Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Hahahaha, mkuu kwahali hiyo usingizi hauji usiku unaota upo kwenye pipa mara unataka kutest vyoo unalimwaga kwenye godoro. Unafuraha muda wote yanayoendelea nchini hunahabari nayo.

Epuka kuvuka barabara pekeyako unaweza kugongwa manake kimwili upo tz ila kiakili ushafika New Zealand

MUNGU akuongoze kamanda
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ohoo si unaona hapa tunajifunza hata procedures! Hebu ngoja tuone wengine wanasemaje? Bt nahisi huyo muhitaji hana budi kumuita kwa docus maalum ili huyu dada aitumie kama sbabu ya kuombea ruhusa ya kuishi (visa) huko aendako.
Hapa kunashule hutakiwi kuikosa kabisa, kama kunajambo linakutatiza hujawaza kuuliza mara unakatana na majibu ambayo unajibia maswali yako yote hata ambayo hukuwahi kiwaza.

Hii ndio thread inayounganisha watu waiana zote, rangi zote, makabila yote, dini na wasio na dini. Hii ni nyizi ya wajanja waliopata elimu ya imani na kusaidia watu bure kabisa, kabisa.

Baraka zinazoshuka humu hazijawahi kushuka kwa jambo lolote katika nchi hii ya wenye vinyongo na roho mbaya. Na kila anayejaribu kutia pua kutaka kitiharibia anakula za usso anasepa.

Hongoreni vijana, wazee mliojitolea kuchukua muda wenu. Wanaopata fursa msituangushe, na hakuna kusita ukaanza kujiuliza sijui itakuwaje. Ukiipata shirikisha wenzako humu ili upewe a,b,c zakushika mkononi na kukuongezea ujasiri na umakini.

TWENDE KAZI..........
 
Naanza process za visa wapendwa uwiii its a nightmare to me
kwanza kabisa mshukuru Mungu kwa kukupa uzima na ujasiri, pia mshukuru izzo kwa kuwa na moyo wa upendo na hari ya kusaidia watanzania wenzake. am sure kama izzo angekuwa na moyo mdogo kwa maneno ya kevin nadhani asingeweza kuendelea na sisi hapa jukwaani. tuliza akili kidogo ili uweze kujaza kila kitu kwa ufasaha

ubarikiwe sana izzo ,stunter,daby,lusungo,kirikou,kavel na wengineo tunaowatakia wenzetu mafanikio. wao mbele sisi nyuma.
 
Wale wote mioyo ya husda, chuki na wivu wa watu kufanikiwa wanaanza kuaibika sasa. Uzi ushaanza kuonyesha mafanikio baada ya Mwenzetu Shyshii kufanikiwa.

Na wengine hii iwe insipiration kwenu. Usikate tamaa, pigana na kuwa na tumaini kuwa kama siyo leo wala kesho, amini ipo siku yako pia.

Mungu aendelee kutuwezesha.
Umezungumza kweli Compact. Tunasali kulinda na kuondoa ubaya wote na akili chafu, kwa wote wenye nia ya dhati. Nina amini kila kwenye na mwenye nia, uchafu wote hujitenga.
 
Mwambie akutumie invitation letter, then ukienda Migration fasta wanakupa Passport( kama huna) then unafanya maswala ya visa ubalozini, easy unang'oa,,,, kama nitakuwa nimekosea wakuu watakuja kunicorect
Amesema hata akituma hawatakubali
Alishafanya hivyo ila huwa zina decline, so anatumia ma agent wa huko huko
 
Ndugu wana JF
Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.

Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.

Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.

Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.

Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.

Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.

FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo...

kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.

2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.

CHANGAMOTO
1. changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)

2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu sio zote.

USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.

Jinsi gani utaenda namna ni nyingi.... naorodhesha baadhi hapo chini...
1. kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo...

2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.

3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali,

4. kwenda kwa shughuli za utamaduni

Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake....

Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.

Nawakaribisha nyote. Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele... karibuni tusaidiane tujenge taifa letu... Tuwasaidie vijana wakasake fursa.
nani amewaambia huku nje mnahitajika,Tuliendi bongo mtengeneze nchi yenu ,Watazania bana
 
kwanza kabisa mshukuru Mungu kwa kukupa uzima na ujasiri, pia mshukuru izzo kwa kuwa na moyo wa upendo na hari ya kusaidia watanzania wenzake. am sure kama izzo angekuwa na moyo mdogo kwa maneno ya kevin nadhani asingeweza kuendelea na sisi hapa jukwaani. tuliza akili kidogo ili uweze kujaza kila kitu kwa ufasaha

ubarikiwe sana izzo ,stunter,daby,lusungo,kirikou,kavel na wengineo tunaowatakia wenzetu mafanikio. wao mbele sisi nyuma.
Mkuu Marveljt, imani thabiti kwa jambo fulani. Ndio nguzo ya kufanikisha jambo hilo. Na muhimu zaidi, ni imani kuu kwa MUUMBAJI wetu. Mkuu Izzo angelikuwa na imani haba, Nina uhakika hata wazo la kuandika yote aliyoandika hapa, lingemtoka. Nawashukuru sana Mkuu Lusungo, Richard na wengine wote kwa kuimarisha Uzi huu.

PAMOJA NA KWA IMANI KUU, TUNASHINDA.
 
Hahahaha, mkuu kwahali hiyo usingizi hauji usiku unaota upo kwenye pipa mara unataka kutest vyoo unalimwaga kwenye godoro. Unafuraha muda wote yanayoendelea nchini hunahabari nayo.

Epuka kuvuka barabara pekeyako unaweza kugongwa manake kimwili upo tz ila kiakili ushafika New Zealand

MUNGU akuongoze kamanda
Umenikumbusha siku hiyo ndo naenda kupanda Airbus 380-300 jmn niliotaaa nikawa nawaza itakuaje kupanda dege kubwa hivyo kwa mara ya kwanza ndo zinawikaaaa.... Basi nikawa naota nachelewa ndege [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hongera sana Shyshii kwa kufanikiwa kupata mwajiri nchini New Zealand.

Ni matumaini yangu kwamba utakwenda kufurahia kazi yako mpya na kupata nafasi ya kujifunza kutoka majuu.

Mwanzoni upata changamoto kutoka kwa wazazi na watoto lakini ni hatua za mwanzo za kuzoeana na kujengeana uaminifu.

Kumbuka hiyo ndiyo nafasi ya pekee kwa wewe kuweza kuelekea kupata viza ya kudumu nchini humo, hivyo itumie ipasavyo.

Pia ukumbuke kutafuta chuo usome kozi yoyote ambayo itakupa mwanya na njia pana ya kupata kazi zingine khasa baada ya kupata "permanent residence".

Good luck.
Thanks Richard please endelea kuniombea nifanikiwe
Siendi kufanya u sister duu,najua nilichoacha nyuma,najua natakiwa kuongeza elimu.
 
usife moyo. naimani hiyo umeandikiwa wewe na iko kwa ajili yako. kati ya wote tulioko hapa naimani kuna wengine ambao pia walituma baada ya izzo kuileta hii ishu hapa, lakini wewe umekuwa selected. hivyo kaza moyo dada. tutafika tuko nyuma yako.
Amesema hata akituma hawatakubali
Alishafanya hivyo ila huwa zina decline, so anatumia ma agent wa huko huko
 
Hahahaha, mkuu kwahali hiyo usingizi hauji usiku unaota upo kwenye pipa mara unataka kutest vyoo unalimwaga kwenye godoro. Unafuraha muda wote yanayoendelea nchini hunahabari nayo.

Epuka kuvuka barabara pekeyako unaweza kugongwa manake kimwili upo tz ila kiakili ushafika New Zealand

MUNGU akuongoze kamanda
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom