Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Uzi huu ulinipa chachu ya kuja europe.... Mwaka jana mwez wa tisa niliingia rasmi europe... Nmeshatimiza mwaka na ushee sasa...

Nimekuja kwa njia ya masomo na sina mpango wa kurud bongo kiukwel.
Bongo nilikua na ajira ndio ila sikuona future yoyote . Biashara zangu ilifika hatua serikal ilibadili gafla gia angan ikasababisha biashara zangu zote kuingia doa.. sikuona mwanga.. ila pia nilikua mdau wa uzi huu kitambo sana. So nikaamua niufanyie kaz..

Hii ni ID yangu nyingne mpya ofcourse.. ya zaman naona imepigwa ban ya maisha..
Ila fresh tu.

Cha msing nachoweza sema... Njia ya shule kama una documents zoote muhimu .. bas ni njia nzur sana maana visa unapewa fasta sana.. na msing ni kwamba documents zako ziendane tu... Kwa ulaya haina shida unapewa fasta .. kwa US na canada na Australia inabid uwa convince vzur ili wasione kama utaenda zamia.. ila kwa ulaya.. wala hawaangalii sana. Tena kama unajilipia ada ndo kabisaa...
Hakikisha proof yako ya fanancial ipo vzur.. kama una ndugu wa kukusaidia onyesha bank statements bas fanya hvyo etc... Maana hii ndo kigezo namba 1 cha kupewa au kunyimwa visa. Kama utaona ni nchecheme nchecheme ... Kwamba usije ukaenda ukawa omba omba bure mitaan.

All in all.. lifw huku ni zuri mnoo.. hakuna uonevu wa kijinga. Ubabaishaj na maudh.. husikii watu wameiba mapesaa serikalin wala husikii kelele za ki chawa...

Huku kila kitu utashangaa siku za kwanza.. ni kuzur mnooo..
Nmezaliwa dar nmekulia dar.. naweza sema tandale ya huku kwa huko hata masak haion ndan *****... Ni kuzur kwel..

Mim nasoma.. napiga kaz za kunipa kahela pia ni artist so naingiza pesa kupitia njia hiz.. maana watu wa huku wanathamin sana art...

Uzi tayar.
 
Mkuu ulibahatika kwenda nchi gani?
 
Tupe hatua ulivyo omba chuo mpaka ukapata huko kaka.
 
😂😂😂😂😂😂Aseee nimecheka sana ndugu yangu. Yaani daah ila kwa upande mwingine ukiangalia kweli mara utaambiwa mto ruvu ng'ombe wanakunywa lita nyingi maji yanapungua ndo mana hakuna umeme, mara mvua zikinyesha Daaah 😂😂😂😂😂 huwa naishia kucheka mwenyewe tu. Ila umeongea ukweli bora kwa farao ufie
 
Mkuu uko nchi ipi
 
Ukitaka kujichekecha lazima ujue unaenda wapi?
Unaenda kufanya nini?
Na unaenda kuhamia mazima au kuchuma na kuwekeza ulipotoka.
 
Ukitaka kujichekecha lazima ujue unaenda wapi?
Unaenda kufanya nini?
Na unaenda kuhamia mazima au kuchuma na kuwekeza ulipotoka.
Inategemea na mahali ulipo nchi kama tz tunaishi kwa kudra tu.
 
Hujaweka kwenda kama mtalii, ongezea hapo
 
Habari ndugu zangu, matokeo ya green card yametoka namshukulu mungu nimefanikiwa kupata first notification ya Dv lottery kwamba nimeshinda hatua ya awali ya green card, naomba msaada Kwa yeyote anaefaham jinsi inavyojazwa fom ya Ds 260, pia naomba msaada jinsi ya kupata host U.s.
 
Mcheki EBM,,both instagram and Youtube mkuu.Hongera sana
 
hongera sana. binafsi sifahamuj insi inavyojazwa fom ya Ds 260.
 
Hongera saana ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…