Hahahaa mkuu, leo hii hadi sie vijana wa kitaa tunakula vumbi la Mbagala na passport tumezika uvunguni geto mpaka tunaisahau!
Mvua za mwaka juzi... natoka misele narejea geto uswazi... ile kufungua goli tu, nikatahamaki na kujisemea: "khaaa kumbe nina passport, sa nangoja nini kwenye Bara hili la giza?". Geto limejaa maji mpaka level ya kitanda, gamba la kijani linaelea tu kwenye maji. Siku hiyo nilishinda kutwa nzima nadeki geto na kuanika nyaraka. Uswazini heka heka!
Kweli nawadeiz mpaka masela wa kitaa wanaholdi passport. Kupata channel ya kupaa ndo mbinde kichizi, hasa kwa vijana tunaotokea familia za 'unga robo usicheze mbali'. Otherwise uwe 'msafiri kafiri with nothing to lose' then unajilipua mbele kwa mbele.
-Kaveli-