Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Humu kuna kenge wanataka kutuharibia mada yetu. Tulishasema sisi watanzania wengi roho zetu mbaya sana. Lijitu halikibalinkuona kuwa hapa kuna tija itapatikana yeye anakuna na sera zakisiasa zilizoshindwa kuondoa hata kuharisha damu kwa mji kama wa dar for more than 50 years.

Wapumbavu hawa wanashindwa kuandaa mada zao wakazileta ili watu wachangie wao kutwa kuzichafua nyuzi za maana, watu wako speed 250 yeye anaweka ligogo la mbuyu njiani. Yote haya ni kutokana na roho mbaya.

Kwani nani kamwambia kuwa lazina watanzania wote waondoke waende ulaya. Halafi kila anayeona kuna haja ya kuondoka ujue tayari ameshajaribu mambo kadhaa na kuona hayamtoi na hawezi toka. Wapo wenye ramani zao bongo wanaiba pesa daily huwezi kumwambia anaqeza kwenda kuiba pesa england, watamkata makende kweupee na hafimishi hata siku mbili.

Watu wanajifanya wachambuzi wa mambo ya kilimo na ujinga mwingine usio na maana wakati babu zetu walilima for than century wamepata nini kwa bongo hii zaidi yakupinga viuno tu. Wewe uliona wapi mbolea izalishwe tz alafi mfuko wa parking uandikwe made in kenya? Hii nchi si wazimu mtupu?

Machungwa muheza yabaharibika, sasa unataka watu zaidi waendelee kulima machungwa na peasi watauza wapi? Dumila nyanya zilioza mashambani hakuna pakupeleka, leo unataka watu zaidi walime nyanya watauza wapi?

Vijana graduate wapo mitaani, hawana mitaji, hawakopesheki, hawana lakufanya, mkilala mkiamka mnawaambia fanyeni kazi, mnatumia viungo gani kufikiti jamani?

Hawa jamaa wanakera sana,
 
Hii nchi ya uzulumishi sana.unatafuta kwa nguvu nyingi unanyang'anywa kirahis.mfano mzuri ishu ya viroba.ni bora nijilipue mambele hamna namna.nikuache bro uendelee kupiga porojo mana inaezekana hata wewe haupo bongo land
Eti mtu anasema haondoki africa anahisi akijifungia africa ndio atapata maendeleo. Haya muulize tangu huo uhuru wa bendera wa africa kuna kiwanda cha smartphone? Anavaa majani ya mpapai au jeans from usa? Anakula kwa vijiko vya china au anatumia visu vya tameco?

Anaendesha gari ya nyumbu au toyota ya mjapan? Anapanda bajaji za muhindi au baiskeli za miti za wasukuma? Hata pedi tunaagiza kutoka nje utasema kwenda alaya ni ukoloni si yaleyale tu
 

sio hawaondoki wakipata wanaondoka ni majibu ya mkosaji mzee.... leo wenye pesa za nafuu tanzania karibu wote wamezunguka zunguka duniani hawakukaa kujifungia kama wengine wanavyo lazimisha wengine wawe vipofu ili wao waendelee kuona...
 
Very usefull thread niko mubashara kabisa kudukua mawili matatu ,,,,watu wamechoka! Ila bora kuchoshwa ili upige hatua , uthubutu na uoga pembeni ,,,,wenye fursa mbalimbali pia nashaurii watutupie huku kama kazi,ufadhili wa masomo pia ma agents tupieni mawasiliano
 
Ndugu zako ni mapoyoyo, kama hesabu inapanda vizuri, na kimalkia unakijua jilipue na GRE na English exams then zama kwenye web mwenyewe. Mi nilipita njia hiyo, nikamaliza nikaendelea kupiga mzigo kwa Obama. Bongo kwa likizo tu.
Mkuu naomba uiongelee kidogo hii mitihani. Huwa inanikata stimu sana napotafuta Scholarship.
 
Hahaa kwenye hii ishu ya ku host wageni nitaomba wabongo tuwe makini sana kwani wazungu ni tofauti kabisa na sisi.

Binafsi nimefanya kazi za utalii kupeleka wageni mbuga za wanyama na mt Kilimanjaro, mgeni anaweza akakuzoea kiasi kwamba anakukiss, hugg na bla blaa nyingi tu lakini hamaanishi mfanye ma....penz, na ukiloba tu hapo umeharibu kila kitu ... Hapa sijui nieleze vipi.

Kuna mkasa mmoja uliwahi kutokea waiter asubuh aliingia kwenye hema la mgeni ili kuwapatia bed tea akafungua zip ya mlango bila kugonga hodi, wageni kumbe walikuwa bila nguo wanafanya michezo ya usiku, gafla bin faster jamaa Si akawa kesha wapiga chabo bila kuwaona.....kilichofuata waligoma kuendelea na safari.

Tuliwabembeleza sana lakini walikataa kuna pesa ambao kwa kawaida hutoa inaitwa Tip. Sio mshahara ni kama zawadi lakini ni lazima itolewe kikawaida nayo waligoma kutoa yani kiufupi kwa kukosea kwa waiter kugonga kabla ya kuingia kazi yote iliharibika.

Somo hapa waweza kukaa na mtu kwa miezi 3 then yote ukaharibu ndani ya siku 1 na ikawa kazi bure.

[HASHTAG]#mkuu[/HASHTAG] Izzo nimejiregister help stay lakini sijafanikiwa kupata watalii nazani kwa maelezo yako utafungua njia na kwa kuwa nina uzoefu wa kuishi na wazungu wa nchi mbalimbali sitokuangusha ukinipatia nafasi kuwa host family.

Pia wageni kama hao wanapendelea zaidi kukaa ndani ya familia kujifunza tamaduni na kutembelea maeneo ya utalii sio mtu unakaa na mgeni ndani unamletea muvi tu alafu wewe uko busy na smartphone.

Kwa hili ubunifu unahitajika pili host anapaswa kuwa na average behavior, not too hursh, careless. Standard living neither too poor nor rich.

Mwisho kabisa ukiwa host never disclosure all of your potential to your client. Hapa ndio msemo wa ukifaa na kiu baharini we ni mzembe unaingia, wazungu ni wajanja sana na mara nyingi hawafanyi kitu kwa bahati mbaya anaweza kukupima degree za uvumilivu, uaminifu na mengine mengi kupitia vitu vidogo vidogo sana. Ndio maana nasisitiza don't take opportunity of being host for granted
 
...ukishatapeliwa fanya kurudi kwenye hii comment ukumbuke nilichoandika! Naona watu povu zinawatoka wanapinga hoja kwa matusi na lugha kali. Hivi hata huko malta, utakwenda kwa miguu?
 
How did you do that ?

Mimi nimeanza na kuchoma chips hapa Kwamtogole na nina kamgahawa kadogo, lakini hali ni tete sana.

Tupe uzoefu wako, ulitokaje?
Huyu jamaa atakua kwenye vikundi vyao Vya elnet sjui forever liv so he hopes so[emoji102]
 


Boss fanya yafuatayo; andika tena ukitumia l na r kwa ufasaha na tuelewe wapi ni mwanzo na mwisho wa sentensi. Mental slavery ni kuamini kuwa huko kwa wazungu ndio kutakapompatia mtu mafanikio ilihali resources/malighafi kule ziko limited wao wanawaza kila uchao namna wanavyoweza kurudi huku kuexploit zaidi. Tanzania ni moja ya resource rich country -- sijui hata kama unanielewa
 
Huwa nawadharau sana hawa watu....
unakuta jitu linaloongea huo ujinga ..halina lolote linategemea Makombo anayoiba Shemeji yake.... eti awamu ya 5 Demit[emoji16] [emoji16]
 
Nilichokigundua anasema haondoki huku wanatuimiza tuendelee kubaki hapa ikiwa yeye hayupo afrika siku nyingi.na huo ni ubinafsi wa hali ya juu.Tanzania sio sehem sahihi ya kuishi tena.just imagine
1:mgonjwa wa mguu anafanyiwa opereshen ya kichwa anakufa.ni tanzania tu
2:mgonjwa wa moyo ananyimwa passport ya kwenda kufanya matibabu anakufa,
3😛esa za rambirambi zinaliwa bila huruma wananchi wanaambiwa ardhi ya kijani
4:wakina ben wanapotea kirahisirahisi na nchi haifatilii
5:biashara halali inafanywa haramu kama ya viroba unafilisiwa faster hata ukijiua hatujali
6:wasomi kibao wanashinda vijiweni,kazi zote wanapewa expert kutoka nje hadi machinga kariakoo.
7:nchi tunayonyanyaswa na wageni
8:nimechoka kuielezea inanipa hasira
 
ulipoona zimekosewa lekebisha....
 
Thank you Kaveli lakini JF imesaidia sana kututoa point moja kwenda nyingine,na hizi mambo unazozimwaga hapa watu tunafunguka
 

Pinda awataka watanzania kuwekeza nje ya nchi

eb soma hapo unaweza pata kitu...
 

:: Balozi Wa Tanzania Nchini Burundi Amewataka Watanzania Kuwekeza Nchini Burundi
pita na hapa watu wapo nje lakini wanakumbuka kwao... sijui unaokota nini humo katika hizo zaga....
 
Mkuu naomba uiongelee kidogo hii mitihani. Huwa inanikata stimu sana napotafuta Scholarship.
Hizi exams naona inategemea na chuo
Mimi nimeapply scholarship vizuri wakawa wanataka hiyo mitihani nikawa tumia barua ya UDSM,wakagoma.
Ikabidi niwaulize nifanyeje wakasema nitafute agent wa chuo chao hapa TZ,nika search hakuna agent, ni karudi kuwaambia hakuna agent wao tz
Wakasema watanitumia online English test ya lisaa na nusu,kweli walituma nikafanya hiyo test nika submit,wakarudisha majibu mana test walinitumia wengine kabisaa so matokea wakayapeleka chuo nilichoomba,hicho chuo wamenitumia admission form nizijaze zikiwa zinahitaji referee na mwajili aseme kitu kuhusu mimi
Fomu ya mwajiri nimejaza mwenyewe nampelekea J3 assign,kuna fomu ya kujieleza kuhusiana na kozi unayoomba that's all.
Kwahyo tusikate tamaa tuendelee kujaribu kuomba na kuomba siku moja Mungu atasikia.
 
Mkuu heshima kwako... Umemaliza kitu kuhusu wabongo.


Binafsi mimi hizi roho nyeusi za wabongo ni moja wapo ya sababu kuu ni kwanini naona Tanzania sio mahala pazuri pakuendelea kuishi.
 
Mkuu labda chuo gani Hicho
 
Naomba Link hiyo na Mimi niombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…