Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mimi nimewekeza kweny elimu kwa miaka 15, nina degree mshahara mdogo, nipo kazini bado kazi zinabana ziwez fanya biashara, nitaendelea kujiwekeza kwenye elimu hasa ya nje ili kutoka. Ningeamua kufanya biashara basi ningekomea form 4 au la saba
 
Mkuu Tokyo40 tumekusaka sana na Richard mdau wetu kwema? Karibu sana mkuu

Asante kwa hiyo link hopeful wadau wataiona..... Unaweza kutoa hints nyingine....

Kwa Japan, njia rahisi ni kwa ndoa. Watu hawaoani huku wala kuzaliana. Wanigeria wanaoa kila siku na Wajapani.

Kwa kusoma hapa, mpaka uletwe na serikali. Scholarship wanatoa kuanzia Ph.D level.

Unaweza kuja kwa kusoma Kijapani. Naifahamu shule moja ya lugha, gharama ni $1000 kwa mwezi. Wachina wanakuja hivo na kutafuta maisha wakiingia. Pia, viza hazina tabu za kuishi. Unaweza kusoma hapo kwa $500, na $500 unalipa chumba katika dorm yao. Pia, viza yako ya mwaka unaruhusiwa kufanya kazi na shule ina contact na makampuni. Baada ya hapo, akili kichwani.

Maisha ya Japan sio ghali kama unavyosoma katika magazeti. Unaweza kula kwa $10 kwa siku na kushiba. Kazi zipo nyingi tu, viwandani wanatafuta wafanyakazi, Wajapani hawazitaki na hawataki kuzaa. Kama ukitaka, nimeweka link ya vyumba vya kulala vya $500 kwa mwezi kutoka kwa agent. Unaishi kigeto, katika chumba kimoja, katikati ya jiji la Tokyo. Mgeni yoyote anakaribishwa.

Shule ya Kijapani: 東京近郊埼玉県さいたま市の日本語学校

Chumba Tokyo: www.realestate.co.jp
 
Mkuu fungu kiasi gani..
Kwa bongo sasa hivi pass zinazingua saana kupata ni mpaka uwe na safari ya uhakika na uwe na vithibitisho.

Ila unaweza tumia njia za nyuma kuipata japo siyo nzuri ila kuna muda inabidi tuzitumie.
Tenga kilo 150 ila kiuhalali ni 50 tu kuna watu wanafanya hii nenda na viambatanisho vyako vyote ndani ya wiki una pass yako Mkononi.
 
Poa asante..mkuu
 
ni mara yangu ya kwanza kuona mtanzania anatoa njia kwa wenzake kwenda nje...watanzania wengi n wabnafs wakishafankiwa wao hawatak wenzao wafankiwe
Mm toka mwezi wa 10 mwaka jana natafuta mtu wa kunisaidia kuweza kusoma South Afrika hawajitokezi tena nisaidiwe kuelekezwa tuuu sio kusomeshwaaa lakini kimyaaaaaa.....Japo mtu aniambie andaa bajeti kiasi fulani kwa mwaka lakini kimyaaa
 
Daah mkuu umenikumbusha mbali na huu mji... Binafsi niliupenda mno pamoja na Malmo....

Malmo safi sana.

Mimi nilifika wakati pasi zetu tulikuwa tunapewa viza miezi mitatu uwanjani, na ukiingia nchi moja ya Nordic, unaruhusiwa zote.

Nikajikuta juu huko Lapland mpaka Trondheim, Norway na Kuopio, Finland.

Good memories.
 
Mkuu ngoja nikipata time nitakuja na ramani yote ya vita kazi itabaki kwenu wenyewe
 
Tomb huyu jamaa akileta ramani uniite.
Mkuu ngoja nikipata time nitakuja na ramani yote ya vita kazi itabaki kwenu wenyewe
 
Malmo safi sana.

Mimi nilifika wakati pasi zetu tulikuwa tunapewa viza miezi mitatu uwanjani, na ukiingia nchi moja ya Nordic, unaruhusiwa zote.

Nikajikuta juu huko Lapland mpaka Trondheim, Norway na Kuopio, Finland.

Good memories.
Sana, ktk miji ya Sweden niliupenda mno Malmo...
 
ni mara yangu ya kwanza kuona mtanzania anatoa njia kwa wenzake kwenda nje...watanzania wengi n wabnafs wakishafankiwa wao hawatak wenzao wafankiwe
Hao hao watanzania ukiwasaidia wanakuwa Nyoka tu...
Tunajuana so hakuna wakumlaumu mwenzie Tabia zetu ndio Tatizo Ukiamua kumsaidia Mtanzania ukubali chochote kibaya atakachokufanyia ndio maana wengine hawataki hayo mambo kila MTU apambane mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…