Omary - Msamalia
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 2,079
- 4,521
Siku 3 zilizopita chama cha CHADEMA kimefanya Uzinduzi wa Kampeni zake Mkoa wa Dar es Salaam, Katika hali isiyotarajiwa mwitikio wa watu umekuwa Mdogo kuliko Kawaida sana naweza kusema(Waliohudhuria ni chini ya 5000).
Wafuasi na wapenzi wa Chadema walioko sehemu mbali mbali wanaweza kujitetea kwa Kusema CCM wao wana Wasanii na Wanabeba watu kwenye maroli, Kwa maoni yangu hii ni Hoja dhaifu sana kwa mtu makini na mwenye utashi.
Kitengo Cha Hamasa CHADEMA kimelala au Hakifanyi kazi yake ipasavyo, msichukulie kwa wepesi Sanaa (Hasa ya Muziki). Maandiko yanasema Huko Mbinguni Kuna Malaika Maalumu wa Sifa(Nyimbo za Injili ndio zinasikilizwa sana kuliko Mahubiri ya Kanisani).
Muziki ni silaha muhimu sana kwenye Hamasa, Vijana wote wanaovaa nguo za kubana hawakuota mitindo hiyo ila waliiona kwa Wasanii. Muziki ni silaha hatari na yenye nguvu ya Saikolojia.
Si kweli CHADEMA Hamhitaji wanamuziki, Mnao wabunge na wengine wameimba jana na leo, Chadema msipuuze wala msiwabeze wasanii wakubwa wanapanda kwenye majukwaa ya CCM, Hebu fikiri Msanii Kama Harmonize leo anaimba Mistari aliyopangiwa na CCM na kesho anashiriki kwenye Tamasha kubwa la Michezo (Kwa watu Neutral), lazima atakuwa balozi na atawathiri kisaikolojia hata wale wasio na vyama au Swing voters.
Kingine CHADEMA msiwapuuze Watanzania wala msifanye kosa lingine la kiufundi kama siku ya leo (Jumapili) waandaaji wa Ratiba ya Kampeni wameshindwa kujua kama Siku ya leo Simba na Yanga wanashughuli zao tena kwenye Maeneo muhimu ya Kimkakati(Dar Es salaam na Arusha), mlipaswa msitishe shughuli zenu (Mtumie fursa hii kupiga Story na Mwananchi mmoja mmoja) Mhudhurie haya matukio mawili.
Mwisho Chadema rudini meza ya Mazungumzo kwa upole na Unyenyekevu na Vyombo vya Habari. Wapiga kura wengi wanakaa maeneo ambayo Youtube ina load kwa shida sana, na wakiingia Youtube wanawasikiliza wasanii wanaohudhuria Mikutano ya CCM