Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza


Hiyo ni sababu namba moja.
 
Mkuu nakuja inbox unipe indetaila how to reach malta. Serious.
 
Mkuu ni kweli... Uhamiaji hawatoi passport bila reason.... Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
Nakumbuka wakati nafuatilia passport kuna afisa mmoja akaniuliza kwa dharau kwamba unataka passport ya nini!? Na unataka kwenda nchi gani!? Nikamjibu naenda kuolewa na bibi mmoja pamoja na biashara, wote ofisini wakaagua kicheko. Tanzania kuna baadhi wanafikiri kupata passport hadi wazazi wako ni mawaziri.
 
Nmepata mchongo wa kwenda japan na mwenyeji wangu kaniambia fursa za kazi kibao na nkifika natafutiwa mwanamke tunafunga ndoa napata kikaratas maisha mengine yataendela. Kwa mwenye uzoefu na inchi hiyo ningependa kujua mengi
Asia ni nchi tatu tu za kwenda Japan , Malaysia, Singapore ila huku ukiwa ni mtu wa IT utafanikiwa sana na South Korea
 
hii ni shule mkuu, big up.
 
Kwl mkuu...miaka hiyo ya 90 ilikuwa Tanzanian passport holder unaringa UK na SCANDINAVIA. countries free entry.
Baada ya wasomali ,, Nigerians na wahindi kuanza kununuwa passport za Tanzania tukapigwa pin tusiingie inchi hizo bila kuwa na viza,
....kibaya zaidi Nigerians walikuwa wanabebea madawa ya kulevya kupitia passport zetu,
.wahindi na wasomali walitumia sana kuingia inchi hizo kama REFUGE,
Airport wakiulizwa .wanasema mimi ni msomali au muhindi. nimenunuwa passport Tanzania... Natafuta ukimbuzi.
 
Hahahaha umenichekesha hapo kwa kibibi...

Mkuu ingependeza ukitueleza mchakato mzima wa safari yako na ulipo leo....
 
Kibaya Zaidi wakati ule wengi tulilewa maji ya ujamaa, si wengi walipenda kutoka nje. Ninakumbuka zile nyimbo za shule "Kambona ameolewa ah aha huko ulaya". Kila mtu alijivunia kuishi nyumbani. Wasomi wengi wakati ule walirudi nyumbani na gari, fridge, na jiko vya kuanzia maisha. Ukirudi tu unakabidhiwa nyumba za serikali aither ni flats za Upanga au zile za Bagamoyo Rd karibu na St Peters.
 
Hahahahah umenichekesha sana na nimekumbuka mbali....

Enzi hizo hata passport walimiliki hao wasomi waloenda na kurudi.... Leo maelfu wanamiliki hadi vijana wakitaa... Wakiweka visa free bongo itahamia London!!
 
Lazima uulizwe MKUU.. Kwani hujuwi kama kunafika kipindi materials ya passport.. Mfano vitabu.. vinakuwa vimekwisha?mnapaswa msubiri hata mwezi mzima material Yaje..sasa kwnn vitabu vipotee bure kwa sababu ya watu ambao hawasafiri?inchi nyingi za DUNIANI.. Au mfano hyo south tu..MTU anazaliwa hadi anakufa hajawahi kushika passport... ID tu inatosha...huwezi kuchukuwa passport unaiweka tu CHINI YA KITANDA..huku wenzio mialiko ya ULAYA INA expire . .lazima uwe na sababu za msingi. Na ukidhi vigezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…