Mkuu
lusungo shukrani kwa kuleta huu uzi.
izzo mkuu endelea na moyo huo huo pamoja na wadau wote mliochangia humu.
Kuna mambo nimejifunza mengi sana na kwa huu uzi nimefufua ndoto ya kwenda ulaya. Nakumbuka wakati nipo sekondari kuna wazungu walikua wanakuja shule, kipindi hicho nina upako wa kiingereza yes no what when zilikuwepo kwa wingi. Mimi sikujua kwamba ile ilikua ni fursa ya kwenda ulaya. Nimesoma huu uzi nikakumbuka kama ningejiongeza ningekua nipo huko.
Kwa kupitia nondo za huku kuna mambo nimeyagundua, kwanza ukiwa na nia utafanikiwa. Pia kwenda ulaya sio jambo kubwa sana ila mikakati ya nguvu inatakiwa.
Mkuu
izzo kaleta plan za kwenda huko, kwa kupitia Malta na ku_host wageni toka ulaya. Ila kwa upande wangu nimejiwekea mpango mkakati wa miaka 2 ili nifanikiwe.. [HASHTAG]#RoadtoEurope[/HASHTAG]..!!
1. Naanza kwa kutafuta
Passport, ikae tuu ndani maana ndio kitu cha muhimu. Wadau wameshaatoa njia ya kuipata naamini nitaipata.
2.
Nauli, hapa ndio mziki ulipo. Nauli ndio kila kitu, lazima niitafute. Japo sina kazi ila ndani ya miaka hiyo 2 najua itaeleweka
3.
Kiingereza, japo cha kuombea maji kipo ila kukiongeza zaidi inanipasa. Sio unaongea na mtu unaanza kusearch vocabulary mojamoja kichwani.
4.
Scholarship, japo kwa sisi wenye diploma zinakua ngumu na chache ila nitaanza kuzitafuta kwa udi na uvumba. Zile mb za kuangalia Messi's skills au Ronaldo's skills youtube nitazitumia kutafutia scholarship.
5. Kutafuta demu mzungu aliyepo Ulaya kwa kupitia online dating sites. Najua wazungu akikupenda anakupenda kweli, akijilengesha mmoja hana bahati. Namng'ang'ania kama kupe hata kwa ndumba itabidi 😛.
Naamini Mwenyenzi Mungu atasaidia na mimi niende Ulaya siku moja, aliyewezesha wengine wawepo na mimi atanisaidia.
Wakuu msisite kutoa miongozo, mbinu, nafasi ya kutusaidia na sisi tuweze kwenda huko wanapopaita Ulaya.
[HASHTAG]#RoadtoUlaya[/HASHTAG]......🙂🙂🙂🙂