyo. Mwishoni mwa 2019 wale wawili wa mwanzo wakachukua tena mimba (utafikiri wanaaambizana)na kupata likizo ya uzazi. Ikumbukwe wakisharudi kuzaa basi changamoto za malezi ni kubwa mno kama vile kufundisha nusu siku kwa muda wa miezi sita, kuugua kwa watoto hivyo kuhitajika kwa ruhusa za mara kwa mara n.k. ukiangalia kwa undani, hawa wanaperform robo tu ya majukumu yao kiukweli halafu wanalipwa sawa na wa kiume.
5. Kukosa uvumilivu na Micharuko, yaani unamkuta mwalimu amejiandaa kusikia vijimaneno kutoka kwa wanafunzi (jambo ambalo ni la kawaida kwa wanafunzi kuzungumzazungumza kuhusu walimu wao) ili akawakomeshe kwa 'kuwachamba'......kichekesho!
Kwanini wa miaka 35?
1. wengi wao wameshakuwa na muelekeo wa maisha (mwenza, watoto n.k) au wanakuwa wameshakubaliana na hali halisi na hivyo hawawi wasumbufu (watulivu).
2. wanaweza kuzimudu vizuri changamoto za malezi ya watoto
3. wanavaa vizuri (wanajiheshimu angalau) kwani wanakuwa hawana cha ajabu sana cha kuonyesha watu.
Nawasilisha kwa maboresho!