Mkuu [HASHTAG]#Daby[/HASHTAG] mpaka sasa nahisi huyu
mgaka12 ndiyo
britanicca kwa maana hana hoja yenye mashiko juu ya lile alitakalo eti watu wasisaidiwe mi naona hakukuwa na maana yoyote ya kuweka vizuizi bila kutoa sababu zenye kuingia akilini mwetu ili jamaa asitusaidie.
Kitu kingine hii ni nguvu ya watu wengi na wenye malengo dhabiti juu ya hili lipo mbele yetu ili mradi kundi la watu kadhaa lifanikiwe naamini na wengine tutafuaata.
Mkuu
mgaka12 wewe ni binadamu na we pia unamapungufu yako hivyo kwa namna moja ama nyingine upo sahihi.
Watu kama nyinyi kwenye jamii lazima muwepo ili kuleta changamoto kwa watu ili wafeli mipango yao ama muwazidishie speed.
Tangu uzi uanze niliamini tu kuna mtu au watu watakuja kuweka magogo kwenye uzi huu ili mambo wayavuruge lakini naamini hii team iliyopo ni watu wenye misimamo.
Mkuu [HASHTAG]#izzo[/HASHTAG] mpaka kuamua kuja kutoa msaada kwa ndugu zake najua kuna mazingira ambayo anayaandaa kwanza mpaka sasa kama ulikuwa hujui kuna watu wanapigwa michujo wapatikane watu wanaostahili hili swala izzo kashalizungumzia.
Mwisho mkuu naomba utuache tupambane kwa hili lililopo kama ingependeza ungetoa maoni ya kusapoti na siyo ulivyokuja umefura kuweka vingingi.
Kuna wengine tumejifunza vitu vingi na tupo kwenye hatua nzuri ya kwenda kufanikisha hivyo basi tunakuomba sana utuachie hili swala kwa maana umelikutia katikati hujui watu wametumia nguvu gani mpaka kulifikisha hapa.
Ndugu zangu naombeno tuendelee kushikamana mtu mmoja asituangushe lazima tufanikishe.