Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Yaa..pale ni viza free mkuu kwa tanzanian passport holder.. mkuu hapafai..pana njaa hatari...halafu cha ajabu ukifika wanakuita muafrica...wao wanajiona sio waafrica...nimekaa Antananarivo pale...kwnz hawajuwi English wanaongea kimashangaa...au French kwa mbali... Ukifika pale ndy utajuwa Tanzania tumepiga hatua kiasi gani ktk Africa yetu hii...kuanzia chakula chao KIBOVU...hata CHUMVI hawaweki kwny CHAKULA
...hata UGALI hawaujuwi.. Wao ni wali tu..kuna siku tulihangaika kusaka UNGA WA MAHINDI shoprite zote hawajuwi...ila PAPUCHI INJE INJE MKUU..kule ukiwa disco...ukiona mwanamke kavaa viatu virefu means anauza..wewe uliza BEI tu...ndy style yao..kile kisiwa wafaransa kibao wanakuja kula raha tu na kuondoka..tena UFARANSA wanaingia ENTRY TU....ila cha kushangaza MKUU pale MTU akifa...anawekwa KWENYE shelfu ndani ya nyumba ila inajengwa makaburini....kule MTU akizikwa na city ndy anazikwa ardhini..au anaonekana ni MTU LOFA SANA..hana uwezo wa kujenga BANDA LA KUHIFADHI JAMAA ZAKE..kwa hyo wakimuweka maiti kwenye shelfu....then baada ya mwaka wanakuja kufunguwa ile nyumba wanachukuwa maiti wanacheza nayo mziki..tena mziki mkubwa unafunguliwa makaburini.watu wanajaa kushuhudia maiti wanavyocheza nayo mziki.na ndugu wanakuwa na bajeti hiyo ya sherehe hiyo.kila ikifika mwaka.maiti itatolewa wanacheza nayo ngoma na kuibadilisha nguo.HALAFU WANAIRUDISHA TENA KWENYE SHELFU ...wanafunga HOUSE wanaondoka....na wanaamini wasipofanya hivyo maiti itawaletea mikosi....mkuu niliogopa sana siku za mwanzo..pia pale rais wao Fulani alifukuzwa na mawe kqmq mwizi.. na wanainchi...akakimbilia mafichoni south...rais alikuwa na uwanja wake wa ndege mwenyewe na pesa inaingia mfukoni kwake..mkuu hapafai pale...Tanzania yetu ni marekani...nyumba ZAO zipo milimani na mabondeni tu...

Visiwa vingi ambavyo Africa au Europe ambavyo vina watu weusi hata kama hawa a uraia wa nchi za Ulaya uwa wakiona watu wanatoka bara La Africa wanawaita waafrica na wakati rangi moja kasoro Zanzibar tu,visiwa hivyo Kama Madagascar,Comoros,Reunions([emoji632]),Mauritius etc,lakin pia Madagascar inaweza ikawa njia pia ya kuingia visiwa vya Reunions na ukaanza maisha hapo au ukajiongeza kWa kuingia Europe kupitia France maana hicho kisiwa ni cha kifaransa,wananchi pia ni wafaransa,wanapiga kura Kama watu wanaoishi France(wenye uraia).
 
Hivi hii kujilipua ni kwa wote!? Mie nilidhani kujilipua kunawahusu wale ambao waliingia nchi za majuu kama Watanzania kisha wakasema wao ni wasomali, warundi, wasudan etc na kuchana au kuchoma moto passports zao.

Ila wale ambao waliomba makaratasi kama Watanzania na majina yao ya waliyotoka nayo bongo na vyeti vya elimu kuanzia bongo hadi majuu hawa nilidhani hawamo kwenye kundi la waliojilipua. Hebu nifahamisheni waungwana.

Ni muhimu sana hii kwa wenye roho nzuri kama wewe wafunguke maana wapo watu wengi wana ndoto zaa lakini wanashindwa waanzie wapi
 
Mkuu Richard asante kwa kuja...

Ni kweli UK na USA ni kugumu ila ni kwa baadhi ya maeneo...

Lakini nchi nzuri zaidi ni za Nordic pamoja na Germany... Ujerumani tangu ianze kupokea wakimbizi raia wake wamebadilika sana juu ya ubaguzi.... Siku hizi wako poa tofauti na zamani...

Ila nashauri zaidi watu waende Nordic

Karibu mkuu kwa mawazo
Ujermani pako Poa mkuu, na huduma za kijamii wapo vizur.... ukishapata Residence permit selikali inakulipia asilimia flan kwaajir ya kusoma Lugha , nauli, na pesa ya makazi. Pia wanazo ofisi zibaitwa Job-center ni kwaajili ya kuwatadutia wageni kazi... Pia kazi zisizo rasmi ni nyingi kama kusambaza magazet, upishi migahawani, usafi nk. Na unapata pesa nzuri tu mwisho wa siku... ubaguzi umebaki kwa wachache sana.. na kumbuka hali ya Usalama ni kubwa sana... wenzetu walishtuka kitambo mfano Hamburg na Berlin hadi kuna makanisa ya Waghana... ebu tuamkeni na tujiamini tusiogope simulizi za uongo na kukatishana tamaa....
 
Waungwana msisahau pia kuchungulia hii link hapa chini. Fuateni maelekezo kwa makini na kuangalia tarehe husika. Kwa kuwa gharama za kutuma maombi si kubwa jitahidi kutuma maombi mengi kadri muwezavyo ili kuongeza probability ya kuchaguliwa. Kila la heri na baraka katika maombi yenye.

Electronic Diversity Visa Lottery
Asante mkuu na sisi tujaribu bahati zetu.
 
Mkuu MziziMkavu alikua akifanya ishu za kuwapeleka watu ulaya kwa malipo fulani... Unafika huko wanafanya arrangement ya mwaliko mpaka residence permit....

Wasiliana nae kama bado wanafanya hizo mambo....
Na mimi nataka jamani, unawasiliana vipi na Mzizi Mkavu?aweke mawasiliano achangamkie Fursa watu tujilipue.
Unafanya kazi tembo mshahara sisimizi una kazi ya kuwaza mpaka unazeeka kwa mawazo, aaaghh!!
 
Kabisa mkuu... Tunataka tuanzishe hii movement... Haiwezekani kila uendapo ni wakenya na wanaija tuuu.... Ndo tumeanza hopeful tutafika mbalj...
Movement ni nzuri ina implementiwa vipi ndo tatizo
Au mnaanzaje ili kweli watu walio na nia za dhati kwenye nyanja za kusoma,kufanya kazi nk wakapata connection through Tanzanians walio nje ya Tanzania?
Tuache ubinafsi na tuwe tayari kusaidiana hapo ndo tutaweza kuona Watanzania wamezaa all over the world.
 
Mkuu lusungo hongera uzi mzuri, una manufaa sana pia.

Hii kitu ya kuhangaishwa na passport imenishtua, it's not right kuhangaishwa Mtanzania halisi. Ni vizuri kuwa careful since the right to have a passport as a Tanzanian was abused before, lakini they can tell, inapokuja suala la kugundua mzawa na asie mzawa. Kila mtanzania ana ya haki kuwa na passport ya Tanzania bila kunyanyaswa.
Mimi niliomba scholarship sasa kimbembe passport kuanzia ofisi unayofanyia kazi ukimwambia HR niandikie barua ya kupata passport mtu anahisi unaenda Ulaya kesho
Ukienda ofisi za Uhamiaji nako mbinde ila thanks Lord nilimpata rafiki akanielekeza km unataka kuipata haraka passport.
Nimeipata tena passport kubwa ya miaka kumi kilichobaki ni ku apply scholarship mpaka usiku wa manane Halmashauri kumenichosha mwenzenu.
 
Mbinu nyepesi sana ya kufanikisha ndoto zenu coz naona wengi mnatamani kuja au kwenda Ulaya na US lakini njia mnayotumia ni ndefu ikiwamo ya ndoa za usanii siku hz wanafatilia sana na njia hii siku hz ni ngumu kwa sasa hv kwani siasa za sasa ni siasa za utengano na kufunga mipaka dhidi ya wageni
Ok njia ya kwanza ni kuingia nchi ya Malta ,Malta ndio nchi inayomkaribisha mgeni yeyote na yenye sheria nyepesi sana za uhamiaji kwa wananchi wanaotoka nchi za Commonwealth ( British colonisation)
So ukishafika Malta ukiweza kukaa ndani ya Malta ndani ya mwaka mmoja bila ya kufanya jinai huna haki ya kuomba uraia so kama utakuwa umekwenda kusoma , kufanya kazi, kutembea au kwenda kufanya kazi ya kujitolea (kazi za bila ya malipo)
Ukishapata uraia wa Malta unakuwa na uwezo wa kwenda kufanya kazi nchi yeyote ya Ulaya kwani Malta ni nchi iliyo kwenye jumuhiya ya Ulaya
So kama unabahati unaweza kupata lakini nchi nying za ulaya au nchi za dunia ya kwanza kupata kazi kwa elimu uliyosomea Africa ni ngumu sana mpaka usome kwao ndio wanakuamini
Owk kama utakuwa uko vizuri kiafya unaweza kwenda Jeshini ,nchi nyingi za ulaya zinachukua raia wa nchi za ulaya kama wanajeshi au kama umetoka nje ya jumuhiya ya ulaya ni lazima upate parmanent resident kitu ambacho ni kigumu sana kukipata kwa nyinyi mnaokuja huku kiujanja janja
Nchi zinazochukua raia wa nchi nyingine kwenye majeshi yao nitakuja na list yao muda si mrefu
lakini ni nchi ambazo zipo kwenye kundi la A list duniani zikiwamo nchi zote za Scandinavian
Ushaingia jeshini ,majeshi mengi ya Ulaya wanapaga watu ambao si raia wa nchi hyo mkataba miaka mitano mitano ndani ya hyo miaka mitano unaruhusiwa kusoma chochote utakachopenda gharama ni za jeshi so utachagua cha kusoma kama umetoka bongo na ka degree chako utasoma masters kama umetoka manyoya utatafuta cha kusoma ndani ya miaka mitano ni mingi sana na unapata faida mbili moja kulipwa mshahara ,huduma za Afya na uhakika wa kupata uraia kama utaitaji
So ukimaliza miaka mitano tu usiongeze tena mkataba ongeza tena kama umeipenda kazi ya jeshi so kama umeona ni manyoya unaiacha so unalipwa mafao yako na unakwenda kuomba uraia na unapata hata bila ya kufanya mtihani wa kuomba uraia na hii kuna nchi hawataki uraia pacha kama Germany au Norway so kama nchi hawataki uraia pacha basi unachagua mmoja ukishamaliza kupata uraia wa nchi hyo uliyoichagua ww from there unatafuta kazi kwa vyeti ulivyosomea jeshini na tena wakijua ulikuwa mwanajeshi wanakuheshimu sana kwani unaonekana umejitoa kwa nchi so unapata kazi na maisha yanaendelea ndani ya miaka 6 tu mission inakuwa imekwisha ukipita Airport ukionyesha gamba la mzungu unapita tu hupekuliwi pekuliwi kama mwenye passport ya Bongo
Kuna website ambazo watu kutoka sehemu zote za dunia wanatafuta watu wa kuja kumfanyia kazi ya kujitolea ambapo yeye atakupa chakula na sehemu ya kukaa bure kipindi chote utakachokuwa pale kwake mwaka mmoja tu ndani ya Malta bhasi
Lakini leo kunambia sijui mnapanga kuondoka kwenda nchi ambayo huna mwenyeji naona mnacheza nyinyi na mnadanganyana Ulaya na US ya sasa si kama ya zamani utaishia jela au kufa tena na balozi zenu zilivyo ngumu kwa raia wake utakoma na kujuta kuja tena mkuu wenu amesema muachwe njia nyepesi kabsa ndani ya miaka 6 tu umefanikisha mwaka mmoja Malta miaka 5 jeshini mwaka wa sita unapassport ya mzungu
Na hii ni kwa wanawake na wanaume sehemu pekee ni kufika Malta tu mwaka mmoja tatizo nililogundua Waafrica wengi akili yetu tunawaza ulaya tena zile nchi tajiri tu lakini mmeshindwa kujua dunia nzima wanawaza hvyo hvyo njia hii ya malta bado wengi awajaijua then tafuta mtu wa malta kafanye kazi ya kujitolea kwa mwaka mmoja kwanza unapata pa kukaa kula na mwenyeji lakini kwenda sehemu kwa mipango mipango mtakuwa mnadanganyana tu wanawake hasa wa Tanganyika wamekuwa wanaogapa sana kuchukua maamuzi ya kuondoka lakini nataka kuwambia tena wanawake ndio njia nyepesi sana kwani wazungu wanawaheshimu sana wanawake cha kwanza kwa heshima kwa wazungu
1 Wanawake
2 Mbwa au wanyama
3 Mwanaume
So kwa dada zangu kwa njia hii ya Jeshi ni bora sana kwao tena sana naongea hv kwa kujua ninachosem

Ningependa kuwambia ndugu zangu Watanganyika kwamba dunia ya sasa maendeleo yamehama kutoka kwenye nchi zinazoongea kingereza na kuhamia kwenye nchi ambazo haziongei kingereza kwani dunia nzima robo tatu wanajifunza au wanajua kingereza na target yao ni kwenda kukaa nchi zinazoogea kingereza sasa utakuta nchi zinazoongea kingereza zimeshajaa wahamiaji kibao lakini niwape siri kubwa kuwa nchi zisizo ongea kingereza zinaitaji sana watu kwani watu wamekuwa wakienda kwenye nchi zinazoongea kingereza

MALCOM LUMUMBA
Mkuu nipe hizo link za website?
 
Mimi niliomba scholarship sasa kimbembe passport kuanzia ofisi unayofanyia kazi ukimwambia HR niandikie barua ya kupata passport mtu anahisi unaenda Ulaya kesho
Ukienda ofisi za Uhamiaji nako mbinde ila thanks Lord nilimpata rafiki akanielekeza km unataka kuipata haraka passport.
Nimeipata t ena passport kubwa ya miaka kumi kilichobaki ni ku apply scholarship mpaka usiku wa manane Halmashauri kumenichosha mwenzenu.


Usikate tamaa mkuu. Inashangaza sana kusikia hivi, wenyewe kwa wenyewe tunavyoumizana. Sasa HR kukuandikia barua au Immigration kufanya kazi yao inavyotakiwa upate passport wanaona kama 'wanakusaidia'
Wakati wote hao hizo ni kazi zao, na wewe ni haki yako.
 
Usikate tamaa mkuu. Inashangaza sana kusikia hivi, wenyewe kwa wenyewe tunavyoumizana. Sasa HR kukuandikia barua au Immigration kufanya kazi yao inavyotakiwa upate passport wanaona kama 'wanakusaidia'
Wakati wote hao hizo ni kazi zao, na wewe ni haki yako.
Ujanja ujanja na roho mbaya tu ili wapate pa kula.
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
Pole sana ndugu, vumilia tu tuijenge nchi wote.
 
Europe kumekua kugumu sana kuingia siku hizi, ninaona wadada wengi wanaopata mwaliko wa miezi sita wanaingia online dating wakifika nchi hiyo kwani ni rahisi kukutana na mhusika wakati ukiwa pale, wakishaonana dinner mbili tatu anamweleza kuwa amekuja for visiting na inabidi arudi bongo. Kama date amekolea basi atamfuata bongo na mambo yanaendelea kutoka pale.
Ndio maana mvua zimekua za maombi siku hizi,yani mabinti wanasafiri kufuata "boloyang" kwa wazungu?alohhh!!
 
Back
Top Bottom