Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Haya nipe Information nitaipata vipi hiyo Barua ya mwaliko?
Akuuu!!mi thijui chochote ila nataka mpeane hapa hapa baba kwa faida ya wote.dhumun la uzi huu ni kwa ajil ya umma.pm wengine tutakosa
 
Hahahaha, jiongeze kamanda hii bongo usipokuwa makini wafwaaaa.

Mm nilivyoona usumbufu umezidi nilipiga moyo konde nikaachini nikafanya kazi. Nilitengeneza offer letter ya ajira kutoka kampuni moja yakibumba ya nchini Marekani. Ile offer letter ilikuwa inatisha ukiiangakia lazima upagawe, mshahara na marupurupu ya maana sana. Nikatika zangu uhamiaji.
Nikajaza mafomu yao nikasogea dirishani, kuingalia tuu, wakashangaa, vipi, nikawaambia kuna anko yupo mbele ni baharia kanisukia dili, na nikamwambia kama una dogo wewe muandae tu mm namsaidia mbona.

Kwenye barua nimeonyesha zimebaki siku 5 kuondoka so pass inatakiwa ndani ya siku 3. Akaniambia haiwezekani. Nikamwambia nielekeze kwa bosi nimpe contacts za anko antwangie na ukumbuke anko hewa yuko USA. Haaa basi ntakusaidia. Mwanangu ndani ya siku 3 nikakamata pass.

Ilifikia mahali kutokana na usumbufu nikaamua kujichongea mihuri mwenyewe. Nikitakiwa barua ya serikali za mitaa, nazama kwa pc naprint, naigonga muhuri nakuletea. Bongo tunachoshana sana jamani.
 


Asee hongera zake, alijitoa mhanga haswa. Maelezo mubashara pia.
Ila kwa sasa hali haitabiriki sana katika baadhi ya nchi watu wengi walizoea kuishia, labda kwa hizo za ulaya.
Kwa North America labda Canada. Tena prime minister alisema juzi wanakaribisha asylum seekers kutoka States. Sasa sijui nchi nyingine kama watakaribiswa the same way.
 
Reactions: BAK
Kweli bongo nyoso
 
Hapana mkuu! nikishapata citizenship ya nchi nyingine, uraia wa tz una cease automatically. Btw, napata shida kurudi ku-rew passport inapoisha ama kujaa...
Haya kila lenye heri mkuu, ila tu fanya kuwa kumbuka wajomba inapofika x-mass.
 

siku hizi hata hawakubali kabisa wadada chini ya 25 yrs old, au mtu asiye na elimu wa miaka chini ya 40 kuingia ulaya kwa sababu wanajua watatafuta wachumba vibabu, au vi bibi juu ya ujanja ujanja ili wapate makaratasi. na pia inakuwa ni migo kwa taifa kuanza kukuhuduma au kukusomesha, na siku hizi kazi za bila elimu hazipo siku hizi, juu ya wahamiaji ni wengi na wakimbizi ni wengi, wameongeza msharti sana jamani hadi huruma kwa wale wanajipanga sasa kuingia ulaya wanabidi wawe na sababu haswa yenye kueleweka ili wapate Visa ya kuingia.
 
We jamaa ni noma sana. Tiririka kmanda wabongo sisi roho za korosho sana. Mbongo anaweza kukata mikono ili nyoka akugonge ufilie mbali.
 
Nilisikia ukioa au kuolewa na mtu kutoka developing countries lazima uonyeshe income ya kuanzia £25,000 kwa mwaka kabla hujamfile, hii ni kuthibitisha hatapata shida wala kutegemea social funds. Sijui kama ni ya kweli, mbona majanga.
 
Nilisikia ukioa au kuolewa na mtu kutoka developing countries lazima uonyeshe income ya kuanzia £25,000 kwa mwaka kabla hujamfile, hii ni kuthibitisha hatapata shida wala kutegemea social funds. Sijui kama ni ya kweli, mbona majanga.
ni kweli
 
Nikipata sehemu pa kujilipua, najilipua mpaka akili.. Tanzania maisha yanakua magumu kila siku, mwenye namna ya kupata scholarship aweke hapa nijaribu hizo bahati..
Mambo ya scholarship jamani mtuwekee, mm hadi naona kero, ukijipanga kuomba vyuo kama 10 duuu utazuguka kwenda kuchukua barua za reference kwa malecturer hadi ukome. Mm nilitaabika sana, kila siku nipo chuo kuomba reference letter, jamaa hawapatikani, email zao kama za maroboti hazijibiwe.

Nikaamua kujilipua kwa kuchonga muhuri wa department, logo yao ipo kwanet, recommendation najifanyia mwenyewe sitaki ujinga kabisa.

Mwaka juzi nikapata admission Coventry University - MSc Oil and Gas Management, scholarship zinapitia wizara ya elimu, natimba mjengoni wananiuliza wewe umejuaje kama kuna scholarahip, nikawafungulia pc nikawaonyesha tangazo kwenye website yao. Daaaa nilijua tu hapa sina changu. Nilikosa scholarship ile.

Bongo nihatari sana, inawezekana leo hio tungekuwa mbali sana na kuwa na wataalamu wa kila aina, lakini wapiiii.
 
Huwa ninakwenda kusali Portugal sehemu inaitwa Fatima (wa-Katoliki wataelewa), sasa mara ya kwanza nimekwenda vizuri, kurudi na passport yangu ya kijani nimebeba picha na sanamu za mama Maria, nyingine zilikuwa za jumuai, nyingine ni zawadi za watu wa karibu. Lisbon Air Port sasa kuonekana mwanamke mweusi na passport ya kijani, niliulizwa mara mbili mbili unatoka wapi, begi lilifunguliwa, sanamu zilipitishwa kwenye screen. Uzuri wake, niliondoka Fatima saa nne asubuhi wakati ndege yangu ilikuwa saa nne usiku.
Baadae ndiyo ninaelewa kuwa ili ni njia ya wasafirishaji madawa na walinishuku kuwa ninaondoka na mzigo.
 
Dah mkuu embu nielekeze hayo maujanja yako ili kesho morning tu nitie maguu migration coz nasafari ya kenya halafu migration wanizingua tu.
 
China kuzuri kununulia simu na nguo lakini ukitaka kujilipua mmmh!uhakika wa kutoboa ni mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…