Uchaguzi 2020 Ushauri kwa waandaaji wa Kampeni za CHADEMA

Omary - Msamalia

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
2,079
Reaction score
4,521
Siku 3 zilizopita chama cha CHADEMA kimefanya Uzinduzi wa Kampeni zake Mkoa wa Dar es Salaam, Katika hali isiyotarajiwa mwitikio wa watu umekuwa Mdogo kuliko Kawaida sana naweza kusema(Waliohudhuria ni chini ya 5000).
Wafuasi na wapenzi wa Chadema walioko sehemu mbali mbali wanaweza kujitetea kwa Kusema CCM wao wana Wasanii na Wanabeba watu kwenye maroli, Kwa maoni yangu hii ni Hoja dhaifu sana kwa mtu makini na mwenye utashi.

Kitengo Cha Hamasa CHADEMA kimelala au Hakifanyi kazi yake ipasavyo, msichukulie kwa wepesi Sanaa (Hasa ya Muziki). Maandiko yanasema Huko Mbinguni Kuna Malaika Maalumu wa Sifa(Nyimbo za Injili ndio zinasikilizwa sana kuliko Mahubiri ya Kanisani).

Muziki ni silaha muhimu sana kwenye Hamasa, Vijana wote wanaovaa nguo za kubana hawakuota mitindo hiyo ila waliiona kwa Wasanii. Muziki ni silaha hatari na yenye nguvu ya Saikolojia.

Si kweli CHADEMA Hamhitaji wanamuziki, Mnao wabunge na wengine wameimba jana na leo, Chadema msipuuze wala msiwabeze wasanii wakubwa wanapanda kwenye majukwaa ya CCM, Hebu fikiri Msanii Kama Harmonize leo anaimba Mistari aliyopangiwa na CCM na kesho anashiriki kwenye Tamasha kubwa la Michezo (Kwa watu Neutral), lazima atakuwa balozi na atawathiri kisaikolojia hata wale wasio na vyama au Swing voters.

Kingine CHADEMA msiwapuuze Watanzania wala msifanye kosa lingine la kiufundi kama siku ya leo (Jumapili) waandaaji wa Ratiba ya Kampeni wameshindwa kujua kama Siku ya leo Simba na Yanga wanashughuli zao tena kwenye Maeneo muhimu ya Kimkakati(Dar Es salaam na Arusha), mlipaswa msitishe shughuli zenu (Mtumie fursa hii kupiga Story na Mwananchi mmoja mmoja) Mhudhurie haya matukio mawili.

Mwisho Chadema rudini meza ya Mazungumzo kwa upole na Unyenyekevu na Vyombo vya Habari. Wapiga kura wengi wanakaa maeneo ambayo Youtube ina load kwa shida sana, na wakiingia Youtube wanawasikiliza wasanii wanaohudhuria Mikutano ya CCM
 
Naipenda CDM siwezi kupoteza kura yangu kuipa CCM.
Kiukweli kabisa Mbowe hakustahili kuwa mwenyekiti tena kaishiwa maarifa mapya.
Amsha amsha hazipo kabisa as if ndo mara ya kwanza tunashiriki uchaguzi mwaka huu.
 
Watanzania msiwafanye wajinga ila Mimi nimezunguka mikoa yote kuanzaia kusini mpaka kasikazini


Ukweli Ni kwamba watu wapo tayari kwa mabadiliko ila walikuwa wanasubiri ni nani analeta hayo mabadiliko?

Ila ukweli kwa Sasa watu wapo tayari kwa mabadiliko makubwa na Lissu ndio muarobaini wa huu utawala.
 
Leo Dar es salaam kulikwa na Tamasha la Mpira ya Yanga lenye kiingilio lakini Kampeni za Chadema hazikuwa na kiingilio ila wakazi wa Tabata Segera na Maeneo ya Jirani walioona Mechi ya Yanga ni muhimu kuliko ujumbe wa Lissu ni wengi sana..

Lissu alitakiwa ahudhuri uwanja wa Taifa, Tanzania hakuna kiongozi aliyewagusa mashabiki wa Yanga na Simba wanaishi nao.
 
Naipenda CDM siwezi kupoteza kura yangu kuipa CCM.
Kiukweli kabisa Mbowe hakustahili kuwa mwenyekiti tena kaishiwa maarifa mapya.
Amsha amsha hazipo kabisa as if ndo mara ya kwanza tunashiriki uchaguzi mwaka huu.
Unafikiri hizo amshaamsha za wanamziki zinafanywa bure? Unadhani hao wasanii wote wanaenda kwenye majukwaa ya CCM kwa kupenda pamoja na kuwa wanalipwa ?
Fikiria upya.
 
Ilipaswa wafike Uwanja wa Taifa
 
Nikilinganisha na kampeni za 2015. Lowassa alikuwa akivutia umati mkubwa lakini anashindwa kunadi sera. Wengi alikuwa akiwakatisha tamaa. Hapa Dar aligawana kura sana na Magu na alimzidi kura chache sana. Wabunge wengi wa Dar (Mdee, Mnyika, Kubenea etc) walipata kura nyingi kuliko Lowassa.

Kampeni za 2020 bado hazijavuta mikusanyiko ya mikubwa. Lakini Lissu ananadi sera vizuri. Wakiendelea kusambaza hizi short videos za Lissu kwa wapiga kura kupitia Twitter, Facebook, Instagram na WhatsApp watawafikia mamilioni ya watanzania bila kuhitaji hayo mashindano ya nyomi. Siasa ni sayansi.......na cha muhimu ni Lissu aendelee kuwashawishi wapiga kura.......Na anafanya hiyo kazi vizuri.......
 
Pesa ndio issue, yawezekana hawana budget ya intertainment.
Bajeti ni shida kweli,

Ila mimi nazungumzia Idara ya Hamasa ya Chama,Unadhani leo Lissu angeenda Taifa akakaa Meza na Kikwete angefukuzwa?


CCM wakitumia hizi fursa kuna watu watalalamika Simba na Yanga ni timu za CCM kumbe ni watu wa Public Relations wanafanya kazi vyema
 
Unadhani Lissu atafika Kura za Lowassa kwa sababu ya Kuongea?, unadhani watu milioni sita walikuwa hawajui kuwa Lowassa sio mzungumzaji?


Kwenye Jamii kuna kitu inaitwa Peer Influence
 
Una uwezo wa kuzunguka? au umezungukwa?? Mtoa mada kuwashauri kitaalamu lakini kwa ubishi wenu kaeni hivyo hivyo.CCM inawapiga mabao kama mmesimama.Kwa taarifa yako majukwaa safari hii siyo issue.Leo mbowe au Lissu mmoja wao alitakiwa kuhudhuria uwanja wa mkapa kama mpezi wa timu ya wananchi.
 
Hivi ww upo Tanzania au wapi,sasa chadema arudi kufanya mazungumzo na vyombo vya habari maana yake ni nini???

Wamiliki wa vyombo vya habari ndio hawahitaji kufanya kazi na chadema sababu wamekatazwa na CCM toka 2016 sasa ww unaposema CDM wafanye mazungumzo nao sijui unakielewa unachokizungumza???
 

Ndugu haya mambo hayahitaji Hasira ndugu yanahitaji utulivu wa Akili na maamuzi sahihi, Yaani Chadema kuongea na waandishi inakuwa swala la kutunishiana misuli mzee?, uanajua Kama UAE imeitambua Israel

News are bias mzee you have to avoid hili swala likuangukie

Mimi sina nia mbaya na Chadema, lakini subiri Uone kama akina Membe watawafukuza Waandishi wa Habari na Baada ya Muda tuuite ACT ni CCM B
 
Wenzio nyomi kwao ndo kila kitu. Yaani wasipopata nyomi usiku hawalali. Toka kampeni zimeanza, hatuzioni picha zao za kampeni zinarushwa kwa nadra sana. Hii kanda ya pwani mpaka sasa wameshafeli labda wakienda huko maeneo mengine.
 
Sawa ndugu
 
CHADEMA walishapoteza toka wakati wa kujiandikisha kupiga kura.

Sikuona hata wakihamasisha watu wapige kura. Uzinduzi wa kampeni zap ni kama walishtukiza.

Wanapwaya sana hao jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…