Ushauri kwa wadada wote wanaotumia rangi ya mdomo, zina madhara

Emok Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2018
Posts
1,094
Reaction score
800

Salamu zenu wana JF,

Leo nataka niwaelimishe wadada wanaopenda kupaka lipsticks mdomoni moja ya vitu vinavyounda lipsticks ni heavy metals kama vile mercury na silver.

Madhara yake ni nini?
Mwili wa binadamu una protein ambayo hutengeneza kinga za mwili( antibodies). Sasa hizo heavy metals zinaharibu( denature) protein na enzymes.

Hivyo basi baada ya muda binti unaanza kusumbuliwa na maradhi ya ajabu ajabu kama cancer.

Hitimisho: Wadada muache kutumia hizi lipsticks no hatari kwa afya zenu.Pia mwanaume muokoe mpenzi wako kwa kumkataza kutumia lipsticks

Alternative: lamba lamba lips zako au paka mafuta ya ALIZETI.

Asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
 
Mmh! Mie bado kushawishika kuacha kwa kweli sababu mizunguko yangu yote lazima lipstick ihusike.

Mie nadhani mtushauri tusipake mara kwa mara na sio kuacha kabisa sababu mkisema tuache tofauti ya mdomo wa mwanaume na mwanamke itakuwa wapi.
 
Mmh! Mie bado kushawishika kuacha kwa kweli sababu mitoko yangu yote lazima lipstick ihusike.

Mie nadhani mtushauri tusipake mara kwa mara na sio kuacha kabisa sababu mkisema tuache tofauti ya mdomo wa mwanaume na mwanamke itakuwa wapi.
Sawa punguza,

Lakini tofauti ya mwanaume na mwanamke haipo kwenye kupaka lipstick ndugu yangu[emoji23] [emoji23]
 
Mmh! Mie bado kushawishika kuacha kwa kweli sababu mitoko yangu yote lazima lipstick ihusike.

Mie nadhani mtushauri tusipake mara kwa mara na sio kuacha kabisa sababu mkisema tuache tofauti ya mdomo wa mwanaume na mwanamke itakuwa wapi.
Hilo neno Mitoko au Utoko kwa wengine wajuao Kiswahili ni matusi
 
Hahahaaa. Kama ipi sasa ikiwa kila mmoja mdomo wake mkavu?
Paka mafuta chora na wanja ni basi tu wanaume hawana nongwa ila mtu unamkuta na domo jekunduu km kidonda siwasemi ubaya sema ukiwa tu msafi inatosha hayo ma lipstick hata sio kiviiile.
 
Dunia ya sasa tutaacha kila kitu[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Itakuwa mwali akija kabla ya mambo yetu yale unamuosha lipsi kwanza[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Lipstick ni kiboko kwa kuharibu ndoa za watu hasa wanaume wachepukaju,akienda kwa kimwali kingine kinamkiss begani haha akirudi kwa mkewe anaulizwa hii lipstick kwenye shati umetoa wapi,na hapo ndo vita ya tatu ya dunia inapoanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…