Lusungo, Ahsante kwa uzi huu na kwa uzalendo huu.
Kwa wale ambao wanauzoefu wa migodi ya Tanzania please msing'ang'anie humo Geita, Kahama, buly... tafuteni kutoka kwenda nje ya mipaka ya Tanzania kama expat tuiletee nchi fedha za kigeni. Watanzania wanaheshima kubwa Congo DR, Zambia, Senegal, Ivory Coast, Mali, Ghana, Ethiopia, .........
Nimezunguka migodi ya nchi hizi nyingi nimekutana na watanzania wengi na wanafanya kazi nzuri na wanalipwa vizuri kwa average ya USD7000 kwa mwezi ambayo ni sawa na 15M ya Tanzania.
Tukiwa na Watanzania 100 wanaliingizia pato Taifa ya USD700,000 kwa mwezi pesa za kigeni
Tukiwa na Watanania 1000 wataingiza USD 7,000,000.
Tukiwa na Watanzania 10,000 wataingiza USD 70M which is possible for now tuache woga
Kuna mtu nilimuita kuna nafasi ya kazi nilipokuwa mgodi mmoja wa Lumwana kule Zambia wakati ule yeye alikuwa anafanya kazi pale TBS akaniambia hawezi kuiacha familia wakati ule dili za mikutano zilikuwa ziko chart mala leo wako movenpick, kesho Kunduchi beach full usanii lakini nilimwambia usitumainie kazi za dili hakunisikia leo hii yuko chali.
Tulenge kufikisha maexpat 100,000 ambao wataletea Taifa fedha za kigeni 700M USD kwa mwezi ambayo ni sawa na 1.5Tillion Tanzanian shs. sidhani kama kuna zao lolote tunao export lenye kuleta hizi pesa kwa mwezi. If we have failed to export products let us export human skills/resources please. mpaka sasa nimeweza kuwaconnect watu 12 kufanya kazi hizi na wengine mpaka sasa wananizidi hata mshahara but I am proud of this, I want Tanzanian to flood Africa as expats in the mining industry, doctors, IT and accounting. Tusibaki kupigana vikumbo Vodacom, TIGO, Airtel, TRA, Bandarini, huko dili hakuna na zilikuwa siyo halali tutachukia watawala bure. Stand up and get out there.
Huku unafanya kazi week 6 site na week 2 uko home unaendeleza miradi yako na ukiwa site hutumii hata shilingi yako vitu vyote unakuwaprovided mshahara unaukuta nyumbani Tanzania kwenye A/C unakusubiri (very clean money, hakuna kutega dili).
Mimi nilipata kazi kwa ku-apply online application kwa mara ya kwanza AngloGold Ashanti na kutokana na uzoefu niliokuwa nimepata hapo TZ wakanikubali and now I am changing from one company to another, country to country within Africa, sitaki kwenda ulaya au America, huko nitakuwa mtumwa. I like my Africa.
Google makampuni then apply na usiamini au usisubiri kutafutiwa apply ukiamini utapata ila ikitokea amejitokeza mdau kukusaidia it is very fine.
Thanks.