Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Huyu jamaa apewe nishani...Dar -Nairobi -Kampala -Juba-Khatourm-Port Al saed -Syria -Turkey hadi Denmark si mchezo.
Hiyo inawezekana hasa kwa wasio na Elimu ila kwa sisi tuliosoma ni waoga mnoo wakuthubutu na kuwaza risk kibao.......pia tunapenda sana kupita legal ways ambazo kikawaida ndizo huchelewesha safari
Niwape moyo wapambanaji wote wenye lengo la kutoka nje wasisite waendelee!!
 
Mimi nipo Tanzania,sema nilishawahi kuishi nje kidogo,niliona wanavyohangaika wageni ila ukipata makaratasi mambo yanakuwa mazuri.
Kama uko tz na ulikuwa nje na ukashindwa maisha ni wewe. Kila mmoja ameandikiwa njia yake na sehemu yakubarikiwa na kufanikiwa. Kukata tamaa hakutakiwi.
 
Kama uko tz na ulikuwa nje na ukashindwa maisha ni wewe. Kila mmoja ameandikiwa njia yake na sehemu yakubarikiwa na kufanikiwa. Kukata tamaa hakutakiwi.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 
Mkuu Izzo nahitaji scholarship za Masters, Paper ya kiingereza sio issue sana ntakomaa nacho
 
Mkuu kama huna mpango wa kusepa TZ nenda MMU tuachie uzi watu.
 
Mwache aendelea kukaa bongo wakati watoto wa viongozi wanaishi London. Watuache tukale bata Copenhagen
 
Vipi kuhusu za postgraduate mkuu
 
Wewe ni zaidi ya mpumbavuu.
 

Mkuu Kaveli nakusalimu popote pale ulipo.

Bruh don't cry you gotta keep yo head...

 
Jamani Ndg Watanzania Japan imetoa schoralship kwa Watanzania nafasi 5 kusoma vyuo huko
Kwa watakaosoma degree Ya kwanza wawe wamezaliwa mwaka 1996 hadi 2001 mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 26/05/2017
Ni kwa ajili Ya muhula WA masomo 2018/2019
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti Ya ubalozi wa japani
Ukipata Habari hii Mwambie hata jirani yako amuombee mwanaye hata Kama wewe umri umekutupa Mkono toa usiwe na roho Ya nongwa..
Asante..!!
 
Asante kwa taarifa mkuu...
Ngoja tukachungulie..!
 
mdau kwenye kupata schengen visa ni lazima kulipia ile travel insurance policy (wanasema minimum ni Euro 30000). hicho kigezo si ni kikwazo kikubwa au namna? ushauri tafadhali.
 
jamani watanzania shambulieni nafasi za masomo nchi ya Mauritius kila mwaka huwa wanatoa kwa nchi zote za Afrika, hii haina masharti mengi siyo lazima uwe umefuzu mtihani wa lugha, ni uhakika hii kupata
unachotakiwa kufanya nikuomba nafasi katika chuo chochote cha serikali cha nchi hiyo ya Mauritius, ukipata acknolgment letter kutoka chuo husika kuna fomu utaipeleka wizara ya mambo ya nje utaonana na mkurugunzi msaidizi wa mambo ya nje anaitwa Ms Mwakiwago anakusainia na kukupitisha hapo then yeye atatuma huko kwenye nchi husika haina complicated inshi nyingi sana.
Mwisho wa maombi ni tarehe 31 mwezi huu
mara nyingi hizi nafasi kwa Tanzania huwa zinarudi bila watu kuomba tafafadhali changamkia hii nafasi
Mshirikishe hata jirani yako aombe iyo lazima uwe wewe, nimesikia malalamiko eti humu kuna roho za korosho
http://ministry-education.govmu.org...Documents/tertiary/2017/Application Form .pdf
google Mauritius scholarship 2017 utaziona na vyuo vya serikali vipo ni vinne tu
Utakuwa unalipiwa garama za chuo ambzo ni takiribani sh MUR 100,000 ambazo ni sawasawa na Tzs milioni sita na nusu na ushee,
na pesa ya matumizi kila mwezi MUR 8,300 sawasawa na LAki 5 na ushee
ni kiinchi kidogo lakini uchumi wake ni mkubwa sana kipo kisiwani

Nauli utajilipia ya kwenda daraja la Economy ukifika huko utaonyesha ticketi yako na kurudishiwa pesa yote uliyotumia kwa nauli

PM HAZIRUHUSIWI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…