Ushauri: Lwandamila afukuzwe haraka sana Yanga

Tulieni safari bado ndefu!
Ya kwenu imeshafika tamati
Yaani labda muwe vibaraka. Chura wapo bandarini kwenye safari ya kuelekea Jangwani.
Yaani mtu kapigwa ngumi yuko chini anasema ungenipiga kichwa. Wewe uliona wapi mfungwa anachagua adhabu na jela?Hiyo ni kazi ya hakimu (Simba).Ukipewa amri unalala na usingizi huna. Ndio adha ya kuwa mfungwa.
 
Jamani Wanayanga wenzangu hili nililisema tokea mwanzo,sikuridhia kabisa suala la kumtoa Pluijm na kumleta huyu Mzambia.

Niliwaambia kabisa hofu yangu ni kubwa,haya sasa mambo mnayaona.
cc Guasa Amboni nasmapesa mgaagaa na upwa na wengine wote tuliojadili kuhusu suala la ujio wa kocha mpya kwenye mechi za mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara.
 

1.Juzi wakati mabao ya spid ya 4G yakiwa yanafungwa hamkusema hayo

2. Kumbuka , kocha hukumuana hata mara moja anasimama ama kutoa maelekezo zaidi ya jukumu hilo kuchukuliwa na mwambusi , unadhani itakuwa hivyo daima?

3. Alitumia mashindano haya , kusoma ligi za bongo na kuwajua vizuri wachezaji wake , ubora na mapungufu yao, na amemaliza research sasa subiri ligi ndio utamjua vizuri.
 
Sisi ndio mabigwa wenu kumbuka so muwe na adabu! Acha kuchanganya siasa na mpira! !
 
wewe.umemfukuza nani toka uzaliwe?
 
Wewe ni mmoja kati ya wale Yanga-left wing. BTW poleni kwa vipigo vizito mlivyoshushiwa wiki. Hivi vipigo sio vya nchi hii
 
Yaani watu akili mbovu kocha afukuzwe bonanza ambalo lipo kisiasa sana mbona timu inacheza vizuri wakati wa babu time ilikuwa dk ya 70 inakata moto
 
Maneno yako Nifah hayajaanguka chini hakukuwa na sababu timu inafanya vizuri kisha kubadilisha kocha imekuwa mlima mkubwa kwetu kuupanda nakuunga mkono hapa . Wacha tujipange hakuna namna waliofanya maamuzi watakuwa wanajuta sisi huku wanatulaza mapema .
 
Hakika mkuu naumia sana! Sidhani kama maumivu haya yataisha leo wala kesho.
Juzi jumapili nilitoka na Niqab nyumbani maana sithubutu kukatiza kitaa najisikia aibu sana,sasa kesho sijui nauweka wapi uso wangu.

Hadi leo kwa mara ya kwanza maishani nimeacha kupokea simu ya baba yangu mpenzi (yeye ni Mzee wa Msimbazi)
Imeniuma sana [emoji24].
 
Mm naunga mkono hoja!
Haiwezekani mm shabiki niingie uwanjani nikae na kocha akae tuuuu dk90!
Wakati ndio kazi yake na huifanya mara1 kwa wiki.
Iweje ashindwe kusima hata dk 40 kati ya 90? Kwa kuwa tia nia na moyo wachezaji na kuwapa techniques mbalimbali kulingana na mabadikiliko ya uwanjani (mchezo).

Tatizo anajiona kuwa uongozi wa Yanga ndio unamuabudu kama Mungu.
Ame ajiriwa kwa utaratibu wa hovyo sn, kacheza rafu kwa Puljin afu Matokeo ni mkojo wa Kuku!!
Fukuza huyu jamaa. Bora Puljin
 
Pole bibie hapana pokea simu ya mzazi yeye anathamani kubwa kuliko hicho ambacho mnakinzana wengi tulipata khofu na kutabiri madhira haya na kweli yametokea piga moyo konde ni sehemu ya mchezo tena basi hakuna raha kama kuumia kwa unachokipenda hapo unadhihirisha upenzi wako ulio TUKUKA kwa timu yetu once again pole dada yangu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…