kayanda01
JF-Expert Member
- Feb 14, 2014
- 1,216
- 1,062
Feki hakuna na Dunlop zote lazima waoneshe hivyo vitu vyote muhimu nahisi hukutazama vizuri mkuu
Mkuu, trust me. Kwa macho yangu nimekagua sana carefully na kushuhudia Dunlop 185/65/15 ya South Africa (made by Sumitomo) hazina kabisa rating ya TREADWEAR wala TEMPERATURE wala TRACTION.
Ilinishangaza sana! Muuzaji akasema kuwa eti size hiyo tu (185) Dunlop hawawekagi hizo ratings tajwa.
Nilizunguka kwa sellers wengine watatu tofauti, kote hali ni ile ile. Tairi haioneshi TEMPERATURE wala TRACTION wala TREADWEAR ratings.
Nikaelekezwa niende kwa NAS Tyres ltd kwamba ndiyo Authorized Dealer wa Dunlop kwa kanda hiyo. Nas tyres wakanambia hawauzi rejareja. Wakanilink na agent wao aliyepo pale pale mjini. Nikaenda kwa agent, akanambia nisubiri lisaa limoja tyre zitakuwa tayari. Tyres zilipofika, ni vile vile... hazina rating ya temperature wala TREADWEAR wala TRACTION. Dunlop 185/65/15 by Sumitomo South Africa.
Nikaenda Autoexpress garage... wakawa hawana hizo tyre.
Nikaghaili na kuachana nazo!!
Ilikuwa ni Mwanza. Nilikuwa nahitaji tyres 6 za Dunlop size tajwa.
So, nahisi kabisa Dunlop size 185/65/15 zilizopo Mwanza ni fekero!!
Mkuu, naomba nawe ulichunguze hili, specifically Dunlop za Sumitomo South Africa, size 185/65/15 zilizopo hapo dukani kwako, zinaonesha ratings za temperature na traction na treadwear?