Asalam,
Nilifuatilia sana suala la kesi iliyofunguliwa na hawa mawakili. Nikafuatilia hukumu na baada ya hukumu nikajipa muda kufuatilia mitazamo, uelewa, na mipango ya wafungua kesi. Huu ndio ushauri wangu.
1. Zamani sio kama sasa, hasa kwa taifa lililopevuka kama Tanzania, TUHESHIMU TAASISI NA MFIFUMO YAKE.
... mara baada ya ile hukumu mawakili waliosimamia kesi walitoa matamko mawili, la kwanza kama mawakili na la pili ( kwa maelezo ya Wakili Mwambukusi) kama watanganyika. La kwanza lilikuwa sawa, la pili linahitaji washauriwe namna ya kwenda nalo, kinyume chake watakufa kabla ya kutimiza malengo yao.
Wachina wana hekima hii "maliza jambo moja kwanza kabla ya kuanza jingine" na mimi walau ningepata nafasi ningewashauri Wakili Mwambukusi na wengine wamalize kwanza suala la Rufaa ya Kesi waliyofungua kabla ya kutangaza mikakati mingine ya mbeleni au jambo jipya. Hii kanuni sio tu kwa masuala mapana kama haya lkn hata katika maisha binafsi.
Mara baada ya kumsikiliza wakili Mwambukusi nilipata mashaka sana juu ya uelewa wake wa siasa za Tz na akili yangu ikapata hofu kutaka kuamini maneno ya wapinzani wake kuwa muda mwingi huwa kapiga vyombo na jani.
Tanzania inaongozwa na Taasisi. Taasisi ni nzuri zikiwa na watu wema. Ni mbaya zikiwa na watu wabaya. Hii ni bila kujali wanafuata sheria au lah. Kuna suala la kufuata sheria lkn kuna suala la tunu ( virtue). Kwa Tanzania siasa vimepewa vyama na sio mtu binafsi. Walioweka hilo wanajua. Mwambukusi lazima aingie kwenye Chama flan. Hapa napo mtaona tatizo.
2. Heshma kwa viongozi. Pamoja na mengine sana yenye Changamoto, yako yanayopaswa kulindwa. Kuna tofauti ya kukosoa kazi za Bunge na kumkosoa utu wake mbunge mmoja mmoja au Spika. Hapa waliyumba na haipaswi. Inatakiwa kujenga hoja juu ya hoja na sio hoja juu ya mtu labda kama jambo binafsi la mtu linaingilia kimaslahi na jambo husika. Huwezi kuamka asbh ukasema mkuu wangu wa eneo la kazi hana akili, huku ni kutojipa kazi za kutosha. Chambua mwenye akili au asie na akili alifikaje hapo.
3. Wasitafute umaarufu binafsi. Umaarufu binafsi katafute kwa kufanya biashara. Taasisi zina nguvu kuliko mtu mmoja mmoja kwenye Siasa. Chama cha siasa kina watu, kinaweza kuamua kuandamana au lah.
4. Wapime uelewa wa wanaowatetea. Hakuna maana kufa kwajili ya mtu mjinga ambae hajui unamfia kwa lipi. Wakili mwambukusi na wengine wake wapime wanampigania nani, na huyo nani anaelewa ni kwa kiasi gani wana pambana. Inawezekana wanapigania jambo ambalo hata halina maana.
5. Wao na hawa wengine CHADEMA watambue kuwa CCM HAITOTOKA MADARAKANI SASA. Haliwezi kutokea hilo kwa Tanzania. Chadema wanajua, act wanajua, na kila mmoja anajua. La kufanya ni kujaribu kutafuta namna ya Amani ya kuishauri CCM KUFANYA MAMBO VEMA.
6. Tuendelee khiombea amani, utulivu na Umoja nchi yetu