Ushauri: Mahari ifutwe?

Ushauri: Mahari ifutwe?

Daah hiili suala linahuzunisha sana kuna Jamaa Jana alikua anasimulia ameshindwa kuoa sababu ya Mahari yaani unaambiwa ukweni walimwambia alipe Million 2 na Laki 5, shughuli anazofanya na malipo ya mahari haviendani kabisa hivyo amebaki kuishi uchumba sugu huu mwaka wa 10 bado hajaoa mke kashamzalisha watoto watatu ila ndoa hawajafunga kisa Mahari parefu

Mahari hizi au vikwazo vya kutokuoa?
Mwambie kijana atafute mshenga anajua kuongea vizur ili kuweka asante yako kwa wazazi mkononi.
Mahali ni utamanduni ,ni heshima kubwa kwa wazazi pande zote mbili na ni heshima kwa yule unayemwooa,pia ni asante kwa wazazi
 
Wanawake umewaona wameolewa kifua kimesimama [emoji23][emoji23][emoji23]. Amechezewa na watu zaidi ya ya wanne ndio anakuja kuolewa, leo useme amekuja kwangu kwaajili ya ndoa ilihali wanatafuta unafuu wa maisha. Mabinti wangapi walioolewa uliona wanauwezo wakimaisha wakati wamesimama hawajui waende wapi. Kamuulize binti aliyetoka chuoni kama anataka ndoa, atakwambia, I want to develop my carrier na kuwastable ila ndoa sio mpango, subiri 1 to 2 years uone atakujibu nini maana wanakuwa wameweka mwanaume kama contingency plan baada ya maisha au ajira kuwakataa. Kijana, wanaume tunaishi kwenye hii hii jamii tuliochanganyikana na wanawake hivyo ujue wao sio malaika na siwatakatifu ni binadamu tu. Usitetee point kwakumkweza mtu fulani ili aonekane yeye ni bora huo ni ukosaji wa maarifa. Watu wanafanya hadi upumbavu mpaka tushaanza tusiulizane yaliyopita tugange yajayo leo useme eti chuchu saa sita. Njoo uone mabinti wanavyotoa mimba hospitalini. Acha primitive thinking.
Tatizo mtoto wa kiume n mharibifu!
 
mahari iwepo tena iwe kubwa
mahari ndogo kabisa iwe ng'ombe 5 zilizoshiba vizur
hawa vijana wasiotaka kujishugulisha wasioe kama wanatarajia mtelezo had kweny mahari
 
Kwa jinsi ulivyoeleza tukio hilo hiyo "mahari" iliyokuwa ikidaiwa siyo Mahari bali ni bei ya kumnunua huyo binti.

Katika dini ya kiisilamu Mahari huwa ni fedha au mali inayotolewa na muoaji kwa ajili ya muolewaji na hiyo mali inakuwa ni mali ya muolewaji na sio vinginevyo, kama ikibidi wazazi na jamaa wengine wapewe kiasi cha hiyo mahari basi ni jukumu na muolewaji kuridhia kuwapa hao wazazi au ndugu.

Hapo sasa utaona mahari inakuwa sio Bei bali ni zawadi ya upendo kwa muolewaji kutoka kwa muoaji.
 
Kwahiyo kwa akili zako kusomesha ndio kibari cha mzazi kuomba Mahari?
Mahari imewekwa kama shukran kwa muhusika baada ya kulelewa na kutunzwa nyumbani kwao toka anakuwa we unadhani hyo million moja ndo umemaliza gharama za malezi za aliyekutunzia mke hapo sijaongelea wale waliosomeshwa naongelea hawa kina mwajuma wa mbagala yaani ulelewe mke halafu umchukue bure kwanza ndoa isingekuwa na thamani na visa vya kuachana vingekuwa vingi si unajua akizingua unavuta tu.
 
Tukitaka jamii iharibike basi tuondoe mahari. Hakutakuwa na heshima yoyote kwenye ndoa. Mahari ni binding factor
 
Nadhani wewe ndio una primitive thinking, au ndo nyie mnawaza ukioa aliye na uwezo atakusaidia maisha?? Maisha mwanaume hasaidiwi anapambana, mke wangu nimemuona akiwa anamalizia mwaka wake mwisho chuo na ni mhasibu aliyeajiliwa Sasa, na rafiki zake wote aliosoma nao tumeshakula ubwabwa yaanii wameolewa Sasa sijui wanafunzi gani wa chuo ambao hawataki kuolewa, hayo mawazo ya kwamba eti mwanamke kuolewa anatafuta unafuu wa maisha ni mawazo ya kijinga Sana, mbona hao wanaume wanaoa wengine hata mahari wanasaidiwa na wanawake hao hao, Kwani hujaona wanaume nao wanataka kuoa wanawake wenye pesa hao wanawake nao watakuwa wanatafuta unafuu wa maisha?? Hebu amka usingizi mkuu, kama wa kwako alisema anataka kuolewa na wewe Kwa sababu ya maisha usisemee wote, halafu suala la kusema eti wanakuja wamechoka nani anawachosha?? Kama huoni haja ya kuoa na usioe.
Umechanganya mafaili mkuu
 
Mahali ni utaratibu tu ambao mi nauona ni wa kimahusiano zaidi, Kwa mfano sisi waislam Kuna familia wanakuambia lete tu mbuzi, 50k, 100k kitu ambacho is incomparable to mambo ambayo yatakuja yazalishe haimuzi hata
 
Back
Top Bottom