Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

sio mbaya mkuu, ila huko botswana wapo very organized, huwezi zamia na kujificha muda mrefu, pia pesa yao inaitwa Pura ina thamani kuliko Rand ya Afrika kusini, la muhimu ningekushauri ingia online tafuta shule ya sekondary au msingi binafsi anza kuomba kazi ukiwa huku huku pia omba hata kupitia wizara ya Elimu ya huko ukiwa huku, wakikukubali hutopata matatizo, na hata kama ukipata shule ya binafsi inamaana shule hiyo ndio itakayokusaidia kupata work permit na documents zingine, nakuhakikishia huko lazima upate mdada mzuri na atakupenda kweli kwa kifupi Botswana wanawake ni wengi saana kuliko wanaume, na pia watu wengi hua wanachelewa kuoa kwahiyo we mbongo ukifika na ukatangaza ndoa mbona faster unapata jiko.

Daah, kuna bia zao za ukweli sana St Luis hazina hang over. kule utakutana na watoto wa herero miguu ya bia......

kila la heri kaka. mi hua naenda enda huko.
[emoji121]
MKUU,

MADINI KAMA HAYA ND'O NAYATAFUTA KUTWA KUCHA HAYA.

NGOJA NIANZE TARATIBU.
 
Mkuu inategemea unataka kwenda inchi gani kujilipua...zipo inchi zipo ulaya lakini utatamani ubaki Africa..sasa wewe nidokeze unataka uende inchi gani?
Mkuu kama upo vizuri komaa hapa hapa bongo,nenda morogoro kanunue shamba kubwa tu then fanya mambo uone lazima utatoboa mkuu.
 
naomba kwa anaejua ishu ya ukimbiz atupe mawili matatu.nataka wengine wajilipue new zealand au australia.kwa aliepo nyarugusu naomba mrejesho tafadhali.process ikoje?yani ramani kamili.kuna wadada walienda huko mwaka jana gafla nawaona arizona wengine new zealand.

Ina wezekana maana waha wengi wamejisajili ili kupata huduma kama wanazopatiwa wakimbizi... kila kitu for free even majiko ya gas wao ni kuishi tu bila kufanya kazi... kwakuwa hawatakiwi kufanyakazi wanatakiwa kuhudumiwa...
 
Habari wakuu, naomba kufaham njia rahisi (cheap) ya kusafiri kwenda Sweden. Natarajia kusafiri mwezi august ila nataka kubana sana bujeti yangu.

Natanguliza shukrani

cc: lusungo, izzo, Richards, na wengineo wote
 
visa unayo?
 
kama ni ya EU is very simple b
ndio iko tayari
ook flight by KLM mpaka amsterdam then panda Treni ya umeme ni karibu na more cheaper au angalia alternatives zote kwenda straight mpaka stolkhom au kushukia amsterdam
 
Wanaothubutu naomba watupe MREJESHO ili kutoa hamasa kwa wengine!!
Hii itasaidia sana
 
Dah wadau naona thread imepoa au watu mmeshasafiri nini????????????

I have good newz for you nimewasiliana na zile taasisi nilizo sema kwenye project number 2

So mwezi wa 5 Tanganyika mnaweza pata ugeni wa vijana wa 5 kutoka nchi pendwa ya Malta wa tatu wadada na wawili ni wakaka sasa kuhusu kuhost natafuta mtu mwaminifu wa kumuunganisha nao wakija yeye ndio awapokee na kuwatafutia host kama itawezekana

kirikou1 kweupee Hary Jay Ndata Prishaz WiseLady Mrike wembeee talentboy Dr.adams faida Daby Tombstone Piledrive Padri Mcharo Shyshii lucley kui tagamwa binti kiziwi dangadunguri Tembo2 lusungo kweupee pius1021 Prof cognition Agogo Jr Chakochangu soul provider Mrike
Mm hapa nichek kwa email mtamadunsanaa@gmail.com namba ya simu 0692637111
 
kwanini unalazimisha tutiririke hapa? kwa kifupi hujaongea uhalisia wa maisha ya huko jinsi yalivyo magumu kwa uzoefu wa kuishi huko unapopaita ughaibuni nimegundua umedanganya vitu vingi sana na kama utataka nikuumbue nitafanya hivyo,

huko nje kuna wanaijeria wengi wanafanyishwa kazi kama watumwa wa kingono na makahaba, kuanzia italy hadi huko USA, kuna wengi waliondoka wazima lakini wakarudi washakua mabwabwa.

katika vitu ambavyo sintovisahau maishani ni ile hali ya kudharauliwa na kubaguliwa kwavile tu mimi ni mwafrika,
niliwahi kwenda kumsabahi jamaa yangu mmoja katika visiwa vya Turks and Caicos ambavyo karibu na jamaica na dominican republic maarufu sana kutokana na jiji lao liitwalo santo domingo, nilitoka vizuri pale Nassau bahamas nikiwa na round trip air ticket, nikapanda ndege kuelekea katika nchi hiyo ila nilipofika katika uwanja wao wa ndege uliop Cock bun, baada ya kutoa passport yangu ili nikaguliwe nitoke, ilipoonekana tu niya TZ, nikaambiwa nitulie pembeni kwanza wahudumiwe wazungu wa ulaya na marekani, kisha nikachukuliwa maelezo kuhusu nchi yangu, Tz ipo afrika sehem gani? nami nimefuata nini huko kwakua hawajazoea kumuona mwafrika anaenda kutembea katika kisiwa hicho cha maraha, nikawaeleza nimekwenda kumtembelea jamaa yangu ambae ni mzaliwa wa hapo, nikapekuliwa kisha wakanikuta nina cash dola 3000 na pia ni visa card ya carebean bank, maswali yakawa mengi zaidi imekuaje mtu kutoka africa ana hizo pesa na pia anavisa card, nikawajibu mimi ni mwanafunzi naishi katika nchi ya jirani tu na hapo, swali lingine huko kwenu afrika hakuna vyuo mpaka uje kusoma huku? au ndio mmeishakimbia kama kawaida yenu, cha kushangaza watu hao na wenyewe ni weusi tu kama sisi, niliumia saana mpaka mwenyeji wangu anafika na kunichukua tayari hamu ya kukaa hata zile wiki mbili ilikua ishakata.

naomba niwashauri tu ndugu zangu kama uanweza kuangalia fursa na kuzifanyia kazi ni bora kufanya hivyo,,,

sishauri mtu kukimbia na kuishi maisha ya kubaguliwa as if hauna nchi....
Mkuu Bruce Lee
Kwanza pole Na Ubaguzi ulio kutana nao huko Caribbean.Ubaguzi tunao Hapa Hapa Bongo.Tukianza Na uhamiaji yetu sio wote wanawanyanyasa watu Wanao toka nchi za kiafrika.Fikiria wewe ndio Mnaigeria umetuwa Dareslam unafikiria utapewa (red carpet?).
Mwanzilishi wa uzi huu kafungua ili kutoa mwanga kwa Watu wanao taka kwenda nje.Kaandika maoni yake Na Kwa mtu yeyeto anaye taka kuchangia.Hamna mtu alielazimishwa kuchangia wala kukubali maoni yake.
Milango mingi imefunguliwa Ktk huu uzi.Kuanzia vyuo vikuu duniani,kupata passport,namna ya kwenda kuomba visa balozi mbali mbali,Kuhusu Japan,Malta,SA,EU,USA Na nchi nyingi tu. Tovuti za kujifunza Lugha za nje.
Siwezi kuviorodhesha vyote.Kwa kifupi watu wengi wanaelewa changamoto za nchi za nje :Ubaguzi,kudharauliwa,utumwa pamoja Na yote hayo wengi wanataka kujionea kama yalivyo kukuta wewe,
Muhimu NI kutoka BONGO Hata ukirudi akili Na fursa zitafunguka.Kabla ya wewe kwenda Ughaibuni ungeyajuaje mambo yote uliyo ya eleza? Umethubutu kwenda nje ya Tanzania.
Hongera sanaaaaa tu Kwa Lusungo,Richard,Izzo,Tokyo 40,Segito wa kalenga,Chillah,Isanga family,BAK,na wachangiaji wote ambao sikuwataja Kwa majina Na bila ya kukusahau Wewe Bruce Lee.
Mubarikiwe Wote.
 
izzo nakuelewa sana,mimi natamani nirudi hata leo tz nianze michakato ila nina contract ya kazi imenibana mpaka mwezi wa 7 ntarudi tz.
wabongo wanapenda stori lakini kufanyia kazi ni suala jingine.
Kuna ndugu nmempa mpango mzima wa kwenda Malta kutafuta maisha na nauli ntamuazima kanijibu nisubiri atafikiria wakati anakaa nyumbani hana kazi wala nini,anakaa kwenye tv 25 hours..
nipe mm iyo fursa hakika sitachezea namba yangu hii hapa 0692637111 email mtamadunsanaa@gmail.com
 
izzo nakuelewa sana,mimi natamani nirudi hata leo tz nianze michakato ila nina contract ya kazi imenibana mpaka mwezi wa 7 ntarudi tz.
wabongo wanapenda stori lakini kufanyia kazi ni suala jingine.
Kuna ndugu nmempa mpango mzima wa kwenda Malta kutafuta maisha na nauli ntamuazima kanijibu nisubiri atafikiria wakati anakaa nyumbani hana kazi wala nini,anakaa kwenye tv 25 hours..
Naomba unisaidie juu ya hilo nataman sana kutoka bongo na ntafanya kujituma niendako tatizo lipo tu kwenye nauli bas
 
Mkuu Bruce Lee
Kwanza pole Na Ubaguzi ulio kutana nao huko Caribbean.Ubaguzi tunao Hapa Hapa Bongo.Tukianza Na uhamiaji yetu sio wote wanawanyanyasa watu Wanao toka nchi za kiafrika.Fikiria wewe ndio Mnaigeria umetuwa Dareslam unafikiria utapewa (red carpet?).
Mwanzilishi wa uzi huu kafungua ili kutoa mwanga kwa Watu wanao taka kwenda nje.Kaandika maoni yake Na Kwa mtu yeyeto anaye taka kuchangia.Hamna mtu alielazimishwa kuchangia wala kukubali maoni yake.
Milango mingi imefunguliwa Ktk huu uzi.Kuanzia vyuo vikuu duniani,kupata passport,namna ya kwenda kuomba visa balozi mbali mbali,Kuhusu Japan,Malta,SA,EU,USA Na nchi nyingi tu. Tovuti za kujifunza Lugha za nje.
Siwezi kuviorodhesha vyote.Kwa kifupi watu wengi wanaelewa changamoto za nchi za nje :Ubaguzi,kudharauliwa,utumwa pamoja Na yote hayo wengi wanataka kujionea kama yalivyo kukuta wewe,
Muhimu NI kutoka BONGO Hata ukirudi akili Na fursa zitafunguka.Kabla ya wewe kwenda Ughaibuni ungeyajuaje mambo yote uliyo ya eleza? Umethubutu kwenda nje ya Tanzania.
Hongera sanaaaaa tu Kwa Lusungo,Richard,Izzo,Tokyo 40,Segito wa kalenga,Chillah,Isanga family,BAK,na wachangiaji wote ambao sikuwataja Kwa majina Na bila ya kukusahau Wewe Bruce Lee.
Mubarikiwe Wote.

exposure nilioipata ndio imenifanya kua mbunifu zaidi na kuziona fursa zaidi zilizopo hapa nyumbani na sasa nachokifanya ni kutumia rasilimali zilizopo nchini na kujenga strong financial base halafu huko hua naenda kutembea na kujifunza zaidi, karibu saana mkuu waweza tembelea website yangu caanansupplies.co.tz tuongee zaidi na kupeana fursa zipo nyingi sana. hakuna kitu kizuri kama unaenda nje ku relux kuliko kwenda ku unga unga vi dei waka ili usurvive.
karibuni wote
 
Good
 
sio mbaya mkuu, ila huko botswana wapo very organized, huwezi zamia na kujificha muda mrefu, pia pesa yao inaitwa Pura ina thamani kuliko Rand ya Afrika kusini, la muhimu ningekushauri ingia online tafuta shule ya sekondary au msingi binafsi anza kuomba kazi ukiwa huku huku pia omba hata kupitia wizara ya Elimu ya huko ukiwa huku, wakikukubali hutopata matatizo, na hata kama ukipata shule ya binafsi inamaana shule hiyo ndio itakayokusaidia kupata work permit na documents zingine, nakuhakikishia huko lazima upate mdada mzuri na atakupenda kweli kwa kifupi Botswana wanawake ni wengi saana kuliko wanaume, na pia watu wengi hua wanachelewa kuoa kwahiyo we mbongo ukifika na ukatangaza ndoa mbona faster unapata jiko.

Daah, kuna bia zao za ukweli sana St Luis hazina hang over. kule utakutana na watoto wa herero miguu ya bia......

kila la heri kaka. mi hua naenda enda huko.
Mkuu ww upo Gaborone au umeishi huko?
 
Back
Top Bottom