Nadhani wewe ndio una primitive thinking, au ndo nyie mnawaza ukioa aliye na uwezo atakusaidia maisha?? Maisha mwanaume hasaidiwi anapambana, mke wangu nimemuona akiwa anamalizia mwaka wake mwisho chuo na ni mhasibu aliyeajiliwa Sasa, na rafiki zake wote aliosoma nao tumeshakula ubwabwa yaanii wameolewa Sasa sijui wanafunzi gani wa chuo ambao hawataki kuolewa, hayo mawazo ya kwamba eti mwanamke kuolewa anatafuta unafuu wa maisha ni mawazo ya kijinga Sana, mbona hao wanaume wanaoa wengine hata mahari wanasaidiwa na wanawake hao hao, Kwani hujaona wanaume nao wanataka kuoa wanawake wenye pesa hao wanawake nao watakuwa wanatafuta unafuu wa maisha?? Hebu amka usingizi mkuu, kama wa kwako alisema anataka kuolewa na wewe Kwa sababu ya maisha usisemee wote, halafu suala la kusema eti wanakuja wamechoka nani anawachosha?? Kama huoni haja ya kuoa na usioe.