Nyuzi kama hizi ni sawa na kuwafundisha Waafrika kuwa Watumwa bila minyororo.
Mnatukumbusha kauli za Kamuzu Banda na Mabutu Seseseko, leo hii Malawi ndio imetoa wafanyakazi wa nyumbani wa kiume (foreign male domestic workers) kuliko nchi nyingine Afrika.
DRC ni katika nchi tajiri Afrika hii lakini waangalie Wakongo wengi walipo, zaidi ya wanaume kukata viuno jukwaani, kuimba na kujichubua. Leo Wakongo sio watu wakula mbwa na nyani.
Hii Tanzania yetu, unaweza kutimiza ndoto yako, hata kuanzia mchimba mkaa mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa. Why not? Right here in Tanzania
Tunawapeleka watu wetu kwenda kuosha vyombo, choo na vinyeshi huko barani Ulaya wakati ardhi zetu zina rutuba ya kukutosha na tunaweza kuishi na kuendesha maisha yetu kupitia kilimo?
Tunayajua hayo yote lakini tunahitaji kizazi ambacho kitakachojilipua hapa hapa barani Afrika, kijitoe muhanga na sadaka kwa ajili ya kizazi kipya yaani tutumie muda wetu wote kufanya mapinduzi ya kiuchumi hapa hapa Afrika kama vile wazee wetu walitumia muda wao wote kutukomboa kwenye minyororo ya Wakoloni.
Wakoloni, waliishi vipi na kufanikisha maisha yao hapa Afrika?
Mapinduzi ya Kiuchumi yanahitajika. Hatuondoki Afrika.