Vizuri kamanda.
Kuna vijana kadhaa ambao mm nawajua. Tulitengeneza kama network flan hivi yakupeana habari ya mambo ya scholarships. Hali ilikuwa nzuri sana, mambo yalienda murwa sana.
Wengi tulipata admission na hatukuwahi kufanya mitihani ya english kwani vyuo tulivyoomba walikuwa na option kama ulifanya undergraduate english ikiwa language of instruction and examination, ukitoa uthibitisho basi wanakupa admission (kwa wale waliopitia ud ukienda adm wanakupa barua yakuthibitisha kuwa english was language of instruction and examination.) ingawaje utaratibu huu hautumiki kwa vyuo vyote.
Baada ya kukamata admission, harakati zakuomba scholarship zilianza na bahati nzuri hatukufanikiwa hata mtu mmoja.
Katika kutafuta ushauri wengine walisema mara nyingi hamkidhi vigezo hasa katika eneo la personal statement na vipengele vingine.