Ushauri kwa vijana ambao hamjawahi kuajiriwa

Hiyo ndio Tanzania sasa. Haki vile wewe unenielewa haswa. Inasikitisha Kila ninapo fanya kazi najikuta naacha mwenyewe. Mimi sipendi kuwa chawa, sipendi kuonewa, sipendi kutumikishwa. Sipendi kunyonywa mbaya Zaidi yote ninayo yachukia yanafanywa kwenye ajira zetu hizi. Nimeacha kazi kampuni Zaidi ya 4😭 Moja wapo hapo Hadi nilishitakiana nao mahakamani
 
Sasa unaishije
 
Unahoja za msingi sana baba yangu ni mstaafu mwalimu wa secondary siku moja aliwahi nitamkia hivi wale wenzangu wote walioachaga kazi za serikali wakaamua kufanya shughuli zao wenyewe leo hii nimatajiri na wengine wamekimbilia canada na japani baada ya kufanikiwa hata watoto wao wapo level za juu kias kwamba wakikutana nyumbani moshi yeye ndie huonekana low class funancially kuliko agemate wengi.
Ajira za Tanzania iwe sekta binafsi au serikali nizakitumwa na haziruhusu mtu kuonesha zaidi ya alichonacho full kubanwa kubanwa,kusimangwa,kutishwa n.k
 
Duuh Sasa si Bora kazini unajua mwisho wa mwezi uhakika
Bora ujiajiri. Lakini Bora ya mtu ni kile anachoona yeye kinafaa...maana picha halisi ya maisha ya mtu anayo yeye mwenyewe. Ajira za kiTanzania ni utumwa mtupu amini usiamini...kama ujawahi kiajiriwa huwezi kuelewa ninacho kimaanisha hapa.
 
Ni utumwa haswa. Na ukiona mpaka mtu mzima amesema hivyo ujue amekutana na mengi sana.
 
 
Unachokisema ni sahihi sana,kama kweli tungejimudu vijana tungetoka nje ya nchi na waajiriwa wapya watakuja kuamini baada ya miaka kupita kwakweli nakuunga mkono sana
 
Unyenyekevu ni muhimu popote pale unapokua na ni nyenzo katika kupata maisha mazuri.
UKIONA NI KAZI KUNYENYEKEA FUNGUA KAMPUNI LAKO BASI
Kunyenyekea na Heshima ni vitu viwili tofauti. Mtu mwenye uwezo wa kumnyenyekea mwingine ana vielement vya uchawa. Unyenyekevu ukizidi sana unakuwa utumwa. Mimi nitakuheshimu lakini sio kukunyenyekea
 
umeona wapi injinia docta rubani ananyanyasika?
Hawa mainjinia si ndio hawa hawa wakikabidhiwa tenda za ujenz wa madarasa wanapokea maelekezo kutoka kwa madiwan au unazungumzia injinia gan??

Madaktari si ndo hawa hawa wanafokewa na ma wanasiasa daily umesahau ile ajali ya costa ilokuwa inapeleka msiba moshi cku zle??? Daktar anaulizwa eti ulikua wapi mbna nyumban kwako tulikufata hukuwepo? Yan mtu ukae nyumban all the time kama mwanafunz wa boarding!!!!

Hao maruban huez jua undan wa maisha yao coz wapo wachache kwa hyo ni nadra kuona the real color of their job!!
 
Huu uzi nadhani ndio uzi the best kwa kufungia mwaka. Kwa ulichokiandika hapa ipo wazi bila ubishi kuwa wewe una ufahamu na ujuzi au experience ya kutosha eneo la kazi.

Hiki ulichokisema ni ukweli wa 100% wa kinachoonekana na kuendelea maeneo ya kazi. Na ndio maana Tanzania kutoboa ni mtihani kwa watu wenye talents, wenye uwezo, intelligent, na wabunifu labda kama utaanzisha kitu chako binafsi.

Tanzania haifeli sababu watu hawana akili au uwezo, Tanzania inafeli sababu kuna watu washenzi wameshikilia position muhimu na kuzigeuza mali zao binafsi ile hali hawazimudu.

Nimekuelewa sana hicho kipande cha ukiwa unajua shida ipo wapi na ukataka kurekebisha then unashangaa waliokuzunguka wanakupinga kwa nguvu kabisa wakikutaka ufanye kinyume cha uhalisia jambo ambalo linakufanya tena ushiriki uharibifu.

Kwa mtu mwenye uwezo wa kiakili lazima utapatwa na msongo wa mawazo eneo la kazi na utakuwa na majuto sababu unaona kabisa unashirikishwa kuharibu badala ya kutengeneza.

MUNGU atusaidie kwakweli tujenga mfumo mpya huu uliopo ufe na hawa takataka waliopo.
 
Kuna dada yupo department ya uhasibu aisee ukimuona unaweza muonea huruma namna anahangaika nayo. Maana anahoji vitu vya msingi na vya logic ila maelekezo kutoka juu anayopewa anajikuta anatamani kuacha kazi hata kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…