Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Na kumbuku karibia Scandinavia yote ubalozi ni mmoja hapo bongo
 
Kweli kabisa man, tena hapo kwa wakenya kumefunika vya kwetu vingi sana... Yaani sasa hivi ukienda nje ya bara la afrika ukiongea kiswahili unauluzwa kama wewe ni mkenya. It seems that chochote kizuri kilichopo afrika mashariki basi inatambulika kinatoka kenya uko duniani
Hata nilivykua Dubai nilikua najitambulisha kama mkenya, maana kule wakenya wanawafahamu sijui walikua wanawauzia chai/kahawa Dubai miaka hiyo, so at least wanaelewa ila wengi ukiwatajia Tanzania hawaelewi
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.

haki ya MAMA naapa usije ukategema TZ hii upate vyeo vya juu, angalia Tu utaona, hii nchi ina LAANA, na kinachoifanya ibaki na AMANI ni WALOKOLE wanaolia mchana na usiku makanisani mwao, maana kipindi cha ibrahimu wangekuepo watakatifu 2 tu nchi isingechomwa, sasa hawa wote waende wapi
 
Sio kweli mpk ufuate utaratibu wao,na mtu ukipata residence hapa sweden huwezi kutamani kuhamia Denmark maana upatikanaji wa kazi Kati ya Denmark na sweden hapa ni easy mkuu
Ninawajua wemgi tu waloanzia Sweden baada ya kupata kibali wakahamia DK....
 
Hata nilivykua Dubai nilikua najitambulisha kama mkenya, maana kule wakenya wanawafahamu sijui walikua wanawauzia chai/kahawa Dubai miaka hiyo, so at least wanaelewa ila wengi ukiwatajia Tanzania hawaelewi
Ahahahah binamu why hukumpaisha ngosha bhn
 
Hata nilivykua Dubai nilikua najitambulisha kama mkenya, maana kule wakenya wanawafahamu sijui walikua wanawauzia chai/kahawa Dubai miaka hiyo, so at least wanaelewa ila wengi ukiwatajia Tanzania hawaelewi
Aisee kuna jamaa yangu mmoja aliniambia ukiwaambia unatoka na tanzania, na hili wakuelewe basi itabidi uwape lecture haswaa.... Na sijui utatumia reference gani maana mlima kilimanjaro wanafahamu unapatikana kenya.
 
Katika nchi za scandinavia Sweden bado sheria zao za kupata uraia sio ngumu ingawa wameanza na wao kuweka vikwako, ikiwemo kutotoa uraia wa kudumu kama kipindi cha nyuma
Yeah Sweden ndo wamelegeza kidogo ila DK na Norway wamekaza sana!!
 
Aisee kuna jamaa yangu mmoja aliniambia ukiwaambia unatoka na tanzania, na hili wakuelewe basi itabidi uwape lecture haswaa.... Na sijui utatumia reference gani maana mlima kilimanjaro wanafahamu unapatikana kenya.
Wakenya ni wepesi na wako wamoja sana ndio maana identity yso ni rahisi kujulikana....
 
Back
Top Bottom