Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Wewe unaishi Africa ipi....
unazungumzia Nchi ambayo Raisi anajigeuza kuwa mungu anachosema yeye ndio mwisho Tanganyika hii tuna zaidi ya miaka 50 tangu Uhuru hivi unayohabari Mwaka wa Jana wakulima wa Nyanya walivuna nakulisha Ng'ombe...au Mwenzetu ni miongoni mwa wanufaika wa Nchi hii kiasi kwamba hamjui Taabu wanazokutana nazo wadanganyika.....
Humu kuna kenge wanataka kutuharibia mada yetu. Tulishasema sisi watanzania wengi roho zetu mbaya sana. Lijitu halikibalinkuona kuwa hapa kuna tija itapatikana yeye anakuna na sera zakisiasa zilizoshindwa kuondoa hata kuharisha damu kwa mji kama wa dar for more than 50 years.

Wapumbavu hawa wanashindwa kuandaa mada zao wakazileta ili watu wachangie wao kutwa kuzichafua nyuzi za maana, watu wako speed 250 yeye anaweka ligogo la mbuyu njiani. Yote haya ni kutokana na roho mbaya.

Kwani nani kamwambia kuwa lazina watanzania wote waondoke waende ulaya. Halafi kila anayeona kuna haja ya kuondoka ujue tayari ameshajaribu mambo kadhaa na kuona hayamtoi na hawezi toka. Wapo wenye ramani zao bongo wanaiba pesa daily huwezi kumwambia anaqeza kwenda kuiba pesa england, watamkata makende kweupee na hafimishi hata siku mbili.

Watu wanajifanya wachambuzi wa mambo ya kilimo na ujinga mwingine usio na maana wakati babu zetu walilima for than century wamepata nini kwa bongo hii zaidi yakupinga viuno tu. Wewe uliona wapi mbolea izalishwe tz alafi mfuko wa parking uandikwe made in kenya? Hii nchi si wazimu mtupu?

Machungwa muheza yabaharibika, sasa unataka watu zaidi waendelee kulima machungwa na peasi watauza wapi? Dumila nyanya zilioza mashambani hakuna pakupeleka, leo unataka watu zaidi walime nyanya watauza wapi?

Vijana graduate wapo mitaani, hawana mitaji, hawakopesheki, hawana lakufanya, mkilala mkiamka mnawaambia fanyeni kazi, mnatumia viungo gani kufikiti jamani?

Hawa jamaa wanakera sana,
 
Hii nchi ya uzulumishi sana.unatafuta kwa nguvu nyingi unanyang'anywa kirahis.mfano mzuri ishu ya viroba.ni bora nijilipue mambele hamna namna.nikuache bro uendelee kupiga porojo mana inaezekana hata wewe haupo bongo land
Eti mtu anasema haondoki africa anahisi akijifungia africa ndio atapata maendeleo. Haya muulize tangu huo uhuru wa bendera wa africa kuna kiwanda cha smartphone? Anavaa majani ya mpapai au jeans from usa? Anakula kwa vijiko vya china au anatumia visu vya tameco?

Anaendesha gari ya nyumbu au toyota ya mjapan? Anapanda bajaji za muhindi au baiskeli za miti za wasukuma? Hata pedi tunaagiza kutoka nje utasema kwenda alaya ni ukoloni si yaleyale tu
 
sio hawaondoki wakipata wanaondoka ni majibu ya mkosaji mzee.... leo wenye pesa za nafuu tanzania karibu wote wamezunguka zunguka duniani hawakukaa kujifungia kama wengine wanavyo lazimisha wengine wawe vipofu ili wao waendelee kuona...
 
Very usefull thread niko mubashara kabisa kudukua mawili matatu ,,,,watu wamechoka! Ila bora kuchoshwa ili upige hatua , uthubutu na uoga pembeni ,,,,wenye fursa mbalimbali pia nashaurii watutupie huku kama kazi,ufadhili wa masomo pia ma agents tupieni mawasiliano
 
Ndugu zako ni mapoyoyo, kama hesabu inapanda vizuri, na kimalkia unakijua jilipue na GRE na English exams then zama kwenye web mwenyewe. Mi nilipita njia hiyo, nikamaliza nikaendelea kupiga mzigo kwa Obama. Bongo kwa likizo tu.
Mkuu naomba uiongelee kidogo hii mitihani. Huwa inanikata stimu sana napotafuta Scholarship.
 
Ndugu zangu Watanganyika baada ya kuja na Option number one ya Malta sasa ni Option number 2 nia ni kutaka ndugu na jamaa zetu muweze kutimiza ndoto zenu za kutafuta maisha nje ya JPM empire ambako kumeonekana kama mwiba kwa ajira za vijana na maendeleo ya hasa vijana

Baada ya Option ya Malta kuonekana ni ngumu japo sijui ugumu wake ni nini lakini si mbaya kuna Option namba 2 mpaka 3 lakini leo tunaendelea na Option number 2

OPS (Mission)
Mission hii inahusu nchi za Canada, USA, Germany , Denmark, Norway, Sweden na Malta

Kuhusu USA mm binafsi sipendelei mje US coz siasa za US dhidi ya wageni zimebadilika sana kumekuwa na siasa za utengano dhidi ya wageni

Ok tuendelee nimekuwa karibu na kufanya kazi na taasisi ktk nchi zote nilizozitaja taasisi hzo zinadeal na vijana ktk maswala ya culture exchange ambapo kila mwaka wamekuwa wakichukua vijana kwenda nchi mbalimbali duniani kwenda kujifunza tamaduni zingine na Lugha pia kubadilishana mawazo kama vijana umri wa vijana ni kuanzia miaka 18-30 vijana wa kiume na wakike sasa ni mm kuongea na taasisi hzo waanze kuleta vijana hao Tanganyika lakini utaratibu ni

1 Wanataka Host wa nchi wanayokwenda so kila kijana anapata Host wa nchi husika kwa ajili ya kumtembeza na kuwa mwenyeji wake

2 Kama unakuwa host wake atakaa kwako kwa kipindi chote ambacho ni kuanzia mwezi 1-3 so atakaa kwako si hotel au nyumba za wageni A.K.A (machinjioni)

3 Kila siku yeye atachangia dola 100 kama mchango wa chakula na malazi

4 Kumtembeza sehemu mbalimbali za ndani ya mkoa mfno DSM lakini akitaka kutoka nje ya dar gharama za wote wawili zitakuwa juu yake na gharama kama za kwenda disco na beach zitakuwa juu yake

5 kuhusu kukaa hata uwe na chumba kimoja ila yawe ni maeneo safe choo kiwe kizuri

MISSION YENYEWE
Kama ni mtoto wa kiume utakaa na mtoto wa kike kama ni wakike utakaa na wakiume lakini wenyewe hawajali.njinsia so kama utapenda kukaa na wajinsia yako pia ni sawa tu cha muhimu ni kutengeneza conection tu

ANGALIZO
Wazungu kitendo cha kulala kitanda kimoja na mtu wa jinsia tofauti kwao si tatizo kubdilisha nguo na kubaki na chupi mbele ya jinsia tofauti pia si jambo gumu kwao so hasije fanya hvyo ukaona kakuzimia au anakutega utakuwa wrong sana

Sasa bhasi kitendo cha mtu kukaa kwako miezi 2 au 3 usipo tengeneza conection naye utakuwa mpumbavu sana na kama utakuwa mjanja unaweza kuanzisha mahusiano ya kimapenzi naye kwani wengi ni vijana wa 18-25 lakini mission ni ww kutengeneza conecton kupitia huyo mgeni kwani mtaendelea kuwasiliana na yeye kukualika kwao ni vyepesi sana so nimekupa nyavu na mtumbwi kuvua samaki ni juu yako akili kumkichwa

CHANGAMOTO
Changamoto kubwa ya hii project ni usalama wa wageni kwani humu tunajuana kwa fake id so kumpa mtoto wa watu mtu ambae umjui ni swala la ujasiri na lenye kuitaji akili ya kuvukia barabara inaitaji ujitoe akili lakini ninauwezo wa kuwasiliana na hizo taasisi kwani tunafanyanazo kazi na kuheshimiana tatizo usalama wa hao wageni na hao unaowakabidhi mgeni huyo unamjua asije mchinja mtoto wa watu usiku dah

Kila mgeni na host mmoja na uhakika ni kupata wageni 20-30 kutoka nchi nilizotaja hapo juu kwa mwaka

Kumbuka wageni ni wakike na wakiume so chance ni kwa dada na wakaka wa Tanganyika

Mnaweza kuwatag member wengine wa thread hii na ambao wameonyesha nia ya kutoka na ambao wana michango yao kwenye thread hii ambao awajachangia achaneni nao

kirikou1 kweupee Hary Jay Ndata Prishaz WiseLady Mrike wembeee talentboy Dr.adams faida Daby Tombstone Piledrive Padri Mcharo Shyshii lucley kui tagamwa binti kiziwi dangadunguri Tembo2 lusungo kweupee pius1021 Prof cognition Agogo Jr Chakochangu soul provider Mrike
Hahaa kwenye hii ishu ya ku host wageni nitaomba wabongo tuwe makini sana kwani wazungu ni tofauti kabisa na sisi.

Binafsi nimefanya kazi za utalii kupeleka wageni mbuga za wanyama na mt Kilimanjaro, mgeni anaweza akakuzoea kiasi kwamba anakukiss, hugg na bla blaa nyingi tu lakini hamaanishi mfanye ma....penz, na ukiloba tu hapo umeharibu kila kitu ... Hapa sijui nieleze vipi.

Kuna mkasa mmoja uliwahi kutokea waiter asubuh aliingia kwenye hema la mgeni ili kuwapatia bed tea akafungua zip ya mlango bila kugonga hodi, wageni kumbe walikuwa bila nguo wanafanya michezo ya usiku, gafla bin faster jamaa Si akawa kesha wapiga chabo bila kuwaona.....kilichofuata waligoma kuendelea na safari.

Tuliwabembeleza sana lakini walikataa kuna pesa ambao kwa kawaida hutoa inaitwa Tip. Sio mshahara ni kama zawadi lakini ni lazima itolewe kikawaida nayo waligoma kutoa yani kiufupi kwa kukosea kwa waiter kugonga kabla ya kuingia kazi yote iliharibika.

Somo hapa waweza kukaa na mtu kwa miezi 3 then yote ukaharibu ndani ya siku 1 na ikawa kazi bure.

[HASHTAG]#mkuu[/HASHTAG] Izzo nimejiregister help stay lakini sijafanikiwa kupata watalii nazani kwa maelezo yako utafungua njia na kwa kuwa nina uzoefu wa kuishi na wazungu wa nchi mbalimbali sitokuangusha ukinipatia nafasi kuwa host family.

Pia wageni kama hao wanapendelea zaidi kukaa ndani ya familia kujifunza tamaduni na kutembelea maeneo ya utalii sio mtu unakaa na mgeni ndani unamletea muvi tu alafu wewe uko busy na smartphone.

Kwa hili ubunifu unahitajika pili host anapaswa kuwa na average behavior, not too hursh, careless. Standard living neither too poor nor rich.

Mwisho kabisa ukiwa host never disclosure all of your potential to your client. Hapa ndio msemo wa ukifaa na kiu baharini we ni mzembe unaingia, wazungu ni wajanja sana na mara nyingi hawafanyi kitu kwa bahati mbaya anaweza kukupima degree za uvumilivu, uaminifu na mengine mengi kupitia vitu vidogo vidogo sana. Ndio maana nasisitiza don't take opportunity of being host for granted
 
...ukishatapeliwa fanya kurudi kwenye hii comment ukumbuke nilichoandika! Naona watu povu zinawatoka wanapinga hoja kwa matusi na lugha kali. Hivi hata huko malta, utakwenda kwa miguu?
 
How did you do that ?

Mimi nimeanza na kuchoma chips hapa Kwamtogole na nina kamgahawa kadogo, lakini hali ni tete sana.

Tupe uzoefu wako, ulitokaje?
Huyu jamaa atakua kwenye vikundi vyao Vya elnet sjui forever liv so he hopes so[emoji102]
 
nchi inayokumbwa na upungufu wa chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa... nchi huduma za kijamii si zakulizisha... nchi ambayo mambo mengi hayaendi kama wananchi wanavyotalajia ndo maana hata wewe una sapoti watu waende kusoma watu waende kama wana utaalam hivyo ni hila na hasira zako kwa watu kuona wanaondoka kutimiza ndoto zao kwa kuajialiwa au kujiajiri huko waendapo ambapo wataweza kusave kiasi na kukileta kwao kitaweza kumpa uwezo wa kumiliki greenhous ambayo sasa ni ngumu kwa kijana kumiliki kutokana na gharama kuwa kubwa... wanakaa nyumbani wakiwa wamekata tamaa ya kukosa ajira kukosa mikopo ya kuendeleza au kufikia sehemu ya ndoto zao... njoo na vitu vya kueleweka nyinyi ndio mnataka watu wajiajiri bila ya mitaji alafu hapo hapo kodi ni kubwa rushwa pia mahitaji ya nyumbani (kwa wategemezi)... ni bora mtu kufanya anachoweza kufanya kiliko kushikiliwa akili mental slave ni kitu kibaya watu au mtu ili kuweza kufanikiwa ni lazima afanye kile anachoweza kukifanya kuliko kumpush kufanya hasichoweza hivyo hacha watanganyika wafanye wanachowezafanya bila kuvunja sheria za nchi mkuuu...! mwisho kabisa nibora ukaja na page yako ya kuhamasisha na kuwaonyesha watanganyika njia wanazoweza kupitia ili wafanikiwe hapa hapa maana hii page haiendani na mawazo yako mkuu... ni sawa na yule aliyekuja na post ya bit coin... katika page ambayo si sahihi na wazo lake...

Boss fanya yafuatayo; andika tena ukitumia l na r kwa ufasaha na tuelewe wapi ni mwanzo na mwisho wa sentensi. Mental slavery ni kuamini kuwa huko kwa wazungu ndio kutakapompatia mtu mafanikio ilihali resources/malighafi kule ziko limited wao wanawaza kila uchao namna wanavyoweza kurudi huku kuexploit zaidi. Tanzania ni moja ya resource rich country -- sijui hata kama unanielewa
 
Humu kuna kenge wanataka kutuharibia mada yetu. Tulishasema sisi watanzania wengi roho zetu mbaya sana. Lijitu halikibalinkuona kuwa hapa kuna tija itapatikana yeye anakuna na sera zakisiasa zilizoshindwa kuondoa hata kuharisha damu kwa mji kama wa dar for more than 50 years.

Wapumbavu hawa wanashindwa kuandaa mada zao wakazileta ili watu wachangie wao kutwa kuzichafua nyuzi za maana, watu wako speed 250 yeye anaweka ligogo la mbuyu njiani. Yote haya ni kutokana na roho mbaya.

Kwani nani kamwambia kuwa lazina watanzania wote waondoke waende ulaya. Halafi kila anayeona kuna haja ya kuondoka ujue tayari ameshajaribu mambo kadhaa na kuona hayamtoi na hawezi toka. Wapo wenye ramani zao bongo wanaiba pesa daily huwezi kumwambia anaqeza kwenda kuiba pesa england, watamkata makende kweupee na hafimishi hata siku mbili.

Watu wanajifanya wachambuzi wa mambo ya kilimo na ujinga mwingine usio na maana wakati babu zetu walilima for than century wamepata nini kwa bongo hii zaidi yakupinga viuno tu. Wewe uliona wapi mbolea izalishwe tz alafi mfuko wa parking uandikwe made in kenya? Hii nchi si wazimu mtupu?

Machungwa muheza yabaharibika, sasa unataka watu zaidi waendelee kulima machungwa na peasi watauza wapi? Dumila nyanya zilioza mashambani hakuna pakupeleka, leo unataka watu zaidi walime nyanya watauza wapi?

Vijana graduate wapo mitaani, hawana mitaji, hawakopesheki, hawana lakufanya, mkilala mkiamka mnawaambia fanyeni kazi, mnatumia viungo gani kufikiti jamani?

Hawa jamaa wanakera sana,
Huwa nawadharau sana hawa watu....
unakuta jitu linaloongea huo ujinga ..halina lolote linategemea Makombo anayoiba Shemeji yake.... eti awamu ya 5 Demit[emoji16] [emoji16]
 
Eti mtu anasema haondoki africa anahisi akijifungia africa ndio atapata maendeleo. Haya muulize tangu huo uhuru wa bendera wa africa kuna kiwanda cha smartphone? Anavaa majani ya mpapai au jeans from usa? Anakula kwa vijiko vya china au anatumia visu vya tameco?

Anaendesha gari ya nyumbu au toyota ya mjapan? Anapanda bajaji za muhindi au baiskeli za miti za wasukuma? Hata pedi tunaagiza kutoka nje utasema kwenda alaya ni ukoloni si yaleyale tu
Nilichokigundua anasema haondoki huku wanatuimiza tuendelee kubaki hapa ikiwa yeye hayupo afrika siku nyingi.na huo ni ubinafsi wa hali ya juu.Tanzania sio sehem sahihi ya kuishi tena.just imagine
1:mgonjwa wa mguu anafanyiwa opereshen ya kichwa anakufa.ni tanzania tu
2:mgonjwa wa moyo ananyimwa passport ya kwenda kufanya matibabu anakufa,
3😛esa za rambirambi zinaliwa bila huruma wananchi wanaambiwa ardhi ya kijani
4:wakina ben wanapotea kirahisirahisi na nchi haifatilii
5:biashara halali inafanywa haramu kama ya viroba unafilisiwa faster hata ukijiua hatujali
6:wasomi kibao wanashinda vijiweni,kazi zote wanapewa expert kutoka nje hadi machinga kariakoo.
7:nchi tunayonyanyaswa na wageni
8:nimechoka kuielezea inanipa hasira
 
ulipoona zimekosewa lekebisha....
Boss fanya yafuatayo; andika tena ukitumia l na r kwa ufasaha na tuelewe wapi ni mwanzo na mwisho wa sentensi. Mental slavery ni kuamini kuwa huko kwa wazungu ndio kutakapompatia mtu mafanikio ilihali resources/malighafi kule ziko limited wao wanawaza kila uchao namna wanavyoweza kurudi huku kuexploit zaidi. Tanzania ni moja ya resource rich country -- sijui hata kama unanielewa
 
Among other factors, nadhani baadhi ni:

- Uoga wa maisha. We are extremely fearful of life. We can't take risk ktk utafutaji, tunasahau kwamba there's nothing risk-free in life struggle.

-Lack of international exposure kwa wazazi wetu. Most of us tumezaliwa na kukulia kwenye families ambazo hazikuwa 'global goers'. As such, na sisi tunaishia in the same circle... mtu anapanda Ngorika all the way from sitimbi to Darisalamu, then hiyo ndo maximum exposure ya ndoto zake... kutia maguu Daresalamu.

-language barrier. Hili liko wazi. Wabongo wengi 'kutema yai' ni shuhuli nzito. English is amongst of international languages that highly connect the world. Sisi tumekomaa na kiswahili, lugha ambayo bado haijatoboa kimataifa even at regional level. So ni ngumu sana kujichanganya kwenye international avenues za kutafuta maisha. Mfano tu, jaribu kupitia international forums kwenye social media, wabongo hawasogezi pua huko, utawakuta wachache sana.

Mfano mwingine, mtu ni Masters holder lakini spoken English ni zero! Hawezi kutema 'yai'. Mtu huyu anaogopa na hawezi kuapply kazi at International entities like NGOs, UN Agencies, etc. Human personnel from East africa to UN Agencies... Kenya na Uganda make the majority. Intl languages competence bado ni shida kubwa kwa watanzania.

-Poor education. Wabongo wengi tunaenda class kukaririshwa vitu, na sio kueleweshwa materials. Hivyo inakuwa ngumu sana kupenya abroad under 'professional job' umbrella.

Kuna mtu namfahamu kabisa personally ... kahitimu Bachelor Degree mwaka jana. Cha kushangaza sasa... hajuwi jinsi ya kufungua/kuandika email na kuweka attachment. Hawezi kabisa! So mtanzania kama huyu, anaweza ku-compete kwenye international professional jobs/opportunities?

Nadhani hizo ni miongoni mwa factors zinazosababisha wabongo tusiwe courageous wala aggressive kufukuzia international money.

Wacha tuendelee kulima mchicha ili kupata hela ya dona na rent ya chumba uswazini. Ila ukipata viza, then pasua anga. Bongo hakuna mwanga. Waya mkali mbuzi analamba reli.

Baby don't cry, keep ya head up until the end of time. Life goz'on.

-Kaveli-
Thank you Kaveli lakini JF imesaidia sana kututoa point moja kwenda nyingine,na hizi mambo unazozimwaga hapa watu tunafunguka
 
Boss fanya yafuatayo; andika tena ukitumia l na r kwa ufasaha na tuelewe wapi ni mwanzo na mwisho wa sentensi. Mental slavery ni kuamini kuwa huko kwa wazungu ndio kutakapompatia mtu mafanikio ilihali resources/malighafi kule ziko limited wao wanawaza kila uchao namna wanavyoweza kurudi huku kuexploit zaidi. Tanzania ni moja ya resource rich country -- sijui hata kama unanielewa

Pinda awataka watanzania kuwekeza nje ya nchi

eb soma hapo unaweza pata kitu...
 
Boss fanya yafuatayo; andika tena ukitumia l na r kwa ufasaha na tuelewe wapi ni mwanzo na mwisho wa sentensi. Mental slavery ni kuamini kuwa huko kwa wazungu ndio kutakapompatia mtu mafanikio ilihali resources/malighafi kule ziko limited wao wanawaza kila uchao namna wanavyoweza kurudi huku kuexploit zaidi. Tanzania ni moja ya resource rich country -- sijui hata kama unanielewa

:: Balozi Wa Tanzania Nchini Burundi Amewataka Watanzania Kuwekeza Nchini Burundi
pita na hapa watu wapo nje lakini wanakumbuka kwao... sijui unaokota nini humo katika hizo zaga....
 
Mkuu naomba uiongelee kidogo hii mitihani. Huwa inanikata stimu sana napotafuta Scholarship.
Hizi exams naona inategemea na chuo
Mimi nimeapply scholarship vizuri wakawa wanataka hiyo mitihani nikawa tumia barua ya UDSM,wakagoma.
Ikabidi niwaulize nifanyeje wakasema nitafute agent wa chuo chao hapa TZ,nika search hakuna agent, ni karudi kuwaambia hakuna agent wao tz
Wakasema watanitumia online English test ya lisaa na nusu,kweli walituma nikafanya hiyo test nika submit,wakarudisha majibu mana test walinitumia wengine kabisaa so matokea wakayapeleka chuo nilichoomba,hicho chuo wamenitumia admission form nizijaze zikiwa zinahitaji referee na mwajili aseme kitu kuhusu mimi
Fomu ya mwajiri nimejaza mwenyewe nampelekea J3 assign,kuna fomu ya kujieleza kuhusiana na kozi unayoomba that's all.
Kwahyo tusikate tamaa tuendelee kujaribu kuomba na kuomba siku moja Mungu atasikia.
 
That's correct. Wabongo tunazibiana sisi kwa sisi... waliotusua hawataki kuwavuta waliopo down.

Unakuta mtu amenyaka dili fulani, hawezi kuwastua wengine hata kama yeye hana capacity nayo. Hii ngozi nyeusi hii ni shida sana. Roho mbaya, ushirikina, kuangushana ile ya 'tukose wote', majungu, n.k.

Ndugu nao ni helpless tu. Waweza pata majanga afu ndugu akaibuka week ya pili. Unapata great support kutoka kwa mtu baki ambaye hata hukutegemea.

Ndugu wa damu kabisa yupo vizuri sana kiuchumi, unamuomba akukopeshe laki tatu tu ili ujiajiri kwenye Ujasiriamali, anakuambia hana. Ila kila ukienda kumlilia shida hela ya kula, anakupa na nauli juu. Miafrika tuna ubagamoyo wa ajabu sana mkuu. Ni wachache sana wenye mioyo safi.

The black continent. Penye giza... nuru haiji kwa koroboi.

-Kaveli-
Mkuu heshima kwako... Umemaliza kitu kuhusu wabongo.

Binafsi mimi hizi roho nyeusi za wabongo ni moja wapo ya sababu kuu ni kwanini naona Tanzania sio mahala pazuri pakuendelea kuishi.
 
Hizi exams naona inategemea na chuo
Mimi nimeapply scholarship vizuri wakawa wanataka hiyo mitihani nikawa tumia barua ya UDSM,wakagoma.
Ikabidi niwaulize nifanyeje wakasema nitafute agent wa chuo chao hapa TZ,nika search hakuna agent, ni karudi kuwaambia hakuna agent wao tz
Wakasema watanitumia online English test ya lisaa na nusu,kweli walituma nikafanya hiyo test nika submit,wakarudisha majibu mana test walinitumia wengine kabisaa so matokea wakayapeleka chuo nilichoomba,hicho chuo wamenitumia admission form nizijaze zikiwa zinahitaji referee na mwajili aseme kitu kuhusu mimi
Fomu ya mwajiri nimejaza mwenyewe nampelekea J3 assign,kuna fomu ya kujieleza kuhusiana na kozi unayoomba that's all.
Kwahyo tusikate tamaa tuendelee kujaribu kuomba na kuomba siku moja Mungu atasikia.
Mkuu labda chuo gani Hicho
 
Naomba Link hiyo na Mimi niombe
 
Back
Top Bottom