Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Huyu jamaa apewe nishani...Dar -Nairobi -Kampala -Juba-Khatourm-Port Al saed -Syria -Turkey hadi Denmark si mchezo.
Hiyo inawezekana hasa kwa wasio na Elimu ila kwa sisi tuliosoma ni waoga mnoo wakuthubutu na kuwaza risk kibao.......pia tunapenda sana kupita legal ways ambazo kikawaida ndizo huchelewesha safari
Niwape moyo wapambanaji wote wenye lengo la kutoka nje wasisite waendelee!!
 
Mimi nipo Tanzania,sema nilishawahi kuishi nje kidogo,niliona wanavyohangaika wageni ila ukipata makaratasi mambo yanakuwa mazuri.
Kama uko tz na ulikuwa nje na ukashindwa maisha ni wewe. Kila mmoja ameandikiwa njia yake na sehemu yakubarikiwa na kufanikiwa. Kukata tamaa hakutakiwi.
 
Kama uko tz na ulikuwa nje na ukashindwa maisha ni wewe. Kila mmoja ameandikiwa njia yake na sehemu yakubarikiwa na kufanikiwa. Kukata tamaa hakutakiwi.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 
Japan zipo za PhD South korea mpaka nicheki na wadau

Scandnavia Zipo za Denmark
Norway
Sweden

America zipo za Canada na US

Kiwango cha elimu kusomea ni Masters na PhD

Sharti ufanye mtihani wa kingereza score ni kuanzia 70%

Ni full Scholarship kuanzia nauli ya kwenda na kurudi kwenu kwa mwaka mara mbili maradhi na pocket money kila mwezi
Mkuu Izzo nahitaji scholarship za Masters, Paper ya kiingereza sio issue sana ntakomaa nacho
 
f3d3f1c69fe837f26fcfa18a214662ef.jpg

Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Mnatukumbusha kauli za Kamuzu Banda na Mabutu Seseseko, leo hii Malawi ndio imetoa wafanyakazi wa nyumbani wa kiume (foreign male domestic workers) kuliko nchi nyingine Afrika.
DRC ni katika nchi tajiri Afrika hii lakini waangalie Wakongo wengi walipo, zaidi ya wanaume kukata viuno jukwaani, kuimba na kujichubua. Leo Wakongo sio watu wakula mbwa na nyani.

Hii Tanzania yetu, unaweza kutimiza ndoto yako, hata kuanzia mchimba mkaa mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa. Why not? Right here in Tanzania

Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulaya wakati ardhi zetu zina rutuba ya kukutosha na tunaweza kuishi na kuendesha maisha yetu kupitia kilimo?

Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muhanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya Wakoloni.

Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.
Mkuu kama huna mpango wa kusepa TZ nenda MMU tuachie uzi watu.
 
Eti mtu anasema haondoki africa anahisi akijifungia africa ndio atapata maendeleo. Haya muulize tangu huo uhuru wa bendera wa africa kuna kiwanda cha smartphone? Anavaa majani ya mpapai au jeans from usa? Anakula kwa vijiko vya china au anatumia visu vya tameco?

Anaendesha gari ya nyumbu au toyota ya mjapan? Anapanda bajaji za muhindi au baiskeli za miti za wasukuma? Hata pedi tunaagiza kutoka nje utasema kwenda alaya ni ukoloni si yaleyale tu
Mwache aendelea kukaa bongo wakati watoto wa viongozi wanaishi London. Watuache tukale bata Copenhagen
 
Japan zipo za PhD South korea mpaka nicheki na wadau

Scandnavia Zipo za Denmark
Norway
Sweden

America zipo za Canada na US

Kiwango cha elimu kusomea ni Masters na PhD

Sharti ufanye mtihani wa kingereza score ni kuanzia 70%

Ni full Scholarship kuanzia nauli ya kwenda na kurudi kwenu kwa mwaka mara mbili maradhi na pocket money kila mwezi
Vipi kuhusu za postgraduate mkuu
 
f3d3f1c69fe837f26fcfa18a214662ef.jpg

Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Mnatukumbusha kauli za Kamuzu Banda na Mabutu Seseseko, leo hii Malawi ndio imetoa wafanyakazi wa nyumbani wa kiume (foreign male domestic workers) kuliko nchi nyingine Afrika.
DRC ni katika nchi tajiri Afrika hii lakini waangalie Wakongo wengi walipo, zaidi ya wanaume kukata viuno jukwaani, kuimba na kujichubua. Leo Wakongo sio watu wakula mbwa na nyani.

Hii Tanzania yetu, unaweza kutimiza ndoto yako, hata kuanzia mchimba mkaa mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa. Why not? Right here in Tanzania

Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulaya wakati ardhi zetu zina rutuba ya kukutosha na tunaweza kuishi na kuendesha maisha yetu kupitia kilimo?

Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muhanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya Wakoloni.

Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.
Wewe ni zaidi ya mpumbavuu.
 
Among other factors, nadhani baadhi ni:

- Uoga wa maisha. We are extremely fearful of life. We can't take risk ktk utafutaji, tunasahau kwamba there's nothing risk-free in life struggle.

-Lack of international exposure kwa wazazi wetu. Most of us tumezaliwa na kukulia kwenye families ambazo hazikuwa 'global goers'. As such, na sisi tunaishia in the same circle... mtu anapanda Ngorika all the way from sitimbi to Darisalamu, then hiyo ndo maximum exposure ya ndoto zake... kutia maguu Daresalamu.

-language barrier. Hili liko wazi. Wabongo wengi 'kutema yai' ni shuhuli nzito. English is amongst of international languages that highly connect the world. Sisi tumekomaa na kiswahili, lugha ambayo bado haijatoboa kimataifa even at regional level. So ni ngumu sana kujichanganya kwenye international avenues za kutafuta maisha. Mfano tu, jaribu kupitia international forums kwenye social media, wabongo hawasogezi pua huko, utawakuta wachache sana.

Mfano mwingine, mtu ni Masters holder lakini spoken English ni zero! Hawezi kutema 'yai'. Mtu huyu anaogopa na hawezi kuapply kazi at International entities like NGOs, UN Agencies, etc. Human personnel from East africa to UN Agencies... Kenya na Uganda make the majority. Intl languages competence bado ni shida kubwa kwa watanzania.

-Poor education. Wabongo wengi tunaenda class kukaririshwa vitu, na sio kueleweshwa materials. Hivyo inakuwa ngumu sana kupenya abroad under 'professional job' umbrella.

Kuna mtu namfahamu kabisa personally ... kahitimu Bachelor Degree mwaka jana. Cha kushangaza sasa... hajuwi jinsi ya kufungua/kuandika email na kuweka attachment. Hawezi kabisa! So mtanzania kama huyu, anaweza ku-compete kwenye international professional jobs/opportunities?

Nadhani hizo ni miongoni mwa factors zinazosababisha wabongo tusiwe courageous wala aggressive kufukuzia international money.

Wacha tuendelee kulima mchicha ili kupata hela ya dona na rent ya chumba uswazini. Ila ukipata viza, then pasua anga. Bongo hakuna mwanga. Waya mkali mbuzi analamba reli.

Baby don't cry, keep ya head up until the end of time. Life goz'on.

-Kaveli-

Mkuu Kaveli nakusalimu popote pale ulipo.

Bruh don't cry you gotta keep yo head...

afe9e745a0adcb1f055d364edb76f23e.jpg
 
Jamani Ndg Watanzania Japan imetoa schoralship kwa Watanzania nafasi 5 kusoma vyuo huko
Kwa watakaosoma degree Ya kwanza wawe wamezaliwa mwaka 1996 hadi 2001 mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 26/05/2017
Ni kwa ajili Ya muhula WA masomo 2018/2019
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti Ya ubalozi wa japani
Ukipata Habari hii Mwambie hata jirani yako amuombee mwanaye hata Kama wewe umri umekutupa Mkono toa usiwe na roho Ya nongwa..
Asante..!!
 
Jamani Ndg Watanzania Japan imetoa schoralship kwa Watanzania nafasi 5 kusoma vyuo huko
Kwa watakaosoma degree Ya kwanza wawe wamezaliwa mwaka 1996 hadi 2001 mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 26/05/2017
Ni kwa ajili Ya muhula WA masomo 2018/2019
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti Ya ubalozi wa japani
Ukipata Habari hii hata jirani yako amuombee mwanaye hata Kama wewe umri umekutupa Mkono toa usiwe na roho Ya nongwa..
Asante..!!
Asante kwa taarifa mkuu...
Ngoja tukachungulie..!
 
mdau kwenye kupata schengen visa ni lazima kulipia ile travel insurance policy (wanasema minimum ni Euro 30000). hicho kigezo si ni kikwazo kikubwa au namna? ushauri tafadhali.
 
jamani watanzania shambulieni nafasi za masomo nchi ya Mauritius kila mwaka huwa wanatoa kwa nchi zote za Afrika, hii haina masharti mengi siyo lazima uwe umefuzu mtihani wa lugha, ni uhakika hii kupata
unachotakiwa kufanya nikuomba nafasi katika chuo chochote cha serikali cha nchi hiyo ya Mauritius, ukipata acknolgment letter kutoka chuo husika kuna fomu utaipeleka wizara ya mambo ya nje utaonana na mkurugunzi msaidizi wa mambo ya nje anaitwa Ms Mwakiwago anakusainia na kukupitisha hapo then yeye atatuma huko kwenye nchi husika haina complicated inshi nyingi sana.
Mwisho wa maombi ni tarehe 31 mwezi huu
mara nyingi hizi nafasi kwa Tanzania huwa zinarudi bila watu kuomba tafafadhali changamkia hii nafasi
Mshirikishe hata jirani yako aombe iyo lazima uwe wewe, nimesikia malalamiko eti humu kuna roho za korosho
http://ministry-education.govmu.org...Documents/tertiary/2017/Application Form .pdf
google Mauritius scholarship 2017 utaziona na vyuo vya serikali vipo ni vinne tu
Utakuwa unalipiwa garama za chuo ambzo ni takiribani sh MUR 100,000 ambazo ni sawasawa na Tzs milioni sita na nusu na ushee,
na pesa ya matumizi kila mwezi MUR 8,300 sawasawa na LAki 5 na ushee
ni kiinchi kidogo lakini uchumi wake ni mkubwa sana kipo kisiwani

Nauli utajilipia ya kwenda daraja la Economy ukifika huko utaonyesha ticketi yako na kurudishiwa pesa yote uliyotumia kwa nauli

PM HAZIRUHUSIWI
 
Back
Top Bottom