Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Dah wadau naona thread imepoa au watu mmeshasafiri nini????????????

I have good newz for you nimewasiliana na zile taasisi nilizo sema kwenye project number 2

So mwezi wa 5 Tanganyika mnaweza pata ugeni wa vijana wa 5 kutoka nchi pendwa ya Malta wa tatu wadada na wawili ni wakaka sasa kuhusu kuhost natafuta mtu mwaminifu wa kumuunganisha nao wakija yeye ndio awapokee na kuwatafutia host kama itawezekana
Dah. hao nahisi nitawakosa ila watakaofata itabidi niwepo katika list. Nitakuwa Tz mwez wa 6 . Nakuja kupumzika kidogo then nabadilisha upepo maana SA kwa sasa hakuna issue tena
 
nchi inayokumbwa na upungufu wa chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa... nchi huduma za kijamii si zakulizisha... nchi ambayo mambo mengi hayaendi kama wananchi wanavyotalajia ndo maana hata wewe una sapoti watu waende kusoma watu waende kama wana utaalam hivyo ni hila na hasira zako kwa watu kuona wanaondoka kutimiza ndoto zao kwa kuajialiwa au kujiajiri huko waendapo ambapo wataweza kusave kiasi na kukileta kwao kitaweza kumpa uwezo wa kumiliki greenhous ambayo sasa ni ngumu kwa kijana kumiliki kutokana na gharama kuwa kubwa... wanakaa nyumbani wakiwa wamekata tamaa ya kukosa ajira kukosa mikopo ya kuendeleza au kufikia sehemu ya ndoto zao... njoo na vitu vya kueleweka nyinyi ndio mnataka watu wajiajiri bila ya mitaji alafu hapo hapo kodi ni kubwa rushwa pia mahitaji ya nyumbani (kwa wategemezi)... ni bora mtu kufanya anachoweza kufanya kiliko kushikiliwa akili mental slave ni kitu kibaya watu au mtu ili kuweza kufanikiwa ni lazima afanye kile anachoweza kukifanya kuliko kumpush kufanya hasichoweza hivyo hacha watanganyika wafanye wanachowezafanya bila kuvunja sheria za nchi mkuuu...! mwisho kabisa nibora ukaja na page yako ya kuhamasisha na kuwaonyesha watanganyika njia wanazoweza kupitia ili wafanikiwe hapa hapa maana hii page haiendani na mawazo yako mkuu... ni sawa na yule aliyekuja na post ya bit coin... katika page ambayo si sahihi na wazo lake...
Jiulize kitu, hapo unapoishi unaweza kulima tuta ukapanda mchicha ukatengeneza hela yako ya kwanza. Na fursa ipo zaidi ukihitaji kutanua hii biashara (huu ni mfano tu). Sasa wewe nenda nje uone kama utaweza kuwa na hilo tuta tu la mchicha!!

Acheni kudanganyana, nenda nje kusoma rudi bongo fursa zimejaa tele hapa. Otherwise kama una utaalamu wako nenda nje ukaajiriwe, kumbuka technologia imesogea zaidi kule hivyo waajiriwa ni wachache. Ukitaka kabebe box, ila kumbuka muda utakaotumia kijana mwenzio anaweza kuongeza biashara yake ya mboga mboga hapa hapa akiisimamia vizuri by the time unarudi huna hata pa kuanzia, mwenzio anakunyoosha tu na greenhouses zake!!
 
njoo kigoma kuna kambi zawakimbizi kama tatu na milango iko wazi yani wanasajili wakimbizi wapya kila uchao maswali ni kwa lugha unayoijua ww hasa kiswahili kirundi au kibembe unaulizwa umetokea wapi unataja inchi mojawapo yenye migogoro hasa drc yani ni simple
upo kigoma mkuu...
 
Yeah mkuu kuna matumizi but huwezi linganisha na bongo... Kikubwa kujipanga na kujua nini unafanya... Mfano kazi nyingi za kijungujiko kule US zinaweza kukufanya u save mpaka $2000 after bills.... Na hii ni kwa miaka hii... Nakumbuka nyakati zile ulikua na uwezo wa kusave zaidi coz kulikua na favor nyingi tofauti na sasa!

Ila kwa wataobahatika kwenda Scandinavian countries kule maisha ndiyo simple sana na kutoboa ni rahisi zaidi shauri ya ubure ktk huduma nyingi tu....
Dah we ungekua ndugu yng ningefurahi SNA mana nina kaka marekani na uingereza wako wanaweka ngumu kwenda taifa lolote ulaya nimesoma diploma ya engineering ishu ya IT miaka 3 unataka degree nikasome nnje mana ajira kwetu ngumu na kurudi degree bongo alafu ukose kaz ntakua chizi mana umri unaenda bora nnje ntarudi na mtaji na kujiajili ma bro zangu wanataka nibaki bongo nisome mlimani 4 years duh nataman niombe ukaka kwako
 
Kabisa mkuu... Kitu kingine wivu... Wabongo siku zote tunatamani wengine waanguke tukiamini ndo tutainuka!!

Wengi hatupendi mafanikio ya ndugu hata tuliozaliwa nao...


That's correct. Wabongo tunazibiana sisi kwa sisi... waliotusua hawataki kuwavuta waliopo down.

Unakuta mtu amenyaka dili fulani, hawezi kuwastua wengine hata kama yeye hana capacity nayo. Hii ngozi nyeusi hii ni shida sana. Roho mbaya, ushirikina, kuangushana ile ya 'tukose wote', majungu, n.k.

Ndugu nao ni helpless tu. Waweza pata majanga afu ndugu akaibuka week ya pili. Unapata great support kutoka kwa mtu baki ambaye hata hukutegemea.

Ndugu wa damu kabisa yupo vizuri sana kiuchumi, unamuomba akukopeshe laki tatu tu ili ujiajiri kwenye Ujasiriamali, anakuambia hana. Ila kila ukienda kumlilia shida hela ya kula, anakupa na nauli juu. Miafrika tuna ubagamoyo wa ajabu sana mkuu. Ni wachache sana wenye mioyo safi.

The black continent. Penye giza... nuru haiji kwa koroboi.

-Kaveli-
 
Dah we ungekua ndugu yng ningefurahi SNA mana nina kaka marekani na uingereza wako wanaweka ngumu kwenda taifa lolote ulaya nimesoma diploma ya engineering ishu ya IT miaka 3 unataka degree nikasome nnje mana ajira kwetu ngumu na kurudi degree bongo alafu ukose kaz ntakua chizi mana umri unaenda bora nnje ntarudi na mtaji na kujiajili ma bro zangu wanataka nibaki bongo nisome mlimani 4 years duh nataman niombe ukaka kwako
Ndugu zako ni mapoyoyo, kama hesabu inapanda vizuri, na kimalkia unakijua jilipue na GRE na English exams then zama kwenye web mwenyewe. Mi nilipita njia hiyo, nikamaliza nikaendelea kupiga mzigo kwa Obama. Bongo kwa likizo tu.
 
Ndugu wana JF
Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.

Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.

Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.

Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.

Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.

Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.

FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo...

kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.

2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.

CHANGAMOTO
1. changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)

2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu sio zote.

USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.

Jinsi gani utaenda namna ni nyingi.... naorodhesha baadhi hapo chini...
1. kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo...

2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.

3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali,

4. kwenda kwa shughuli za utamaduni

Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake....

Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.

Nawakaribisha nyote. Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele... karibuni tusaidiane tujenge taifa letu... Tuwasaidie vijana wakasake fursa.


f3d3f1c69fe837f26fcfa18a214662ef.jpg


Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Mnatukumbusha kauli za Kamuzu Banda na Mabutu Seseseko, leo hii Malawi ndio imetoa wafanyakazi wa nyumbani wa kiume (foreign male domestic workers) kuliko nchi nyingine Afrika.
DRC ni katika nchi tajiri Afrika hii lakini waangalie Wakongo wengi walipo, zaidi ya wanaume kukata viuno jukwaani, kuimba na kujichubua. Leo Wakongo sio watu wakula mbwa na nyani.

Hii Tanzania yetu, unaweza kutimiza ndoto yako, hata kuanzia mchimba mkaa mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa. Why not? Right here in Tanzania

Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulaya wakati ardhi zetu zina rutuba ya kukutosha na tunaweza kuishi na kuendesha maisha yetu kupitia kilimo?

Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muhanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya Wakoloni.

Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.
 
f3d3f1c69fe837f26fcfa18a214662ef.jpg


Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulani wakati ardhi zetu zinarutuba ya kukutosha?

Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya utumwa. Leo kuna Msaudi, Muemarati au Muomani ana ndoto kama hii na wakati kwao sio tajiri kama Afrika?
Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.
Wewe unaishi Africa ipi....
unazungumzia Nchi ambayo Raisi anajigeuza kuwa mungu anachosema yeye ndio mwisho Tanganyika hii tuna zaidi ya miaka 50 tangu Uhuru hivi unayohabari Mwaka wa Jana wakulima wa Nyanya walivuna nakulisha Ng'ombe...au Mwenzetu ni miongoni mwa wanufaika wa Nchi hii kiasi kwamba hamjui Taabu wanazokutana nazo wadanganyika.....
 
f3d3f1c69fe837f26fcfa18a214662ef.jpg


Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Mnatukumbusha kauli za Kamuzu Banda na Mabutu Seseseko, leo hii Malawi ndio imetoa wafanyakazi wa nyumbani wa kiume (foreign domestic workers) kuliko nchi nyingine Afrika.
DRC ni katika nchi tajiri Afrika hii lakini waangalie Wakongo wengi walipo, zaidi ya wanaume kukata viuno, kuimba na kujichubua. Leo Wakongo sio watu wakula mbwa na nyani.

Hii Tanzania yetu, unaweza kutimiza ndoto yako, hata kuanzia mchimba mkaa mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa. Why not? Right here in Tanzania

Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulaya wakati ardhi zetu zina rutuba ya kukutosha na tunaweza kuishi na kuendesha maisha yetu kupitia kilimo?

Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muhanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya utumwa. Leo kuna Msaudi, Muemarati au Muomani ana ndoto kama hii na wakati kwao sio tajiri kama Afrika?
Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.
Hii nchi ya uzulumishi sana.unatafuta kwa nguvu nyingi unanyang'anywa kirahis.mfano mzuri ishu ya viroba.ni bora nijilipue mambele hamna namna.nikuache bro uendelee kupiga porojo mana inaezekana hata wewe haupo bongo land
 
Unalima tuta unamwagilia mkojo wako mwenyewe au mate? Unaweza kulima malori mangapi ya mchicha na unauza kwenye masoko gani hapa bongo? Huko shambani kuna barabara zakufikisha huo mchicha wako unakotaka kwenda?

Serikali yako imekuwekea mazingira mazuri yakwenda kuuza mchicha russia na nchi nyingine? Hukusikia msimu uliopita nyanya zilioza mashambani na zikawa malisho ya mbuzi na nguruwe?

Hata hao unaowasikia wako ulaya sikwamba bongo hawana vitega uchumi. Wapo wenye majumba wamepangisha, wapo wenye mashamba makubwa wanalima large scale agriculture sio tuta moja la mchicha uanze kutembeza na beseni mitaani. Wapo wengi wamekeza bongo, mitajo wameitoa mbele huko.

Kama ulifoji cheti huwezi kuwazia kusoma mbele, waache vijana wakapige shule mbele wakirudi sawa wakibaki hukohuko sawa tu.
Kama nimekuelewa sana mkuu.
 
b3309625f0343f259e8ec91cf49adea1.jpg


Makomanda wenzangu wa mitandaoni, hili sio suala na mtu binafsi, vilio vya Afrika tunavisikia kuanzia Sudan ya Kusini, Misri, Angola, Ethiopia, Somalia nk.
Kuna wenye hali mbaya kuliko hapa kwetu Tanzania.
Na sio kama hatujui wala hatujaupitia au kuutumia mfumo huu wa njia za panya za kujikomboa kiuchumi.
Lazima tuwe na mawazo tofauti. Kama Gaza sehemu inayojulikana kama jela iliyokuwa wazi, wananchi wanabaguliwa na wanaishi kama wakimbizi kwenye ardhi yao, na bado vijana wameweza kujikomboa kiuchumi hapo hapo, sembuse Tanzania?
Tanzania tokea tupate Uhuru wetu, hatuna rekodi Taifa letu limejikomboa kwenye Umasikini, mapambano bado yanaendelea.
Awamu ya 5 inafanya zoezi la ku cleaning the virus and rebooting the system. Tuwe wavumilivu.
 
Among other factors, nadhani baadhi ni:

- Uoga wa maisha. We are extremely fearful of life. We can't take risk ktk utafutaji, tunasahau kwamba there's nothing risk-free in life struggle.

-Lack of international exposure kwa wazazi wetu. Most of us tumezaliwa na kukulia kwenye families ambazo hazikuwa 'global goers'. As such, na sisi tunaishia in the same circle... mtu anapanda Ngorika all the way from sitimbi to Darisalamu, then hiyo ndo maximum exposure ya ndoto zake... kutia maguu Daresalamu.

-language barrier. Hili liko wazi. Wabongo wengi 'kutema yai' ni shuhuli nzito. English is amongst of international languages that highly connect the world. Sisi tumekomaa na kiswahili, lugha ambayo bado haijatoboa kimataifa even at regional level. So ni ngumu sana kujichanganya kwenye international avenues za kutafuta maisha. Mfano tu, jaribu kupitia international forums kwenye social media, wabongo hawasogezi pua huko, utawakuta wachache sana.

Mfano mwingine, mtu ni Masters holder lakini spoken English ni zero! Hawezi kutema 'yai'. Mtu huyu anaogopa na hawezi kuapply kazi at International entities like NGOs, UN Agencies, etc. Human personnel from East africa to UN Agencies... Kenya na Uganda make the majority. Intl languages competence bado ni shida kubwa kwa watanzania.

-Poor education. Wabongo wengi tunaenda class kukaririshwa vitu, na sio kueleweshwa materials. Hivyo inakuwa ngumu sana kupenya abroad under 'professional job' umbrella.

Kuna mtu namfahamu kabisa personally ... kahitimu Bachelor Degree mwaka jana. Cha kushangaza sasa... hajuwi jinsi ya kufungua/kuandika email na kuweka attachment. Hawezi kabisa! So mtanzania kama huyu, anaweza ku-compete kwenye international professional jobs/opportunities?

Nadhani hizo ni miongoni mwa factors zinazosababisha wabongo tusiwe courageous wala aggressive kufukuzia international money.

Wacha tuendelee kulima mchicha ili kupata hela ya dona na rent ya chumba uswazini. Ila ukipata viza, then pasua anga. Bongo hakuna mwanga. Waya mkali mbuzi analamba reli.

Baby don't cry, keep ya head up until the end of time. Life goz'on.

-Kaveli-
Mkuu umepita mulemule kwenye mstari hakika waso,i wetu walio wengi ni wasomi wa makaratasi na sio wasomi wa vitendo na ndio maana tukija kwenye practical tunafeli.
Leo hii mtu anaitwa kwenye interview anavyojieleza utasikitika kama mtoto wa sekondari maelezo hayanyoki elimu yetu na sisi wenyewe kutojishughulisha ndio matokeo haya yanakuja kuiaibisha nchi yetu.
Nakumbuka kunaprofesa flani alilia ajira ya magu maneno aliyosema yalidhihilisha alikuwa fake profesa yaani uprofesa wa kuhongwa.
 
Back
Top Bottom