Habari wapendwa,
Ninahitaji kubadilisha matairi ya gari size 195/70 R14
Ninaomba kufahamu uzuri na ubaya wa brands zifuatazo
1.YANA
2.APOLLO
3.JK TYRES
4.TRIANGLE
5.GOODRIDE
Bajeti yangu itaruhusu brands nilizoorodhesha ila unaweza kuongeza nyingine na kutoa ushauri..
Natangulisha shukrani..
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu amani!
Sasa mimi sio fundi wala sio mtaalam sana wa hivi vitu ila naweza kupatia uzoefu wangu wa kuwa na magari kadhaa na kutumia tairi tofauti tofauti.
Kwa maoni yangu, ununuzi wa tairi hutegemea na mfuko wako, matumizi yako, interest/prestige yako.
1. Sasa basi kama gari yako ni kwa matumizi ya town trips tu, nakuhakikishia tairi yeyote mpya inatosha kwa matumizi hayo na itakufaa kwa muda mrefu tu. Hivyo waweza nunua yeyote kati ya hizo. 100% Ok.
Ila kama matumizi yako una safari za mara chache za mbali tairi nyingi za bei nafuu zaweza kufaa kwa 75% ndani ya mwaka hivi.
Kama aina ya gari ni sedan, ambayo unatumia tu katika barabara nyingi za lami bado zipo sawa kwa kiwango kikubwa tu.
Kama gari yako ni suv na mara nyingi upo offroad basi kwa maoni yangu Bf Goodrich na Dunlop wana tairi nzuri sana kwa mahitaji hayo.
Kama una SUV na unapenda mwendo kasi kwa maoni yangu hakuna tairi nzuri kuzidi Michellin. Ni nyepesi na ni imara yaani kasi no ya kufa mtu.
2. Mfuko wako - Kama pesa yako ni ya kuunga,
Kwa sedan tairi ulizozitaja zote ni nzuri ila goodride ni best.
Kwa SUV, Linglong ana tairi nzuri kama utakuwa offroad sana.
Ila kama pesa ni ya kutosha tairi bora kwa suv offroad ni Bf Goodrich na kwa mwendo ni Michellin ila uwe na pesa ya kutosha.
3. Prestige - Kuna watu hawataki tairi zenye majina madogo so wanataka majina makubwa ikiwa ni sehemu ya hadhi.
Kama upo kundi hili nunua matairi yenye majina makubwa kama niliyoyataja, la hasha nunua hayo ambayo hayafahamiki lakini yanaweza kukufaa.
Mwisho: Lipo suala la uimara, ukweli ni kwamba tairi mpya ni mpya tu hata iwe na jina gani. Unaweza kuitumia mwaka mzima bila kupata shida yeyote. Nina maanisha kuwa tairi nyingi mpya ni reliable.
Ila zipo nyingine ni imara zaidi na zina ubora zaidi katika mazingira fulani fulani na hapo ndipo bei zinatofautiana.
Naomba kuwasilisha.