Ukifatilia wenzetu Kenya na Nigeria wengi wamepeana ujanja na kusaidiana kupitia forums zao tu kama tulivyokuwa au dhumuni ya thread hii na ndio maana mm nakataa sana kutumia neno Tanzania kwa sababu Ukisema Tanzania unakuwa na maana ya Tanganyika na Zanzibar lakini wenzetu wa visiwani wametupita sana kwenye ufahamu wazanzibari wengi sana wamesaidiana sana na ktk Watanzania walio nje wengi ni wazanzibari kuliko Watanganyika
Kila kitu kinaanza kama wazo ambalo anakuwa nalo mmoja then anawashirikisha wenzie then mnachangia mawazo kuboresha wazo ndivyo alivyofanya
lusungo kuanzisha thread hii pili mawazo siku zote yanafatiwa na draft au michoro ndio tukaanza kuchangia kwa maandishi hapa then kinachofata ni utekelezaji wa muunganiko wa mawazo na machapisho na utekelezaji ni lazima watu watoke nyuma ya keyboard na keypad waonane live
Kuhusu kutapeliwa au kuibiwa ni mambo ambayo yanaweza kuchangiwa na kwenda chemba kitu ambacho wengi tulikuwa hatupendi mm nawambia ukweli Tanganyika na Serikali yake wameshindwa nguvu na rasilimali watu wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka kutoka shuleni, Vyuoni na kwenye mafunzo ya mikono au ufundi na hii si Tanganyika tu ilishawai kutokea Nigeria ndio maana wanaigeria wakatafuta njia nyingine ambayo ni kutoka nje kutafuta maisha na ndio maana nenda dunia nzima uwezi kukuta hakuna mnaigeria
Lakini Watanganyika bado tunaleta mzaha ndio maana tunapata muda wa kukashifu na kutukanana na kuvunjana moyo lakini huko tunapokwenda ni pabaya zaidi kuliko tulipotoka na safari ya gorigota imefika na Tanganyika tunaweza kujikuta kwa mara ya kwanza Duniani tunatoa wakimbizi wa ugumu wa maisha wakati ndani ya nchi kuna amani na utulivu
Ndo maana dada yangu pamoja na mimi tusiumie sana tunapotukanwa au kukashifiwa kwani siku na saa yaja pale wana wa Adam .....