Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ukiachana na migodini, kuna fursa zipi kule bondeni umeziona
Kule bondeni fursa nilizoziona kwanza ni biashara ndogondogo ni rahisi kufanya kama kuuza mabegi soksi nk pia wageni wengi wanafanya biashara za barber shop, kazi za mahotelini hasa upishi wanalipa vizuri na kazi za dox kwenye meli zinazofanyiwa marekebisho niliona wabongo wengi wakifanya kazi huko upande wa safety kama firefighter but hazilipi vizuri labda upate kwenye meli za uvuvi mnaweza kukaa hata mwezi huko baharini na wakirudi huwa wanalipwa vizuri na kuna wenzetu kama warundi wakongo wao naona wanafanya sana kazi za ulinzi
 
Yeah thanks
Mkuu hao watu huwa nakutana nao sana hata kwenye kuomba scholarship, na wengine wa Nigeria kuhusu cjui kafiwa na wazazi wote so hakunipa shida
Ila Kingine they are so fasta km haupo makini unaliwa kweli ila ukisoma email na ukiconnect dots unajua kabisa hapa ni uongo
Walinipigia nikaanza kumuuliza huyo agent wacha aanze kujikanyaga
Nikabaki nacheka tuu
Ila sijakata tamaa nita apply tena na tena
 
Mrejesho wapendwa
Nilipo tumbo la kuendesha limenipata,ananitaka niwe New Zealand tarehe 30 mwezi huu
Anasema mimi nishulikie visa kuhusu travel ticket ni yeye ushauri please
Izzo njoo huku
Kila la kheri malkia wa Nguvu Mungu akufanyie wepesi hapo mwambie mama akutumie barua ya mwaliko uende nayo ubalozini utapata viza faster
 
Kila la kheri malkia wa Nguvu Mungu akufanyie wepesi hapo mwambie mama akutumie barua ya mwaliko uende nayo ubalozini utapata viza faster
Mkuu nimeongea nao inaonesha ni matapeli tuu
 
Ulisbaoata habar za Botswana Segitoo?
 

Kitu cha kujifunza tu, ni ngumu kwa mtu kupata kazi majuu ambayo sio ya kitaalamu kama haishi nchi hiyo husika. Kuna wageni wengi katika nchi hizo ambao hawana kazi na wana vibali tayari. Njia ya kutumia kupata kazi kama haupo majuu tayari ni mission impossible. Kuna kazi chache za msimu kama za kuchuma matunda majira ya joto amabazo unaweza kubahatisha kuzipata majuu huku ukiwa nchi ningine.

Angalau watu wa Asia hasa Wahindi wanaweza kupata kazi za kitaalamu majuu wakiwa India hasa za IT. Kwa Afrika labda uwe unafanya kazi na kampuni ya Wazungu Afrika upate transfer ya kwenda majuu. Nchi nyingi za majuu zinathamini elimu zao tu.

Njia za moja kwa moja kuja majuu ni masomo na ndoa.
 
Bora ufanye hivyo mkuu huu msala uepuke kihivyooo
 
Shukrani sana Mkuu Izzo. Najua ulimwenguni utapeli umejaa mno. Hivyo sio tatizo kabisa kukumbana nao na kuwaepuka. Asante kwa angalizo lako toka mwanzo. Tunasubiri zaidi toka Germany.
 
Kuwa na aman, hapa ndio kwaanza safari inaanza. Nia tunayo uwezo tunao tutafanikiwa tuu.
 
Nimeshawasiliana nae,kasema ana watoto wawili kwangu haina shida
So nimetuma scanned passport na CV yngu so nasubiri kuckia kutoka kwake
Thanks izzo maisha popote,Yes nina degree lakini ramani hazisomi ngoja nijitoe muhanga mimi.
Nilikuwa na mimi nimcheki ila kwasababu umeshalianzisha ebu endelea nalo tusije zibiana nafasi hizi maana chache... labda ukishindwa tuambie wengine tufungue mawasiliano nae pia... ila nakutakia kila la kheri katika kufanikisha hili mkuu...
 
Umesema kweli Mkuu Money9. Ila hupaswi wala hatupaswi kukata tamaa. Wajua matapeli, wapo kila kona. Kikubwa, tunapaswa kupashana habari kwa lolote linalotokea, ili kupata ushauri na uchunguzi zaidi. MATAPELI WAPO, ILA WASIKUKATISHE NA KUKUZUIA KUSONGA MBELE.
 
Nashindwa ku attach PM
Niliweke hapa namba zao na address zao?
 
Nina diploma ya biomedical engineering nchi gani naweza kupata kazi kiurahisi?
Moja ya kozi ambayo naikubali kwa sasa mkuu kama unataka utoboe fasta..nenda kapige degree pale MUK (Makerere university) au chuo chochote hapa africa ni miaka 3 tu then omba sponsership utokomea ughaibuni hasa Austaria,canada,US,Sweden,Dernmark na uhakika miaka miwili miwili tu utakuwa uko mbali sana kwanza ni moja ya faculty yenye salary ya maana sana kwa nchi nilizo kutajia.
Vinginevyo tafuta uwezekano wowote ilimradi ufike kwenye moja ya nchi hizo halafu ujiendeleze elimu yako ya BIO ukiwa kwenye nchi husika yani kosa tu upate ajira na ukawa uko vizuri practicaly yaani Uwe na uwezo wa kuisambalatisha MRI,X-ray machine,Utrasound machine,Pulseoxymeter n.k na mzungu akakwamini mkuu naimani utafurahia elimu yako.
Nakutakia kila lakheri mkuu kuna jamaa angu yupo RUSSIA anamalizia masomo mwaka huu hiyohiyo BIO ananiambia kama alichelewa vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…