Ushauri kwa Upinzani- Membe asiingizwe kwenye mikakati yenu

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Naomba mods msiuunganishe huu uzi!

Huu ni ushauri wangu kwa vyama vya upinzani! Mmesikia Membe amejitoa CCM, Huu ni mkakati wa chama Tawale kuhakikisha,
1. kwanza kupunguza kura zenu. Hii ni pale Act na Chadema wasipoungana

2. kuhakikisha CCM wanakuwa na taarifa zote za mipango na mikakati yenu. Msijidanganye, taarifa zenu zote zitakuwa White House Dodoma na Lumumba Dar es Salaam.

3. Membe akipeperusha bendera ya upinzani, CCM wakiiba kura Membe hawezi pinga matokeo na kulianzisha . Atakubali kushindwa. NA HII NDO TARGET KUBWA YA CCM. CCM wanaogopa Lissu anaweza kukataa matokeo na kuhamasisha watu kuingia mtaani endapo wataiba kura na kupoka ushindi wa upinzani hivyo vyovyote vile wako tayari kwa gharama yeyote upinzani asimame mtu ambae hatopinga ushindi wao. 2015 walimpandikiza Lowassa na sasa 2020 wamempandikiza Membe

Ushauri kwa Upinzani.
Vyovyote vile hata Act na Chadema wakiungana, Lissu ndo apewe kupeperusha bendera. Kama Membe mnamhitaji mpeni nafasi ya kuwa Waziri Mkuu mtakapochukua nchi/dola na kwa vikao vyenu vya ndani naomba msimshirikishe Membe.

Namalizia kwa kusema ACT NA CHADEMA muungane. Zanzibar Mgombea awe Maalim Seif na Msaidizi Fatma Karume

Na kwa Bara mgombea awe Tundu Lissu na Membe aandaliwe nafasi ya Waziri Mkuu. Mgombea mweza kwa bara mtachagua yeyote yule.
 
Mtaji wa CCM ..

1) Wananchi wenye Elimu ya chinii kabisa ( ambao ndio wengi sana )
2) Vyombo vya Dola.

Upinzani unapaswa UCHANGAMANE na B.Membe lakini USICHANGANYIKANE naye.
Membe hawezi kukataa Matokeo ya wizi wa kura ya CCM, hawezi kuhamasisha nguvu ya umma kupinga wizi wa kura na uonevu wa CCM. Na kama upinzani hawajui HII NDO NJIA PEKEE YA KUIONDOA CCM MADARAKANI.

Bila nguvu ya umma, CCM hawatotoka madarakani hata miaka 100,000 ijayo. Na mtu pekee wa kuhamasisha nguvu ya umma ni TUNDU ANTIPAS LISSU.
 
Nina maadui 11 ikifika 2016 watakimbilia Kenya
 
Acheni uchawi.mbona mnataka kuharibu mambo.Membe ni mpinzani kama wengine msimnyanyapae.
Mwacheni kachero mbobezi atiririke.
 
Wewe ni nani hata kutoa ushauri, una impact gn kwenye upinzani wa tz!! Wacha twende na BM 2020, mwaka huu gia inabadilishwa majini!
 
Sijamsikia membe anasimamia nini,hii Inanipa wasiwasi kama kweli Yuko fit kwa mapambano.
Nafasi ya juu ambayo upinzani wanaweza kumpa Membe ni Waziri Mkuu. Na hapo wasimuhusishe kwenye mikakati yao ya ndani.
 
Wewe ni nani hata kutoa ushauri, una impact gn kwenye upinzani wa tz!! Wacha twende na BM 2020, mwaka huu gia inabadilishwa majini!
Ushauri una option mbili ni kuuchukua hata kuukataa.
Kama Mtanzania wa kawaida nina haki ya kutoa ushauri popote.
 
Membe yuko vizuri tuacheni na sisi chadema tuchukue nchi.
Chadema itachukua nchi wakimsimamisha Lissu. Mtu mwenye hulka ya upiganaji kweli. Bila watu kama Lissu na Heche wanaoweza kumobilize public pressure kwa CCM , upinzani wasahau kuchukua nchi.
 
Naomba mods msiuunganishe huu uzi!

Huu ni ushauri wangu kwa vyama vya upinzani! Mmesikia Membe amejitoa CCM, Huu ni mkakati wa chama Tawale kuhakikisha,
1. kwanza kupunguza kura zenu. Hii ni pale Act na Chadema wasipoungana

2. kuhakikisha CCM wanakuwa na taarifa zote za mipango na mikakati yenu. Msijidanganye, taarifa zenu zote zitakuwa White House Dodoma na Lumumba Dar es Salaam.

3. Membe akipeperusha bendera ya upinzani, CCM wakiiba kura Membe hawezi pinga matokeo na kulianzisha . Atakubali kushindwa. NA HII NDO TARGET KUBWA YA CCM. CCM wanaogopa Lissu anaweza kukataa matokeo na kuhamasisha watu kuingia mtaani endapo wataiba kura na kupoka ushindi wa upinzani hivyo vyovyote vile wako tayari kwa gharama yeyote upinzani asimame mtu ambae hatopinga ushindi wao. 2015 walimpandikiza Lowassa na sasa 2020 wamempandikiza Membe

Ushauri kwa Upinzani.
Vyovyote vile hata Act na Chadema wakiungana, Lissu ndo apewe kupeperusha bendera. Kama Membe mnamhitaji mpeni nafasi ya kuwa Waziri Mkuu mtakapochukua nchi/dola na kwa vikao vyenu vya ndani naomba msimshirikishe Membe.

Namalizia kwa kusema ACT NA CHADEMA muungane. Zanzibar Mgombea awe Maalim Seif na Msaidizi Fatma Karume

Na kwa Bara mgombea awe Tundu Lissu na Membe aandaliwe nafasi ya Waziri Mkuu. Mgombea mweza kwa bara mtachagua yeyote yule.
Membe agombee ubunge kupitia chadema ili awe KUB
 
Chadema itachukua nchi wakimsimamisha Lissu. Mtu mwenye hulka ya upiganaji kweli. Bila watu kama Lissu na Heche wanaoweza kumobilize public pressure kwa CCM , upinzani wasahau kuchukua nchi.

Its just matter of time.
 
Back
Top Bottom