GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nimehudhuria ibada za Wasabato mara kadhaa. Mara zote nimeona msisitizo mkuu wa mahubiri yao ni kuhusu siku ya Sabato.
Lakini pia niliona kuwa mahubiri yao kwa sehemu kubwa yanatoka kwenye vitabu vya Agano la Kale.
Hakuna ubaya kwa mahubiri kutoka kwenye Agano la Kale, lakini endapo hawasomi vitabu vya Agano Jipya, hasa Nyaraka (Epistles), watakuwa wakijipunja sana kwa hasara yao wenyewe bila wao kujua kuwa wanapunjika mno. Wanaweza wakajidanganya, wakadanganya, na hata kudanganywa kirahisi bila wao kujua kuwa wamepotoka, wanapotosha, na wanapotoshwa.
Kwa sababu ya kutokusoma vitabu vya Agano Jipya, wengi wamekuwa wakiyafuata mapokeo ambayo kimsingi hayawasaidii kiroho.
Nitoe ushauri kwa kila Msabato na mtu mwingine yeyote anayetaka kufahamu jinsi Mkristo anavyopaswa kuishi, ajitahidi kusoma vitabu vya Biblia vya Agano Jipya, hasa Nyaraka.
Hivi ndivyo vitabu vya Nyaraka vya kwenye Biblia: Warumi, 1Wakorintho, 2Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1Wathesalonike, 2Wathesalonike, 1Timotheo, 2Timotheo, Tito, Filemoni, Waebrania, Yakobo, 1 Petro, 2Peteo 1Yohana, 2Yohana, 3Yohana, na Yuda.
Akishamaliza hivyo, avisome vitabu vya Injili pamoja na Matendo.
Baada ya hapo sasa, ndipo asome kitabu cha Ufunuo ikifuatiwa na vitabu vyote vya Agano la Kale kuanzia Mwanzo hadi Malaki.
Kwa msingi huo, atakuwa ameshavisoma vitabu vyote vya Biblia hivyo kutamfanya ang'amue utofauti wa maisha ya Agano la Kale na Agano Jipya.
Lakini kama atapaswa kusoma vitabu vichache tu, basi asome vitabu vya Nyaraka!
Kwa nini Nyaraka? Kwa sababu ndizo zenye mwongozo wa maisha ya Mkristo.
Kama mtu hajasoma vitabu vya Nyaraka, anaweza akawa anajitahidi kuyaishi maisha ya Agano la Kale kwenye kipindi cha Agano Jipya, jambo ambalo haliwezekani. Ataishaia tu kuvunjika moyo.