Nashukuru bwana mgogone kwa kuliweka hili sawa lakini kumbuka ni asilimia kumi tu ndio wana moyo wa kusaidia, Mfano ndugu zetu hawa wakenya ni wakabila wakiwa huko nchini kwao, ila wakifika tanzania ni ndugu moja ndio maana huwezi kupata mkenya anatangatanga mitaani akitafuta kazi wanakumbatiana bila kujali tofauti zao wakiwa kwao.
Sisi tukiwa kijijini ,mashuleni, makazini, Vjiweni, mjini ni wanafiki tu tukifika nje tunaota mapembe hatuongei hata lugha yetu, hata mabalozi wetu wanapata shida kuwajua watanzania waliyoko nchi wanazowakilisha isipokuwa mtu anapopata matatizo ndio utamjua kuwa ni mtanzani. tena tuna dharau usiseme.
Nimejaribu kufanya research nikagundua kuwa tumerithi hiyo tabia mbaya kutoka makundi matatu; kwa waarabu 1700(fitina na uchonganishi) tukaja tukarithi tena mjerumani (roho mbaya) ya mkoloni 1800, tukamaliza za wahindi(mnawajua wahindi walivyo na dharau).
chukulia mfano tatizo linatokea tanzania, wandishi wa habari waliyosoma pamoja program moja, module zilezile ila watakavyoreport ni tofauti kabisa, wengine watalalamika wengine watasifia wenye roho ya korosho hawatareport kabisa.