Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

jaaaamani wakuuu na wataalamu naomba hints za kuingia switzerland please ninaomba nimepitia uzi sijaona kuhusu switzerland
 
mjingamimi, Sky Eclat, lusungo, Dr.adams faida, bigmind, Daby, Rich Ze Best, Lizarazu, DUBE, nchemime, Shyshii, Prishaz, cognition ,impelle, Dumelang, Ng'wanapagi, wamba, Tantaw, Wonderful, bily, Richard, Remote, Prof, chindo, PATO8221, Jambazi, dolevaby danya, Chillah, SDG, ganja gal, meney9 , the ox , farharu, dangadunguri, KIKAZI, STUNTER, wiseboy, Mrike , Cole Williams, mgaka12 , kirikou1 , KikulachoChako , kilam , Se-ronga , kiumbe kipya , xav bero, Prishaz

Salaamu wakuu, natumaini mu wazima wa afya. Mimi pia sijambo wa afya, Mungu ni mwema.

Awali ya yote, napenda kutoa shukrani za dhati kabisa to all folks ambao mmekuwa mkiniPM (from time to time) kuulizia progress ya suala langu with mkuu izzo. Ahsanteni sana kwa kuguswa na kujali. Niliwaahidi kutoa full update Tarehe 1 August 2017, na LEO hii ndiyo siku yenyewe.

Nitaanza na Background kidogo ili kukumbushana tu mchakato ulianzia wapi, uliendeleaje, na hatimaye picha limeishaje. Nitaweka maelezo kwa mtiririko wa numbering paragraph, just for the purpose of easy reference kwa wachangiaji.

1. Communication yetu (mimi na mkuu Izzo) ilianzia kwenye post yangu [HASHTAG]#1493[/HASHTAG] kwenye uzi huu. Kwenye post hii nili-share, among other things, PLAN yangu ku-secure scholarship to study in home country for Undergraduate Level (bachelor degree). Ndugu Izzo aliguswa na post yangu hiyo, akaahidi kunisaidia ila kwa kamtihani kidogo... akaniuliza if I can compose a write-up (an essay) of 400 words kuelezea NITAFANYA NINI KAMA NIKIPEWA US DOLLAR 100? Nikamjibu kuwa naweza vizuri tu kuandika hiyo essay.



2. Ilikuwa ni kama 'zali' kwangu, coz kwa mujibu wa Izzo, ni nafasi MOJA tu (kati ya nafasi TANO) ndiyo ilikuwa imebakia for such scholarship opportunity within Izzo's linkage, na nafasi hiyo ikawa offered kwangu. Nikasema YES... let me struggle for this lucky chance:



3. Niliandika hiyo essay fupi ya 400 words na kumaliza. Nikasubiri maelezo zaidi from Izzo juu ya nini cha kufanya. Kisha hapa hapa jukwaani akanipa email ya mtu niitume ile essay. Nikapata hofu email ya huyo mdau (connector/insider) kuwekwa hapa publicly, kwamba je na wengine wakimtumia essays itakuwaje?!! nilitarajia iyo email address ningeipata kwa PM. Ofkoz nilimuuliza mkuu Izzo WHY amefanya hivyo? akanijibu kuwa ataniPM kunipa 'CODE NUMBER' ya kumtumia huyo insider kama utambulisho ili ajue kuwa ni mimi.



4. I sent the essay to such email address. Mtu huyo aka-respond by asking ''name, rank en ur Serial number ?''



Nikacheck with Izzo kuhusu rank & serial number... akaniambia cha kujibu, kwenye name ni majina yangu kamili. Nikareply hiyo email accordingly. Kisha email id hiyo ikanitumia link ya sponsor mwenyewe sasa. Nilipoclick hiyo link, nikaona ni website ambayo naifahamu vizuri tu. Ni sponsor ninayemfahamu, namfahamu kwa maana ya kwamba tayari nilishawahi kufanya application the previous year. Ila nikajisemea moyoni kuwa wacha niaapply tena kwa vile kuna back-up & connection by an insider from Izzo.

5. Izzo akaniPM na kunizuia nisithubutu kuigawa hiyo link. Thus, I should NOT share the link to anyone else. Akasema nikithubutu kui-share hiyo link atajua tu. Mimi nikamjibu kama ifuatavyo... najinukuu:

'' Mkuu, hiyo link ni www.wellsmountainfoundation.org. Wells Mountain Foundation ni taasisi inayotoa support to communities (worldwide) with main focus, among other things, on LITERACY and EDUCATION. Nawajua hawa, na nilishawahi kujaribu kuwaomba scholarship mwaka jana, SIKUPATA!

Hii hapa chini ni email waliyonitumia 1 APRIL 2016 to acknowledge receipt of my completed Application



Application Form yao entails a lot of blanks for plenty write ups, na nilijikunja hasa kuandika, but sikubahatika! To be honest miye sikuwa na mpango wa kuaapply tena, coz it seems being a very competitive scholarship opportunity. Lakini kwa vile umenihakikishia 'connection' kwenye hilo, ndo ninaapply tena kwa mara nyingine.

How did I come to know them? It is just through internet searches. Tangu mwaka juzi nilikuwa nagoogle sana scholarships opportunities, ndipo siku moja nikawaona hao wamarekani Wells Mountain Foundation, na nikaapply accordingly but hollaaaa!

Kikubwa kinachoniuma kwenye hiyo programme, watanzania hawaipati kabisa. Wakati naaply mwaka jana, nilicheki the previous scholars waliopata (2015 scholars)... yani hapakuwepo na mtanzania yeyote hata mmoja!

Na scholars waliopata mwaka jana (2016 scholars) ambapo miye sikupata, pia hakuwepo hata mtanzania mmoja, scholars 41 from 20 developing nations, no any Tanzanian!!! Kwa east africa, ni wakenya na wanganda tu ndo wanaipata sana hiyo fursa.

It hurts kwakweli. It is either Tanzanians are NOT aware of such opportunity or hawaapply. So, sielewi WHY hutaki nishee hiyo website ya Wells Foundation with other Tanzanians ili nao wajaribu bahati yao, yaani wajaribu tu kuapply wao wenyewe solely bila 'connection' yako kuhusika. WHY?

By the way, that is a website, so nadhani itakuwa tu inafahamika kwa watu. YOU and/or I can't hide it from being visited by other people. '' mwisho wa nukuu.

6. Then mkuu Izzo akajibu kuwa kama nilishawahi kufanya application mwaka jana, basi nisiandike application upya. Bali nimtaarifu tu yule insider kuhusu hilo na nimforwadie hiyo Confirmation Email niliyopokea mwaka jana from the Organisation (WMF). Nikafanya hivyo, ila zikapita siku kadhaa insider akiwa kimya. Pia nikamtaarifu Izzo kuhusu ukimya wa insider wetu.

7. Tarehe 25 March 2017, nikapata PM from Izzo... namnukuu: '' Mcheki whats app kama amezifanyia kazi mm sasa hv nimesha withdraw kwenye project yeyote ya hapo jukwaani namba yake hyo +1 (845)... .... ". Sikumcheki huyo mtu by whatsapp.

8. Tarehe 4 April 2017, nikapata another last PM from Izzo... namnukuu: '' Nimewasiliana na Sammy kaniambia amepata email yako na anaifanyia kazi so relaxing mkaka ''

9. Tarehe 30 March 2017, nikapata last email from the insider wetu... namnukuu: ''Your E-mail address has been confirmed''.

10. LEO tarehe 1 August 2017, the Wells Mountain Foundation has released the list of 75 students from 17 developing nations as 2017 WMF Scholars supported through the Empowerment Through Education program. HAKUNA mtanzania hata mmoja! YES, there is NO ANY granted applicant from Tanzania.

Scholars wa 2015 hapakuwa na any mtanzania. Scholars wa 2016 hapakuwa na any mtanzania. Scholars wa 2017 pia hakuna mtanzania. Hata ukicheki miaka ya nyuma hakuna watanzania, ni 2014 tu ndiyo niliona mtanzania mmoja alipata. Kwa scholars from East Africa, kenyans make the majority!! na Ugandans na Rwandeese.

WMF ni NGO iliyopo Marekani. Wana-empower communities in developing countries worldwide. Among other supports, wana-offer scholarship to study in home country for undergraduate studies, under their programme called 'Empowerment Through Education'. Package ya scholarship ni maximum US Dollar 3,000 per academic year.

List ya 2017 Scholars hii hapa: Our Scholars | Wells Mountain Foundation

My kind Appeal: Watanzania wenzagu, jaribuni kutumia hii fursa kwa wahitaji. Visit the site for further info. Wakenya wanalamba sana hii fursa kila mwaka.

Thanks mkuu izzo for the efforts you did put in. Though the thing haijazaa matunda.

-Kaveli-
 
Duh brother Kaveli Ubarikiwe sanaaaaa tu Kwa ujasiri wako.
Kwa kweli mrejesho wako umeniingia Kwa uchungu Na furaha.Uchungu umeikosa nafasi Na furaha umejaribu.


Kaka mgogoone, shukrani pia ndugu kwa michango yenu mizuri kwenye uzi huu. Naamini kwa vyote vyote vile, kuna watu wamenufaika na uzi huu kimaarifa n.k

-Kaveli-
 
Kaka mgogoone, shukrani pia ndugu kwa michango yenu mizuri kwenye uzi huu. Naamini kwa vyote vyote vile, kuna watu wamenufaika na uzi huu kimaarifa n.k

-Kaveli-

Ukifungwa mlango mmoja ujue kuna mingine inafunguliwa.....silaha yako kubwa ya ushindi ni kutokana tamaa....endeleza mapambano mpaka pumzi yako ya mwisho......

Nimesoma mtiririko wa habari yako kwa makini...lakini nilichogundua nje ya andiko ni kuwa una ujasiri wa kipekee ambao sijawahi kuuona kutoka kwa kijana yeyote yule.....una uthubutu wa hali ya juu sana.....

Kwa kifupi nimegundua una kila sababu ya wewe kufanikiwa kwa kuwa kitu kilichomo ndani ni si cha kawaida......

Mungu akujaalie afya njema ili ufanikishe hitaji la moyo wako......
 
Kaveli ilikuwa ina wezekana kuomba ufadhili bila kuwa umeomba chuo au? sijaelewa mkuu... na coz za kuomba kama nyingi ni za kusaidia jamii zaidi ukiangalia kwa wale walio omba kutoka africa...

vipi wewe uliomba kusoma coz gani na ni chuo gani ulitegemea kuomba...
 
Kaveli ilikuwa ina wezekana kuomba ufadhili bila kuwa umeomba chuo au? sijaelewa mkuu... na coz za kuomba kama nyingi ni za kusaidia jamii zaidi ukiangalia kwa wale walio omba kutoka africa...

vipi wewe uliomba kusoma coz gani na ni chuo gani ulitegemea kuomba...
 


Mkuu KikulachoChako, siku zote humu hekima na busara zako huwa zinanigusa sana. Mara zote huwa ni msema kweli... ni kitu kilichopo ndani yako.
Ahsante ndugu yangu kwa dua zako njema. Mungu akujaalie na kukuzidishia hekima.
Mapambano on progress until we kiss the dust.
Zetu dua.

-Kaveli-
 


Yes mkuu, wanaruhusu uombe scholarship hata kama bado hujapata Admission ya Chuo. Hili wamelisema openly kabisa. Kwa wale applicants wasio na admission yet, cha muhimu ni uoneshe ni Chuo gani umeomba admission, na course gani.
Ila nadhani kwa applicants wanaokuwa na admission tayari, wanakuwa kwenye better position.
So kwa mujibu wa WMF, hata kama bado unasubiria admission, ruksa kuapply scholarship from WMF.
Kuhusu mimi, mwaka jana 2016 niliapply scholarship yao kabla sijapata Admission. Then sikubahatika kupata hiyo scholarship. Ila Admission Offer nilipata, nikaipotezea coz sikuwa na namna.
WMF wanasponsor course yoyote undergraduate level. Kuna essays nyingi za kuandika, pia uelezee in details ni jinsi gani hiyo course yako itanufaisha jamii yako. Pia je una background history ya kushiriki kwenye volunteer activities za community? Etc etc. Criteria zao zipo kadhaa wa kadhaa.
Application Deadline ni 1 April kila mwaka. Successful applicants release ni 1 August.

-Kaveli-
 
Naomba ufafanue hizo number na rank! Ulivyowafuatilia, hukupata clue kama hao jamaa siyo tawi la secret society?
 
Tumeomba lakini tumekosa ndugu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…