Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Nimekuwa nikiitafakari sana hii adhabu ya viboko mashuleni kila ninapoona taarifa ya mwanafunzi kuumizwa na mwalimu kichukuliwa hatua kwa kumuumiza mwanafunzi
Ni wazi kwamba kuna wagonjwa wengi wanakufa hospitali kwa uzembe wa madaktari, kuna abiri wengi wanakufa kwa ajiri kwa uzembe wa madereva, kuna vibaka wengi wanafanya uharifu mtaani kwa uzembe wa polisi na kuna watu wengi wamefungwa gerezani bila makosa kwa uzembe wa wapelelezi na wanasheria.
Hata hivyo kelele za malalamiko ya jamii juu ya hizo kada nyingine si sawa na kelele za jamii pale mwalimu anapomuumiza mwanafunzi kwa adhabu ya viboko. Jamii itaongea, itatukana, itatoa dhihaka na viongozi watachukua hatua
Ifahamike kwamba siandiki haya kwa kujaribu kutetea wala kuunga au kuwatetea walimu wanaotoa adhabu ya viboko kupitiliza na kinyume na utaratibu. Binafsi naamini adhabu ya viboko haifai na imepitwa na wakati mashuleni.
Ukisoma sheria ya utoaji adhabu ya viboko shuleni na muongozo wake utaungana na mimi kuwa hii adhabu imepitwa na wakati na haifai kuendelea kutolewa mashuleni kwasababu ni ya mtego kwa walimu na endapo wazazi na wanafunzi wangekuwa makini na sheria hii walimu wengi wangekuwa gerezani
Kwa mfano; mwongozo unataka kwa kosa kubwa mwanafunzi aadhibiwe fimbo nne tu tena anayetakiwa kuadhibu ni Mkuu wa shule.
Hapa kwenye fimbo nne kwa kosa kubwa! Ikumbukwe wanafunzi wengi wanaadhibiwa kwa makosa ya uchelewaji, utoro, kupiga kelele, kutoandika nukuu. Haya yote sio makosa makubwa yanayostahili adhabu ya fimbo. Hapa mwanafunzi anatakiwa kuonywa na kushauriwa tu.
Kuna baadhi ya wanafunzi ni jeuri, wana lugha za matusi, wanavuta bangi, na ukorofi mwingine wa ujana kiasi wanawapandisha hasira walimu kwa makusudi. Unategemea mwanafunzi anayempandishia mwalimu, anayeweza kumtukana au kumvimbia mwalimu asichapwe fimbo zaidi ya nne na achapwe na mkuu wa shule tu au ili mwalimu mwingine amchape fimbo apewe kibali cha maandishi kufanya hivyo.
Hapa unajiuliza, ni walimu wangapi wanauvumilivu huo? Watavumilia kwa muda gani?
Kwa hiyo hapa utagundua kuwa ni kama hii adhabu ilishafutwa ila haijatolewa tamko tu.
Ushauri wangu ni kuwa wizara ifute kabisa adhabu ya viboko ili walimu wawe salama na wanafunzi watakaovunja sheria za shule watafutiwe utaratibu mwingine
Binafsi naamini tukijenga utamaduni wa kutochapa fimbo shuleni wanafunzi watazoea, walimu watazoea na wazazi watazoea na kizuri zaidi wanafunzi wakorofi adhabu yao ikiwa ya kufukuzwa shule na kutafutiwa utaratibu mwingine itawajenga kujiepusha na makosa ya mara kwa mara kuliko hizi fimbo wanazochapwa mara kwa mara