Uchaguzi 2020 Ushauri kwa waandaaji wa Kampeni za CHADEMA

Watanzania walio wengi inasemekana nimasikini kwahiyo sidhani kama wana simu Janja na Kama wana hela ya bando Kama inasemekana hawana hata uwezo wakupata milo mitatu.
Labda tuseme kutoka 2015 watanzania wameendelea sana na wanaweza sasa kutumia teknolojia kufuatilia siasa bila kuhudhuria viwanjani wala kupitia vyombo vya habari vilivyorahisi Kama TV na radio? Tuendelee kutafiti maana haya maendeleo ya ghafla waliopata watanzania yananiambia huenda kweli tuko uchumi wa Kati.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Yaani tanapa wanavyojitahidi kujieleza mpaka huruma
 
Ndio maana najitahidi sana Kuwasisitiza Chadema wameze Jeuri na wakubali kuishi na Watanzania. Wengi wanaongalia Campain zao humu sio wapiga kura husika video inaweza kuwa viewers 5000 watazamaji 1000 wanatokea Kenya 1000 Uganda, na pengine hao viewers walikuwa wanangalia huku wanasogeza mbele na kurusha matukio.

Chadema wasiweke bifu na vyombo vya Habari vya Ndani
 
Siku 3 zilizopita chama cha Chadema kimefanya Uzinduzi wa Kampeni zake Mkoa wa Dar es salaam, Katika hali isiyotarajiwa mwitikio wa watu umekuwa Mdogo kuliko Kawaida sana naweza kusema(Waliohudhuria ni chini ya 5000).
Wafuasi na wapenzi wa Chadema walioko sehemu mbali mbali wanaweza kujitetea kwa Kusema CCM wao wana Wasanii na Wanabeba watu kwenye maroli, Kwa maoni yangu hii ni Hoja dhaifu sana kwa mtu makini na mwenye utashi.

Kitengo Cha Hamasa Chadema kimelala au Hakifanyi kazi yake ipasavyo, msichukulie kwa wepesi Sanaa (Hasa ya Muziki). Maandiko yanasema Huko Mbinguni Kuna Malaika Maalumu wa Sifa(Nyimbo za Injili ndio zinasikilizwa sana kuliko Mahubiri ya Kanisani).
Muziki ni silaha muhimu sana kwenye Hamasa, Vijana wote wanaovaa nguo za kubana hawakuota mitindo hiyo ila waliiona kwa Wasanii. Muziki ni silaha hatari na yenye nguvu ya Saikolojia.

Si kweli Chadema Hamhitaji wanamuziki, Mnao wabunge na wengine wameimba jana na leo, Chadema msipuuze wala msiwabeze wasanii wakubwa wanapanda kwenye majukwaa ya CCM, Hebu fikiri Msanii Kama Harmonize leo anaimba Mistari aliyopangiwa na CCM na kesho anashiriki kwenye Tamasha kubwa la Michezo (Kwa watu Neutral), lazima atakuwa balozi na atawathiri kisaikolojia hata wale wasio na vyama au Swing voters.

Kingine Chadema msiwapuuze Watanzania wala msifanye kosa lingine la kiufundi kama siku ya leo (Jumapili) waandaaji wa Ratiba ya Kampeni wameshindwa kujua kama Siku ya leo Simba na Yanga wanashughuli zao tena kwenye Maeneo muhimu ya Kimkakati(Dar Es salaam na Arusha), mlipaswa msitishe shughuli zenu (Mtumie fursa hii kupiga Story na Mwananchi mmoja mmoja) Mhudhurie haya matukio mawili.

Mwisho Chadema rudini meza ya Mazungumzo kwa upole na Unyenyekevu na Vyombo vya Habari. Wapiga kura wengi wanakaa maeneo ambayo Youtube ina load kwa shida sana, na wakiingia Youtube wanawasikiliza wasanii wanaohudhuria Mikutano ya CCM
Kampeni inachangia sehemu ndogo sana katika uamuzi wa mpiga kura amuchague nani. Kama mpiga kura anafikiri kuwa hakuna athari yo yote aliyopata kwa miaka mitano iliyopita,hakuna namna ya kubadilisha msimamo wake. Katika mambo ya nchi wengi wape hadi pale watakapoelewa kwa nini mabadiliko yanahitajika sasa.

Ujinga ambao CCM imeulea ndiyo mtaji wake.
 
Nikilinganisha na kampeni za 2015. Lowassa alikuwa akivutia umati mkubwa lakini anashindwa kunadi sera. Wengi alikuwa akiwakatisha tamaa. Hapa Dar aligawana kura sana na Magu na alimzidi kura chache sana. Wabunge wengi wa Dar (Mdee, Mnyika, Kubenea etc) walipata kura nyingi kuliko Lowassa.

Kampeni za 2020 bado hazijavuta mikusanyiko ya mikubwa. Lakini Lissu ananadi sera vizuri. Wakiendelea kusambaza hizi short videos za Lissu kwa wapiga kura kupitia Twitter, Facebook, Instagram na WhatsApp watawafikia mamilioni ya watanzania bila kuhitaji hayo mashindano ya nyomi. Siasa ni sayansi.......na cha muhimu ni Lissu aendelee kuwashawishi wapiga kura.......Na anafanya hiyo kazi vizuri.......
Vijana wa kileo chini ya bwana Makamba Januari wanaamini kwenye nyomi
 
Kampeni inachangia sehemu ndogo sana katika uamuzi wa mpiga kura amuchague nani. Kama mpiga kura anafikiri kuwa hakuna athari yo yote aliyopata kwa miaka mitano iliyopita,hakuna namna ya kubadilisha msimamo wake. Katika mambo ya nchi wengi wape hadi pale watakapoelewa kwa nini mabadiliko yanahitajika sasa.

Ujinga ambao CCM imeulea ndiyo mtaji wake.

Kwa hiyo mnatukana wapiga kura sio?
 
Nikilinganisha na kampeni za 2015. Lowassa alikuwa akivutia umati mkubwa lakini anashindwa kunadi sera. Wengi alikuwa akiwakatisha tamaa. Hapa Dar aligawana kura sana na Magu na alimzidi kura chache sana. Wabunge wengi wa Dar (Mdee, Mnyika, Kubenea etc) walipata kura nyingi kuliko Lowassa.

Kampeni za 2020 bado hazijavuta mikusanyiko ya mikubwa. Lakini Lissu ananadi sera vizuri. Wakiendelea kusambaza hizi short videos za Lissu kwa wapiga kura kupitia Twitter, Facebook, Instagram na WhatsApp watawafikia mamilioni ya watanzania bila kuhitaji hayo mashindano ya nyomi. Siasa ni sayansi.......na cha muhimu ni Lissu aendelee kuwashawishi wapiga kura.......Na anafanya hiyo kazi vizuri.......

Pia sio vibaya Lisu na Membe wakifanya mdahalo kwenye TV maana Magufuli hawezi kukubali mdahalo, hasa ambao Lisu atakuwepo. Na kisha mdahalo huo upewe promo ya nguvu wiki moja kabla.
 
Leo Dar es salaam kulikwa na Tamasha la Mpira ya Yanga lenye kiingilio lakini Kampeni za Chadema hazikuwa na kiingilio ila wakazi wa Tabata Segera na Maeneo ya Jirani walioona Mechi ya Yanga ni muhimu kuliko ujumbe wa Lissu ni wengi sana..

Lissu alitakiwa ahudhuri uwanja wa Taifa, Tanzania hakuna kiongozi aliyewagusa mashabiki wa Yanga na Simba wanaishi nao.
Usiwapangie watu Cha kufanya kila mtu ana Uhuru wa kufanya anachotaka.

Kutokwenda kwenye mkutano sio kigezo Cha kutochagua anachokitaka.

Mwenyewe nilikuwa uwanjani taifa
 
Watanzania msiwafanye wajinga ila Mimi nimezunguka mikoa yote kuanzaia kusini mpaka kasikazini

Ukweli Ni kwamba watu wapo tayari kwa mabadiliko ila walikuwa wanasubiri ni nani analeta hayo mabadiliko?

Ila ukweli kwa Sasa watu wapo tayari kwa mabadiliko makubwa na Lissu ndio muarobaini wa huu utawala.
Niliwaza the same.
 
Kampeni inachangia sehemu ndogo sana katika uamuzi wa mpiga kura amuchague nani. Kama mpiga kura anafikiri kuwa hakuna athari yo yote aliyopata kwa miaka mitano iliyopita,hakuna namna ya kubadilisha msimamo wake. Katika mambo ya nchi wengi wape hadi pale watakapoelewa kwa nini mabadiliko yanahitajika sasa.

Ujinga ambao CCM imeulea ndiyo mtaji wake.
Lowassa kaondoka na wapiga Kura wake Kaondoka na Wapembe wake Kaondoka na wapenzi wake Kwa CHADEMA lazima mkubali DR SLAA was The Perfect Guy kuwavusha ila Tamaa na Uroho Wa Madaraka Umewacost Kumdaharau mtu wa familia na kualika mgeni tena mliemponda FISADI mkajua atawavusha Leo yuko wapina Hamtashinda uchaguzi hata Magu amalize Maika yake 10 maana kwa Sasa mkubali tu tunakamilisha Ratiba tu Nchi ishajua Rais ni nani ndio maana CCM hawangaki kufanya Kampeni kila ila siku MUNGU WA SLAA ATAAWADHIBU MPKA MKAMWOMBE MSAMAHAA SLAA
 
Mambo yanazidi kuwa matamu Mwanza CCM imefutwa
Mbona Niko apa mtaaa wajeshini maeneo ya bugando, naleo nimeshinda mjini na kazizangu niza hapahapa mtaaa wa ribeti, ccm imefutwa waapiii yaheeee. Badala ya kushauri mwali wenu anayelazimisha watanzania wampe urais kwa kisingizio cha kushambuliwaaa. Yaaaanii apewe uraisi kama kifuta machoziii.
Achakudanganya watuuuu bwasheee
 
Watanzania msiwafanye wajinga ila Mimi nimezunguka mikoa yote kuanzaia kusini mpaka kasikazini

Ukweli Ni kwamba watu wapo tayari kwa mabadiliko ila walikuwa wanasubiri ni nani analeta hayo mabadiliko?

Ila ukweli kwa Sasa watu wapo tayari kwa mabadiliko makubwa na Lissu ndio muarobaini wa huu utawala.
Hivi wewe mtu huwa una akili au ujinga kichwani! Hizi ndoto zako zinafubuza ukweli. Subiri uchaguzi uone JPM anavyopendwa! Lissu anapwaya
 
Pia sio vibaya Lisu na Membe wakifanya mdahalo kwenye TV maana Magufuli hawezi kukubali mdahalo, hasa ambao Lisu atakuwepo. Na kisha mdahalo huo upewe promo ya nguvu wiki moja kabla.
Yaani strategy ya pamoja kati ya Chadema na ACT ni muhimu mno. Kwenda mbele upinzani unahitaji kufanya ubunifu mwingi kuinua hamasa kwenye mambo ya siasa na kampeni za uchaguzi huu mkuu........
 
Jamani mbona ushauri umekuwa mwingi, na hekima za kumwaga kuna nini?
 
Leo Dar es salaam kulikwa na Tamasha la Mpira ya Yanga lenye kiingilio lakini Kampeni za Chadema hazikuwa na kiingilio ila wakazi wa Tabata Segera na Maeneo ya Jirani walioona Mechi ya Yanga ni muhimu kuliko ujumbe wa Lissu ni wengi sana..

Lissu alitakiwa ahudhuri uwanja wa Taifa, Tanzania hakuna kiongozi aliyewagusa mashabiki wa Yanga na Simba wanaishi nao.
Huko uwanjani, mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz alisikika akisema kwenye kipaza sauti "Magufuli Mitano Tenaaaaa" unadhani wewe ndio ungekuwa Lissu na upo uwanjani ungejisikiaje? Wao wana intelijensia yao pia, inawaeleza ukweli wa mambo ulivyo. Sio wajinga hata kidogo.
 
Mbona Niko apa mtaaa wajeshini maeneo ya bugando, naleo nimeshinda mjini na kazizangu niza hapahapa mtaaa wa ribeti, ccm imefutwa waapiii yaheeee. Badala ya kushauri mwali wenu anayelazimisha watanzania wampe urais kwa kisingizio cha kushambuliwaaa. Yaaaanii apewe uraisi kama kifuta machoziii.
Achakudanganya watuuuu bwasheee
Ninyi Wazinza mko wachache sana hapa Mwanza Sisi Wasukuma na Wakurya na Waha ndio tunalifanya Mwanza lionekane jiji

Ninyi rudini Visiwani mkakabane makoo na na hao maafsaa wenyekufuatilia ukubwa wa samaki
 
Back
Top Bottom