Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Aki watanzania, tuko nyuma bado tukomae kujenga nchi yetu.

Maana maendeleo yanahitaji mikiki mikiki.
Sio kulala lala.
 
Huoni mtoa mada kasema wazi, nchi yetu maskini, fursa hakuna.
Elimu tumo nyuma
Watu hatuna ushirikiano.
Fursa zipo lakini hatuzioni na kuzitumia
Ndio maana wazungu wanapigania kuja kwetu na sisi tunapambana kwenda kwao kwa sababu kila mmoja anaziona fursa za mwenzake.
 
Ukweli fursa zipo, hadi uwe na mtaji wa kutosha ndio utapiga hela kwa haraka.

But kama huna mtaji, utabeba mizigo hadi uchoke.
Fursa zipo lakini hatuzioni na kuzitumia
Ndio maana wazungu wanapigania kuja kwetu na sisi tunapambana kwenda kwao kwa sababu kila mmoja anaziona fursa za mwenzake.
 
Mkuu msaada hapo natak kuzamia hiyo nchi ya Malta. Nifanyeje please
 
Wakuu, mie nashukuru nimepata Scholarship Sweden. Nitakuwa Umea University kuanzia sept mwaka huu, naomba mwenye connections na kazi za vibarua ( Non Skilled jobs) ili nikiwa free haswa masomo yanapokuwa hayajachanganya niwe na-make at least SEK 5,000-10,000 kwa mwezi.

Nipo tayari kufanya kazi yoyote halali ikiwamo kulimia bustani, kuvuna mazao, kuosha magari, kufanya usafi, kubeba box n. k. Kiufupi wakuu sitochagua kazi. Elimu yangu nitaweka pembeni na kupambana kusaka krones tu. Umaskini si kitu kizuri wakuu. Nitapambana kwa kila njia halali kuutokomeza umaskini maishani mwangu. Ee Mungu nisaidie.!!

Nimedharirika sana hapa bongo kutokana na ufukara, sasa kwa hii fursa ninaamini japo ni kwa ajili ya kimasomo ila nitapambana hadi tone la mwisho kuhakikisha natusua. Mie naamini majuu ni majuu tu. Hata kama ni kwenda kimasomo, hata kama kamji nakoenda nikadogo ukilinganisha na Stockholm ila nitapambana tu.
 
Hongera sana mkuu, karibu skandinavia
 
Wakuu mimi namaliza degree mwaka huu nimepanga kuzamia Canada. Nipeni mambinu namna gani nitafika uko..

lusungo bro nakutegemea..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…