izzo kama umeona comment yangu hili suala nimeliongelea hapo juu. Tunaopewa ushauri tujitahidi tunayoambiwa tuyafanyie kazi la sivyo hizi zitakuwa stori kama za chit-chat.
Sipo perfect kuhusu hili ila jamani tunaoshauriwa ili washauri waendelee kutupigania lazima tuonyeshe efforts japo kidogo. Binafsi sikutaka kuexpose nilipofikia kwasasa ila kwa comment yako hii imenibidi japo nitaelezea kwa ufupi.
Kuna jamaa nilikutana naye na nafikiri nilimwelezea kule nyuma nikasema anayehitaji msaada wake anifuate ila sikuona reponse ya mtu yeyote. Huyu jamaa anadeal na visa za Canada na Europe anakutafutia visa then pia anakutafutia mbongo au mtu yeyote wa kukuhost kwa muda huku ukikamilisha mambo yako. Gharama yake ni usd 2000 ila ukiongea naye kikubwa inapungua.
So binafsi nimeamua kudeal naye ananishughulikia visa ya sweden a process zimeanza. Safari itakuwa before tareh 20 April. Kuhusu kurushwa jamaa sina mashaka naye japo binadamu sio wa kuwaamini.
Changamoto iliyopo kwake:
Ni namna ya kupata makaratasi maana napotoka huku nakuwa na schengen visa so bado nafanya mchakato wa namna ya kupata makaratasi na kuishi muda mrefu. Kuna watu nimekutana nao wananipa ramani ya kupata makaratasi lakini still michakato haijafikia hatua inayostahili ila shukrani kwao saana saana.
Gharama za jamaa ni nyingi maana hizo usd nilizotaja hapo sio kitoto.
Ombi langu kwenu kama kuna mtu anajua machimbo ya kupata papers nikishafika nishaurini ila nimeamua kujilipua April.
Msichoke kutushauri vijana wapo wanafutilia documents ila ni vizuri ndugu zangu muweke updates hapa tuwape moyo kina
lusungo na
izzo wanayofanya ni zaidi ya tuliyotarajia kuyapata.