Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Thanks mkuu.
 
Wazo zuri je na hao wanaotaka PM unatoa ushauri gani kwao? Rejea huu uzi toka awali, tulianza vizuri sana Izzo alitueleza mambo mengi sana, akatokea mtu na maneno ya kuudhi Izzo akajitoa ndo hapo wazo la whatsapp likaja.
 
Nafikir hapa ni pazuri zaidi kuliko huko kwenye magroup ya watsap...
Hofu inakujaje huko kwenye whatsapp hapa tulikuwa tunaenda vizuri sana mpaka tukapewa plan ya kuhost wageni kujiandikisha ilikuwa tuanze hii April na June waje je unajua kilichotokea?
 
Kikubwa kinachohofiwa ni kipi? Rejea huu uzi toka post no 1 jibu la kuanzisha group la whatsapp utapata. Kuhusu PM zilikatazwa lakini hamsemi kuhusu hilo.
 
Wakuu hivi nikipata host wa kumfamfanyia kazi ya kujitolea in USA akanipa mwaliko wa miezi mitatu, itakapoisha ana uwezo wa kuniongezea mda wa kuendelea kuishi kule au sheria ya kule hairuhusu ???
 
Hofu inakujaje huko kwenye whatsapp hapa tulikuwa tunaenda vizuri sana mpaka tukapewa plan ya kuhost wageni kujiandikisha ilikuwa tuanze hii April na June waje je unajua kilichotokea?
Mkuu sijajua faida za watsap, utazoenda kupata mbali na utakazo pata hapa..., ? Ila syo mbaya nendeni ila I hope hapa ni mahari sahihi...kwa maoni yangu...
 
Mkuu sijajua faida za watsap, utazoenda kupata mbali na utakazo pata hapa..., ? Ila syo mbaya nendeni ila I hope hapa ni mahari sahihi...kwa maoni yangu...
Mkuu kilichopelekea kuanza kwa whatsapp ni kejeli, dharau na kuita waleta mada matapeli toka kwa baadhi ya wachangiaji, Nina imani yeyote anaejiamini kwa kauli na matendo yake mema Hana haja ya kujificha atakuja tu huko.
 
Mkuu sijajua faida za watsap, utazoenda kupata mbali na utakazo pata hapa..., ? Ila syo mbaya nendeni ila I hope hapa ni mahari sahihi...kwa maoni yangu...
Anza mwanzo kabisa utajua nini kilisababisha watu wafikirie kuanzisha grup la Whatssap. kwani kuna watu humu hawakuwa nania njema kwenye huu uzi. So watu wakaona kwakuwa si wote wenye nia njema humu bora kuepukana nao kwa njia hiyo na njia pekee ni kuunda grup la..........
 
Wakuu hivi nikipata host wa kumfamfanyia kazi ya kujitolea in USA akanipa mwaliko wa miezi mitatu, itakapoisha ana uwezo wa kuniongezea mda wa kuendelea kuishi kule au sheria ya kule hairuhusu ???
tourist visa ya US hata ukiomba week2 utapewa ya mwaka mzima, ipo hivyo. sema ukisema utakaa week2 then ukakaa miezi 12 na ukarudi bongo siku ukienda omba tena unaweza usipewe....ongea na host wako atakupa info zaidi....
 
Poa mkuu, japo nilikuwepo tangu mwanzo..., niliamin ni changamoto tuu..., ila syo mbaya...
 
Mkuu kilichopelekea kuanza kwa whatsapp ni kejeli, dharau na kuita waleta mada matapeli toka kwa baadhi ya wachangiaji, Nina imani yeyote anaejiamini kwa kauli na matendo yake mema Hana haja ya kujificha atakuja tu huko.

Mkuu Zogoo da khama umenena vyema.
Sijui wengi Au wachache ambao hatupendi kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp.
Ukiangalia ktk hili jukwaa mpaka Sasa hatuwaoni wale wenye dharau na kejeli.Wengi wamechangia kutoka Japan Na sehemu tofauti.
Vilevile kaka Izzo ametoa Maelezo Kwa mmoja wetu ambaye anakwenda Japan.Sisi wote tumejifunza mambo manne kuhusu Watu wa nchi za Asia.Kama wote tungekuwa kwenye group wangapi wangeyajua hayo.
Muhimu katika huu uzi unachunguza CV za Watu ambao wana nia ya kutoka au la.
Ni rahisi kuwasaidia wenye nia ya kweli.
 
Saf
tourist visa ya US hata ukiomba week2 utapewa ya mwaka mzima, ipo hivyo. sema ukisema utakaa week2 then ukakaa miezi 12 na ukarudi bongo siku ukienda omba tena unaweza usipewe....ongea na host wako atakupa info zaidi....
Asante mkuu nimeelewa sasa baada ya miezi 12 kuisha anaweza kuniombea tena mingine 12 au zaidi???? Pia mda huo wa miezi 12 naweza kupiga kazi hela ???? au sheria hairuhusu ???
 
Saf

Asante mkuu nimeelewa sasa baada ya miezi 12 kuisha anaweza kuniombea tena mingine 12 au zaidi???? Pia mda huo wa miezi 12 naweza kupiga kazi hela ???? au sheria hairuhusu ???
sheria zao haziruhusu tourists kufanya kazi, kama wenyeji wako ni wajanja waweza faaanya kazi kwa watu wanaowaamini, maana kuna hofu ya kudhurumiwa ukakosa pa kuripoti maana hukutakiwa fanya hizo kazi.
 
Issue ya what's app group iliibuka baada ya jamaa mmoja (though iligundulika ni tapeli) kujaribu kupoteza lengo la thread hii, so ili tuweze kutambuana (maana humu tunatumia fake ID's) na kuepusha udanganyifu ikaonekana its better kukutana pia huko kwa what's app group.
 
Mkuu Saplaiz
Toka uzi ulivyo anzishwa Na Mkuu Lusungo sijaondoka Ktk hili jukwaa.Hata wafitini walivyo chafua hali ya hewa Na Mkuu Izzo akasita kuendelea Na programs hivyo vyote nimevisoma.Kwa bahati nzuri tu wafitini wameweza kutusaidia kuwaona WaTanzania wengi NI wakarimu,wazalendo Na hawana roho za Kwa nini.Kwa wanao taka kuwa kwenye magroup ni sawa tu:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…