FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Pamoja na yote, tusi-underestimate uwezo wa kijeshi wa Russia. Ni miongoni mwa nchi zenye best missile systems katika masuala ya defense (nafahamu kuna debates mbalimbali kuhusiana na theoretical capabilities za silaha ukilinganisha na performance katika mapambano).Haya yote unafikiri vyombo vya ulinzi vya Russia havitambui? Kama UK tu ameweza sambaza Javeline na kuangamiza misafara yote ya Russia Ukraine, what if UK ndo angeingia vitani ground battle dhidi ya Russia? Si wangepasua njia mpaka Russia?
Sasa huyo ni mshirika tu wa US, US mwenyewe muweke pembeni. Russia anafikiria mno kupambana na US, lakini kitu pekee anachosita ni uimara wa zana zake.
Kama vifaru vyake vya kisasa vimeweza kuwekwa chini kizembe vile pale Ukraine, ana uhakika gani hizo Nuclear zake pamoja na Submarines zinaweza tikisa anga la US while US kabla ya kumfikia sehemu nyingi mno ana Base?
US sana sana anamfikiria NATO, akiingia vitani na Russia, Ulaya inaweza ikaathirika zaidi kwa silaha uchwara za Urusi lakini sio US.
Hakuna taifa nilikuwa naliamini ktk medani za Vita kama Russia, ila kupitia hii ya ukraine nimeona ni taifa la kawaida tu, sema ubaya ni kwamba kuna Nuclear kwao, na nina mashaka sasa na hizo Nuclear. Nchi gani inalipuliwa kituo kikubwa cha mafuta kwa helcopter? Hizo s300, s400 defence systems zilizimwa au?
Katika medani hii ya kivita na propaganda, US, German, France na UK ni moto mwingine. Huu ni ukweli mchungu.
Tukumbuke pia hata kiuchumi Russia hamgusi Japan, weka mbali hao jamaa hao juu, Japan mwenyewe tu hamgusi kipesa.
Pia, ni miongoni mwa nchi zenye share mkubwa katika uuzaji wa silaha kwenye soko la dunia.
Hata hivyo, hili suala la Ukraine limetia doa uwezo wao kwa kiasi fulani. Hilo ni kutokana na objectives walizojiwekea zikiwemo tunazozijua pamoja na nature ya vita ambayo wamekuwa wakipigana.
Nadhani niliwahi kusema awali mahali fulani humu kuhusiana na masuala ya muhimu katika kufanikisha malengo mahususi katika vita hasa zenye nature ya uvamizi (invasion).
Invasion lazima iwe na malengo ambayo yanapaswa kuwa achieved kwa gharama ambayo lazima ifanyiwe mahesabu yenye usahihi. Military strategy inapaswa kuzingatia movements sahihi za majeshi pamoja na anticipation ya kiwango cha upinzani kitakachotokana na adui. Hapa ndipo tunapoona utofauti kati ya "operation" na "campaign".
Kumekuwa na makosa ya kiufundi katika hilo kwa upande wa Russia. Resistance ya Ukraine imeonekana sana, pia kutokana na flow ya silaha kutoka nje. Objective kuhusu "de-militarization" kupitia jeshi haijaonekana kuwa achieved ipasavyo hadi sasa. Tusubiri tuone kama itaweza kuwa achieved kwenye mazungumzo yanayoendelea.
Hayo pamoja na masuala mengine ya kiraia kama 'local support' katika sehemu yenye uvamizi n.k. yanapaswa kuzingatiwa ili kutengeneza kitu kinachofahamika kitaalamu kama, technical feasibility, ambapo kwa case hii, pamoja na objectives tulizoambiwa, uvamizi haukuwa technically feasible.