Mkuu,
Wakati nasoma sekondari nilikutana na jamaa mmoja Mswidi, alikuwa akifundisha IST (mimi sikusoma shule hiyo). Siku moja alikuja shuleni kwetu (akiwa katika matembezi ya kawaida na alipenda sana kupiga picha) mimi nikampokea (nilikuwa mwenyekiti wa mwanzilishi wa English club shuleni). Baada ya kumaliza ziara yake, urafiki wetu uliendelea. Uzoefu wangu ulianzia kwake. Hakuishi Tanzania kwa muda mrefu na aliporudi kwao, aliwaelekeza wageni wengi (waliotaka "reference") kwangu na niliwapokea na kuishi nao kwanza ilikuwa nyumbani kwetu na baadae kwangu kwa kipindi kirefu. Wakati fulani nikasafiri na nikapoteza mawasiliano mengi (wajanja waliingilia email yangu) na zoezi lile sikuilifanya tena. Hicho kilikuwa ni kipindi "internet cafe" ipo chuo kikuu UDSM na ilikuw unalipa Tzs. 3000 nusu saa na Kariakoo, Mussa telecommunication unalipa Tzs. 4000/- nusu saa, simu tunapiga kwenye vibanda dk.1 Tzs. 500/-
Kaka ...