Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

!
!
Moja ya uteuzi wa Ovyo kabisa kuwahi kifanywa na mtukufu Mtakatifu Baba Jesika.
Anyway acha niisome namba. Nitafanyaje sasa wakati wife kaniponza.
 
Tutamvumilia a-fail mara ngapi? Hakuna nafasi ya kujifunza ofisi za umma!

Hata marais wote waliopita Marekani kuna vitu walifeli na wengine wamejifunza kutokakwao ndio maana ya kuwepo maisha na ndio maana ya 'dynamism'. Nyerere alifeli nae alikiri, hata Mungu nae alifeli kwa kumuumba Shetani na hapo ndipo maisha yetu yakawa, maisha yanaanza kwa kufeli
 
Ni Mtazamo wangu tu.

Nikimtazama RC Paul Makonda naona nyota yake kiuongozi inazidi Kung'aa na ni imani yangu kama CCM itaendelea kukaa madarakani atazidi kwenda juu kiuongozi maana kuna vitu anafanya yeye baadae inakuwa maamuzi kwa waandamizi wake. Baadhi ya mambo yanayonifanya niwaze ni haya:
1. Ndio mtu wa kwanza kupendekeza hadharani Mh. Samia Suluhu awe makamu wa raisi (Kumbuka bunge la katiba) na kweli imekuwa hivyo

2. Alimpinga Mh. Lowasa hadharani kwamba hawezi kupewa nafasi ya kugombea uraisi ndani ya CCM kweli imekuwa hivyo. ( kumbuka tamko lake akiwa kiongozi wa uvccm)

3. Pamoja na kwamba watu walimtabiria kuondolewa u-dc baada ya JPM kuwa president hali ikawa tofauti, kwani ndiye mtu pekee aliyehakikishiwa kupanda cheo kuwa RC na JPM wakati akiongea na wazee wa dar mapema alipoingia ikulu.

4.Ndio kiongozi aliyejaribu kumaliza mgomo wa madereva wa mabasi ya mkoani mwaka jana tena akiwa kama DC wa kinondoni japo sina hakika na makubaliano yaliyoafikiwa wakati ule kama yameshatekelezwa.

5.Juzi kapiga marufuku matumizi ya shisha Dar muda mfupi baadae waziri mkuu katangaza kuipiga marukufu nchi nzima.

TAKE NOTE:
sijasema msimamo wangu kuhusu uwezo wake kiutendaji au kumkubali kwangu.

ARM[emoji767]2016
 
Not deliberate kufeli, unashauriwa hutaki, unakuwa kiburi etc
 
Leo akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya amewaagiza wakapambane na omba omba kwenye wilaya zao. Hili linashangaza sana! Hivi ombaomba, madada poa, wabwia shisha na mashoga ndo matatizo ya Jiji la Dar? Au anatafutia umaarufu tu?

Tatizo kubwa kuliko yote hapa Dar ni msongamano wa magari, tatizo sugu la maji, uchafu ambao hata ofisi yake na maeneo yake ni machafu! Hivi huyu aliyeanzisha program ya usafi aka-fail, program ya usalama aka-fail, walimu kusafiri bure aka-fail, machangudoa aka-fail ndo ataweza omba omba?

Si amuulize mzee Makamba aliyempa Matonya nauli akarudi Dodoma akaondoka kwenye ukuu wa mkoa akamuacha. Amuulize mzee wa watu alivotaka kuwaondoa madada poa aliambulia majina gani. Hii inaonyesha jinsi gani wakuu wa mikoa hawana kazi maana anajua wapo wanaofikiria maji, barabara na miundombinu kwa ujumla, afya, elimu, nishati nk.
safari ya maili elfu moja inaanza na hatua moja.
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.

Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi, wavuta shisha wote mtetezi wao ni chadema!!!
Chadema/ukawa imeingiaje hpo au ndiyo cdm imekukaa.....isijetokea ukagegedewa dem Wko alafu unakja itupia lawama cdm.....
Nkirudi kwenye mada ukweli iko Hapo Hapo huu Mkuu wa mkoa my a Vitu muhimu na vya msingi kufatilia jiji lina changamoto nyingi Kama usafi,miundombinu mibovu ya barabara,ujenzi holela watu kuzibaa vichochoro
Etc
Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
 
Hilo la 'deliberate' siwezi kulisemea, nimelisemea lile uliloandika mwanzo. Mimi naamini kabisa maisha yanaanza na kufeli. Uvumbuzi mwingi, mawazo mapya mengi yametokana na kufeli kwa jambo fulani. We chunguza nafikiria maisha ya binadamu kuanzia kwenye dini, mataifa makubwa, Organization kubwa za dunia, you just think critically unbiased utagundua na unaweza kumgundua mtu uliyemuheshimu sana kuwa amefika hapo alipo kumbe baada ya kufeli katika jambo fulani
 
Muheshimiwa mtukufu, kijana hodari na mchapakazi Comredi Paul Makonda leo naongea wewe,

Nikiwa kama mkaazi na mzaliwa wa Jiji hili tangu likiitwa Mzizima napenda leo niungane na wewe kupiga vita vitendo vya ushoga na kupambana na element zote za ushoga, lakini nimebaini vita yetu hii imeshaferi kabla hatujainza, maana kila nikiwaangalia watoto zetu huku mtaani wanampenda sana Joti wa Ze Comedy, sasa shida inakuja kwa huyu Joti kuimudu vyema nafasi ya kuigiza kama shangingi la mjini lililokubuhu, sasa huoni hii vita yetu ya kupambana na ushoga tayari inakwamishwa na kina Joti?

Kwakuwa sina muda wa kukuletea hili ofisini lakini nimeona wewe ni active member wa hapa JF na utapita na kusoma uzi huu ili tujuwe tunamdhibiti vipi Joti kwanza ili kuokoa vijana wetu ambao wanamkubali sana?

Karibuni wadau tutafute ufumbuzi wa swala hili kwanza kwa maoni ni nini kifanyike?
 
Mmmmmmh Akili zingine Bhana. utawalipa Wewe Hao The Comedy
 
Nachelea atachukua ushauri wako,lakini kama maagizo na amri zake nyingine itaishia hewani
Tunasubiri lianze kujengwa lile jengo la wazazi la ghorofa tatu alilotutangazia kwa mbwembwe nyingi kujengwa Mwananyamala
Barabara zote za Dar kukarabatiwa mara mmoja tunasubiri
 
Ni Mtazamo wangu tu.

Nikimtazama RC Paul Makonda naona nyota yake kiuongozi inazidi Kung'aa na ni imani yangu kama CCM itaendelea kukaa madarakani atazidi kwenda juu kiuongozi maana kuna vitu anafanya yeye baadae inakuwa maamuzi kwa waandamizi wake. Baadhi ya mambo yanayonifanya niwaze ni haya:
1. Ndio mtu wa kwanza kupendekeza hadharani Mh. Samia Suluhu awe makamu wa raisi (Kumbuka bunge la katiba) na kweli imekuwa hivyo

2. Alimpinga Mh. Lowasa hadharani kwamba hawezi kupewa nafasi ya kugombea uraisi ndani ya CCM kweli imekuwa hivyo. ( kumbuka tamko lake akiwa kiongozi wa uvccm)

3. Pamoja na kwamba watu walimtabiria kuondolewa u-dc baada ya JPM kuwa president hali ikawa tofauti, kwani ndiye mtu pekee aliyehakikishiwa kupanda cheo kuwa RC na JPM wakati akiongea na wazee wa dar mapema alipoingia ikulu.

4.Ndio kiongozi aliyejaribu kumaliza mgomo wa madereva wa mabasi ya mkoani mwaka jana tena akiwa kama DC wa kinondoni japo sina hakika na makubaliano yaliyoafikiwa wakati ule kama yameshatekelezwa.

5.Juzi kapiga marufuku matumizi ya shisha Dar muda mfupi baadae waziri mkuu katangaza kuipiga marukufu nchi nzima.

TAKE NOTE:
sijasema msimamo wangu kuhusu uwezo wake kiutendaji au kumkubali kwangu.

ARM[emoji767]2016

Sasa wewe mkuu tatizo lako ni nn hasa kuhusu utendaji wa RC -Dar
 
Muheshimiwa mtukufu, kijana hodari na mchapakazi Comredi Paul Makonda leo naongea wewe,

Nikiwa kama mkaazi na mzaliwa wa Jiji hili tangu likiitwa Mzizima napenda leo niungane na wewe kupiga vita vitendo vya ushoga na kupambana na element zote za ushoga, lakini nimebaini vita yetu hii imeshaferi kabla hatujainza, maana kila nikiwaangalia watoto zetu huku mtaani wanampenda sana Joti wa Ze Comedy, sasa shida inakuja kwa huyu Joti kuimudu vyema nafasi ya kuigiza kama shangingi la mjini lililokubuhu, sasa huoni hii vita yetu ya kupambana na ushoga tayari inakwamishwa na kina Joti?

Kwakuwa sina muda wa kukuletea hili ofisini lakini nimeona wewe ni active member wa hapa JF na utapita na kusoma uzi huu ili tujuwe tunamdhibiti vipi Joti kwanza ili kuokoa vijana wetu ambao wanamkubali sana?

Karibuni wadau tutafute ufumbuzi wa swala hili kwanza kwa maoni ni nini kifanyike?

Hujafikiria kama hao watoto wanaweza kuhamia Kibaha...........
 
Kwahiyo unamaanisha RC Makonda ndio mtoa maamuzi au? Maana nakumbuka pia marehemu Kabwe alifukuzwa kazi na Mr. President baada ya Makonda kuongea.
 
Eti... Naskia eti Simba akikosa kitoweo, Eti... Simba huyo huyo anaweza akakula hata nyasi eti lakini...[emoji13] [emoji23]
 
Back
Top Bottom