Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Puppet ndio anaefaa kuachia ngazi mara moja,
maana jana ameinanga sana hotuba ya chairman kwakusema kwamba nothing new at all 🐒
Habari Wana JF. Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samiah.

Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe 21/1/2023, Mbowe alidai hatamsema vibaya mama Samiah , Leo inakuwaje ndio anashtuka muda umeenda? na kudai anajuta kumwamini Mama Samiah?.

Pia nakumbuka kwenye mkutano wake na diaspora wa Marekani tarehe 11/12/2022, Mh Mbowe alidai kuwa hatarudi nyuma kwenye mazungumzo, na kudai anaweka maslahi ya nchi mbele na sio CHADEMA, Leo inakuwaje anajutia kumwamini Rais Samiah.

Mh. Mbowe anajua yaliyotokea Zanzibar na alitakiwa kuchukua Kama fundisho. Kwamba pamoja na maridhiano, CCM wakaiweka CUF ya maalim kwenye mtego mpaka leo imekuwa historia. Mwishoni maalim ikabidi akimbilie ACT baada ya Msajili kutumika kumfustrate. Hii ilitosha kumfundisha Mbowe aache kujikomba kwa Mh Samiah na CCM yake. Ilitakiwa ajifunze kutoka kwa Maalim. Kwamba pamoja na Maalim kujishusha na kukubali maridhiano , CCM wakakivunja chama chake Cha CUF na pia kumfanyia unyama 2020.

Sasa Kutokana na kauli ya Mh Mbowe ya Jana, Naomba nishauri yafuatayo:

1. Kwakuwa Mh. Mbowe alilazimisha Maridhiano na yeye kujiweka mbele Kama kiongozi wa maridhiano, basi kwa kuwa maridhiano yameshindikana, nashauri aachie ngazi mara moja. Maana kashindwa kutimiza hayo maridhiano aliyo lazimisha.

2. Kwa kuwa Mh. Mbowe alidharau sauti za wanachama wa CHADEMA kumkataza kuendelea na hayo maridhiano, na kwa kuwa hakufanikiwa na hayo maridhiano aombe Radhi wanachama kwa maamuzi hayo ambayo hayakufanikiwa na yaliyoiweka CHADEMA rehani.

3. Kwa kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kutimiza approach yake ya diplomacy , itakuwa ujinga akiendelea kuongoza approach nyingine dhidi ya serikali au CCM maana haaminiki Tena. Hivyo ajiuzulu kupisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambaye atatumia approach nyingine kabisa kuliko ya Mbowe.

4. Kwamba, kwakuwa imeonekana maridhiano sio njia sahihi ya kutatua malalamiko ya CHADEMA kutokana na kiburi Cha CCM na serikali yake, nashauri CHADEMA waachane na approach ya maridhiano watafute approach nyingine.

5. Kwa kuwa inaonekana maoni ya CHADEMA kwenye mswada ya sheria yamekataliwa na Kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria, nashauri CHADEMA watangaze rasmi kutoshiriki chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Naomba kuwasilisha.
 
1. Hoja iliyopo ni kuwa chama kimekosa mwelekeo, hakuna tunachoamini, hatuna msimamo.

2. Leo hili kesho lile. Imekuwa mwendo wa kimang'amu ng'amu.

3. Tunasema CCM haitatoka madarakani kwa siasa hizi.

4. Tunataka falsafa, Imani na misimamo ya wazi tujue Kwa uwazi tunasimamia nini

5. Kulikoni kuanza kuandika vitu vyako kuwawekea wengine mdomoni?

6. Kama hujui kinachoongelewa ustaarabu ni kuuliza.

7. Bottom line demokrasia ndiyo mwamuzi si mtu mmoja.

8. Kama wanachama tuna haki sawa.
Ni chama kipi kisichokuwa na changamoto? Vyama vipo vingi na pia kuna ruhusa ya kuanzisha vingine vipya. Kwa yeyote anaeona Chadema ya Mbowe ina changamoto ni ruksa kutimukia chamaa kisicho na changamoto au kuanzisha chama chake.

Kwa wenye weredi kipindi hiki cha karibu na uchaguzi ni kukaa pamoja na kutatua changamoto kwa pamoja kuliko kuhubiri mifarakano yenye lango la kukigawa chama.
 
"Kesi" nimetumia kama msemo tu, nikiwa na maana kutofautiana mawazo.

Maswali yako mengine kuyajibu naona kuchoshana, kama una hoja iweke kwa mtindo huo twende sawa, lakini sio maswali juu ya maswali...

Ajabu unasema nimeandika mengi yasiyo eleweka halafu unasema kwangu neno "demokrasia ni shida", wakati kwenye hayo maelezo yangu nimekuonesha na wenzako demokrasia ikoje kwa vitendo, na sio maneno kama haya unayoandika hapa.

- Hapo demokrasia ni shida kwangu au kwenu? au kwenu demokrasia simply mnamaanisha mnachokitaka nyie ndio lazima kiwe tofauti na wengine walivyoamua?! kutaka Mbowe aondoke mna maana ipi? ndio demokrasia yenu hiyo?! hata siwalewi na ndio maana hata mleta mada nae amepotea!.

All in all, muda wa Mbowe ukifika ataondoka, simple, kama hamumtaki muandaneni yule mumtakaye, lakini kupiga kelele zenu wakati huu ni kukivuruga chama kikiwa kwenye harakati zake nyingine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nadhani kuna genge fulani ndani ya Chadema lisilomtaka Mbowe. Watu wanatumia neno demokrasia bila weredi wa neno lenyewe. Wengi wapewe na wachache wasikilizwe. Si rais kutekeleza matakwa ya kila mmoja ndani ya chama chochote cha siasa, wapo wengi wanaopenda Mbowe aendelee kuwa m/kiti na wachache kwa interest wanazozijuwa wao hawataki, hiyo ndio demokrasia wenyewe.

Changamoto ndani ya vyama vya siasa ni jambo la kawaida, na hakuna formula ya kufikia mafanikio, cha muhimu ni kutokata tamaa.
 
Tatizo unataka kunilazimisha kuukataa ukweli. Naomba nikuelimishe kidogo tu, mikutano ya siasa ni haki ya kila raia, haikutakiwa maridhiano kujirudisha Bali kauli ya kisiasa tu kutoka kwa Rais.

Naomba nikupe ushahidi wa mambo mawili kwamba Mbowe alituhakikishia kwamba mambo yataenda vizuri. Kwa mfano Kwenye mkutano wa kwanza wa CHADEMA 2022, pale Mwanza Mbowe alisema wazi kwamba yeye hatamsema vibaya Mama Samiah. Ile kauli ilisababisha CCM kudai Mbowe anampigia kampeni mama Samiah na kuonesha kwamba CHADEMA inamuunga mkono mama Samia, pamoja na dhihaka zote Mbowe akiendelea na hiyo kauli. Leo utasemaje kwamba ilikuwa bahati mbaya?. Mbowe kakiingiza chama kwenye Jambo ambalo chama kingeweza kuepuka.

Pia baada ya hapo Akina Lissu wakapinga maridhiano na CCM ikiwemo na Mimi, Mbowe akashupaza shingo na kudai ameweka taifa mbele kuliko chama. Sasa leo utadai ni bahati mbaya au makosa ya kibinadamu?. Yani mtu anashauriwa hataki, halafu Leo analeta stori za kujuta wakati amekiingiza chama kwenye shida?.

Msimamo wangu ni kwamba pamoja na Mbowe kujuta, aachie madaraka kuonesha kweli anajutia.
Wewe una lako jambo, Mbowe kama mwenyekiti alikuwa na haki ya kuwa na misimamo kama hiyo uliyoisema akiamini kukivusha chama kwa njia ya maridhiano. Aliyeshidwa kutekeleza hayo maridhiano siyo Mbowe wala Chadema hisipokuwa Samia kwa shinikizo la waafidhina ndani ya CCM. Kwanini Mbowe aachie ngazi kwa kosa ambalo hakulitenda yeye? Kama kuna sababu nyingine zielezeni lakini si hizi za maridhiano.

Ni muda mrefu tangu vyama vingi vianzishwe na njia nyingi zimekuwa zikitumika kukabiliana na wizi, sheria kandamizi za uchaguzi na mambo mengine. Njia zote hizi kwa muda wote hazijawai kuzaa matunda. Iweje hii ya maridhiano ndilo liwe kosa la kumfanya aachie ngazi?
 
Nikuulize swali, Mbowe ameenda kwenye vita gani? Na Silaha gani?. Kwa hivyo kujirahisisha kwa Samiah ndio Silaha. Wewe ndio uamke usingizini.

Mbowe must go, maana approach yake imeshindwa ameleta dharau kwa CHADEMA. Yani kukiri kuzidiwa maarifa na mama Samiah ni upuuzi mkubwa.
Unachekesha, kwamba amekiri kuzidiwa maarifa na mama Samia? Ni lini Chadema ilishaizidi maarifa CCM? Kosa lake ni kusema ukweli au kukaidi lile mlilolitaka nyie? Mara ngapi nguvu imetumika kuikabili CCM ikashindikana? Leo hili la maridhiano imekuwa jinai
 
Kukubali amekosea sio vibaya, shida ni kwamba wakati anakosea akaonywa ila akakaza shingo na kuwaona akina Lissu ndio wenye shida. Leo anarudi kulalamika amaechezewa na CCM. Sasa anamlalamikia nani?.

Ili kunielewa vizuri, kaangalie video ya mkutano wa Mbowe Marekani kwa diaspora alivyoongea na Leo anavyoongea. CHADEMA haiotaji kiongozi kinyonga never.
Kukosea hata kama alionywa na kina Lissu ndiyo siasa yenyewe, sasa kajisahihisha baada ya kuona yaliyotokea. Chama kaaeni pamoja na kuandaa mikakati mipya.

Ukiniambia una mahaba na Lissu awe m/kiti, Heche Katibu na Ruge makamo nitakuelewa maana hiyo ndiyo demokrasia. Lakini fuateni utaratibu ndani ya chama na kama wengi watakuwa na mtizamo kama wako sawa, lakini kama wengi bado wako kwa Mbowe basi sanduku la kura litaongea.
 
Ni chama kipi kisichokuwa na changamoto? Vyama vipo vingi na pia kuna ruhusa ya kuanzisha vingine vipya. Kwa yeyote anaeona Chadema ya Mbowe ina changamoto ni ruksa kutimukia chamaa kisicho na changamoto au kuanzisha chama chake.

Kwa wenye weredi kipindi hiki cha karibu na uchaguzi ni kukaa pamoja na kutatua changamoto kwa pamoja kuliko kuhubiri mifarakano yenye lango la kukigawa chama.

Ninalazimika kukujibu kikamilifu, kwani kiungwana, hoja hujibiwa kwa hoja:

1. Hakuna popote nilipowahi kuona yeyote akisema kuna chama hakina changamoto. Wala eti kuwa vyama ni vingi ni habari mpya.

2. Hivyo hoja zako kuhusiana na #1 ni zako, na simjui mwingine zinayemhusu kwa vyovyote.

3. Kuanzisha chama hiyo ni hoja yako. Mtu hufanyia kazi hoja zake. Kulikoni wewe kutoifanyia kazi hoja yako? Au kulikoni kutoa Ushauri binafsi usioombwa?

4. CHADEMA ya Mbowe siijui. Nikidhani vyama ni vya umma. Wenye nchi wananchi kama walivyo wanachama.

5. Hoja yako kwenye #4 unaiona ilivyo mufilisi? Nendeni shule ndugu. Elimu haina mwisho mkapate exposure hata ya kujieleza tu.

6. Mtu anaanzisha je chama chake wakati vyama ni vya umma? Ni mawazo yako kuwa mnacho chama binafsi wewe na nani?

7. Kwenye #6 ni vyema ukajitathmini na hasa kujiridhisha kuihusu afya ya akili yako. Tusiishie kuwashauri kina chalamila kumbe tuna wetu ndani.

8. Hapo #7, kumbe kama manyani hatuyaoni mak*nd* yetu na tunao wetu tukidhani ni wenzetu kumbe wao wakidhani ni malaika.

9. Wapi umeona kumehubiriwa mifarakano? Mara ngapi tumesema na hata kusihi maboresho, na mengi tukiyaona matokeo?

10. Ni mwanzo wewe leo kuona nyuzi kama hIzi:

a) CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

b) Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

c) Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

d) Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

e) Lissu ndilo tegemeo tulilo nalo kwenye kuikomboa nchi hii sasa

f) Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

g) Nk.

11. Mkuu usipende kujipa umuhimu chamani dhidi ya wengine. Usijifanye kukipenda chama sana kuliko wengine.

12. Hapo #11, kwa kipimo kipi ndugu?

13. Ustaarabu ni kujibu hoja kwa hoja.

14. Jiuilize kwenye ulichokuwa umeandika: "ulikuwa ukijibu hoja ipi, wapi?"
 
Ninalazimika kukujibu kikamilifu, kwani kiungwana, hoja hujibiwa kwa hoja:

1. Hakuna popote nilipowahi kuona yeyote akisema kuna chama hakina changamoto. Wala eti kuwa vyama ni vingi ni habari mpya.

2. Hivyo hoja zako kuhusiana na #1 ni zako, na simjui mwingine zinayemhusu kwa vyovyote.

3. Kuanzisha chama hiyo ni hoja yako. Mtu hufanyia kazi hoja zake. Kulikoni wewe kutoifanyia kazi hoja yako? Au kulikoni kutoa Ushauri binafsi usioombwa?

4. CHADEMA ya Mbowe siijui. Nikidhani vyama ni vya umma. Wenye nchi wananchi kama walivyo wanachama.

5. Hoja yako kwenye #4 unaiona ilivyo mufilisi? Nendeni shule ndugu. Elimu haina mwisho mkapate exposure hata ya kujieleza kwa weledi.

6. Mtu anaanzisha je chama chake wakati vyama ni vya umma? Ni mawazo yako kuwa mnacho chama binafsi wewe na nani?

7. Kwenye #6 ni vyema ukajitathmini na hasa kujiridhisha kuhlihusu afya ya akili yako. Tusiishie kuwashauri kina chalamila.

8. Hapo #7, kumbe kama manyani hatuyaoni mak*nd* yetu na tunao wetu tukidhani ni wenzetu kumbe wao wakidhani ni malaika.

9. Wapi umeona kumehubiriwa mifarakano? Mara ngapi tumesema na hata kusihi maboresho, na mengi tukiyaona matokeo?

10. Ni mwanzo wewe leo kuona nyuzi kama hIzi:

a) CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

b) Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

c) Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

d) Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

e) Lissu ndilo tegemeo tulilo nalo kwenye kuikomboa nchi hii sasa

f) nk

11. Mkuu usipende kujipa umuhimu chamani dhidi ya wengine. Usijifanye kukipenda chama sana kuliko wengine.

12. Hapo #11, kwa kipimo kipi ndugu?

13. Ustaarabu ni kujibu hoja kwa hoja.

14. Jiuilize kwenye ulichokuwa umeandika: "ulikuwa ukijibu hoja ipi, wapi?"
Hebu andika vizuri ueleweke, hafu wewe ndio unawambia wengine waende shule wakati hujui kupangilia hoja zako. Bahati mbaya unadhani ndani ya jf upo wewe peke yako unaeandika. Nimesema anzisha chama chako nikimjibu aliyedai Mbowe karithishwa chama na mkwe wake. Na wewe kama unaamini Chadema ni ya wanachama na wafuasi wake, basi pasiwe na kikundi cha watu wanaodhani mawazo yao ni sahihi kuliko ya wengine. Swala la Mbowe kuachia ngazi litegemee maamuzi ya walio wengi na si ka kikundi cha watu.
 
1. Nilichukua muda kukujibu hoja zako zote kwa mpangilio murua kabisa, hoja kwa hoja na aya kwa aya zilizokuwa numbered kuwezesha kuzirejea kirahisi.

2. Kwamba umeandika gazeti, na lote ni aya moja: na kuwa wala hujishangai?

3. Utanisahihisha wapi mkufunzi wa uandishi, kwenye uandishi wewe ndugu? Punguza ujuaji.

4. Siyo wewe huyu ukiniandikia miye awali kuwa: "kama vipi kuanzisha chama?"

IMG_20240114_201018.jpg

5. Hapo #4, linganisha na ulichoandika sasa kulihusu la kuanzisha vyama, kutambua kumbe una matatizo ya msingi ya kumbukumbu.

6. Ulijirisha na mawazo ya kwenye nyuzi nilizoambatanisha awali #10 (a) - (g)? Au ukakurupuka na kuanza kuandika majibu kama umepagawa tu?

7. Ulitambua tunaongelea matatizo ya kukosa misimamo au nini tunaamini; ambayo chimbuko lake limeelezwa mle?

8. Ulitambua umuhimu wa #10 (d)?

9. Kumbe unadhani tuna tatizo na Mbowe kama mtu? Kwanini basi kuchukua muda kushauri kote ilikowezejana hadi huku mitandaoni kama njia ya mwisho?

10. Tunaitoa je CCM madarakani na watu wasiojua wanachokiamini au kukisimamia?

11. #10 (d) Inatuleta hapa:

"Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM."

12. #11 hapo, tunajua CCM na washirika wake kwa kujua au kutokujua wangependa mno tunyamaze, bila shaka kama ninavyo kusoma wewe hapa.

13. Soma #11 kwa utulivu kujiridhisha; kwa hakika, kunyamaza siyo option!

14. Kulikoni tunyaze? Kwanini kusalimu amri Kwa CCM? Kwa nini tusibanane hapa hapa?

Mbona tutaelewana tu?
 
Aisee! Watu walimtaka Mbowe aweke wazi anaongea nn ktk maridhiano, lkn yeye akafanya siri. Sasa inamtafuna.

Kwa maoni yangu Mbowe akubali kuwajibikq kwasabb plan yake hii imefeli.
 
View attachment 2871884

Brazaj; swali moja ambalo umeshidwa kunijibu. Maridhiano ya Mbowe na Samia ni ya hivi karibuni, uko nyuma Chadema na vyama vingine vya upinzani vilishatumia njia mbalimbali kuikabili CCM lakini njia zote zimefeli. Sasa niambie, kwanini Mbowe ajiuzuru kisa tu mpango wake wa maridhiano umeshidwa kuzaa matunda?

Lakini tusiangalie package moja tu kwenye haya maridhiano, niambie tena, ni wanachadema wangapi wameachiwa huru toka mahabusu na magereza chini ya mpango huu wa maridhiano? Mnalalamikia maridhiano lakini hamtoi njia mbadala iliyopaswa kuchukuliwa na kutoa matokeo chanya.
 
Aisee! Watu walimtaka Mbowe aweke wazi anaongea nn ktk maridhiano, lkn yeye akafanya siri. Sasa inamtafuna.

Kwa maoni yangu Mbowe akubali kuwajibikq kwasabb plan yake hii imefeli.
Usiri wa majadiliano ni jambo la kawaida kabisa, na nijuwavyo Mbowe hakuwa peke yake kwenye hayo majadiliano hivyo chama kilijuwa ni nini kilichokuwa kikijadiliwa na maafikiano yaliyofikiwa. Shida ilianzia kwenye vyama vingine vya upinzani vilivyo ona vimetegwa na vilevile mitizamo tofauti kati ya Lissu na Mbowe kwenye hili jambo.

Kukwama kwa maridhiano siyo sababu inayojitosheleza ya kumfanya Mbowe aachie ngazi.
 
Habari Wana JF.

Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samia

Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe 21/1/2023, Mbowe alidai hatamsema vibaya mama Samia. Leo inakuwaje ndio anashtuka muda umeenda? na kudai anajuta kumwamini Mama Samiah?.

Pia nakumbuka kwenye mkutano wake na diaspora wa Marekani tarehe 11/12/2022, Mh Mbowe alidai kuwa hatarudi nyuma kwenye mazungumzo, na kudai anaweka maslahi ya nchi mbele na sio CHADEMA, Leo inakuwaje anajutia kumwamini Rais Samiah.

Mbowe anajua yaliyotokea Zanzibar na alitakiwa kuchukua Kama fundisho. Kwamba pamoja na maridhiano, CCM wakaiweka CUF ya maalim kwenye mtego mpaka leo imekuwa historia. Mwishoni maalim ikabidi akimbilie ACT baada ya Msajili kutumika kumfustrate. Hii ilitosha kumfundisha Mbowe aache kujikomba kwa Mh Samiah na CCM yake. Ilitakiwa ajifunze kutoka kwa Maalim. Kwamba pamoja na Maalim kujishusha na kukubali maridhiano , CCM wakakivunja chama chake Cha CUF na pia kumfanyia unyama 2020.

Sasa Kutokana na kauli ya Mbowe ya Jana, Naomba nishauri yafuatayo:

1. Kwakuwa Mbowe alilazimisha Maridhiano na yeye kujiweka mbele Kama kiongozi wa maridhiano, basi kwa kuwa maridhiano yameshindikana, nashauri aachie ngazi mara moja. Maana kashindwa kutimiza hayo maridhiano aliyo lazimisha.

2. Kwa kuwa Mh. Mbowe alidharau sauti za wanachama wa CHADEMA kumkataza kuendelea na hayo maridhiano, na kwa kuwa hakufanikiwa na hayo maridhiano aombe Radhi wanachama kwa maamuzi hayo ambayo hayakufanikiwa na yaliyoiweka CHADEMA rehani.

3. Kwa kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kutimiza approach yake ya diplomacy , itakuwa ujinga akiendelea kuongoza approach nyingine dhidi ya serikali au CCM maana haaminiki Tena. Hivyo ajiuzulu kupisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambaye atatumia approach nyingine kabisa kuliko ya Mbowe.

4. Kwamba, kwakuwa imeonekana maridhiano sio njia sahihi ya kutatua malalamiko ya CHADEMA kutokana na kiburi Cha CCM na serikali yake, nashauri CHADEMA waachane na approach ya maridhiano watafute approach nyingine.

5. Kwa kuwa inaonekana maoni ya CHADEMA kwenye mswada ya sheria yamekataliwa na Kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria, nashauri CHADEMA watangaze rasmi kutoshiriki chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Naomba kuwasilisha.
.
 
Kwani umelazimishwa kuwa mwanachama wa CHADEMA? Anzisha chama, kikuze upate uzoefu wa vyama vya siasa kisha uje na hizi kelele za Mbowe jiuzulu.

CCM kazi yao ni kumtoa Mbowe kwenye uwenyekiti wa CHADEMA miaka yote. Mbowe mlimuweka jela muda mrefu tu, kwanini hamkummaliza huko huko?

Mbona hamsemi Lipumba ajiuzulu au Hasim Lungwe ajiuzulu? Kuna vyama tangu vimesajiriwa na msajiri wa vyama havijawahi kufanya mkutano au jumuiko lolote, na viongozi ni wale wale lakini sijawahi kusikia mkiwataka wajiuzulu, kwanini iwe ni Mbowe kila siku?

IFUTENI CHADEMA Kama inawakera sana.
 
Brazaj; swali moja ambalo umeshidwa kunijibu. Maridhiano ya Mbowe na Samia ni ya hivi karibuni, uko nyuma Chadema na vyama vingine vya upinzani vilishatumia njia mbalimbali kuikabili CCM lakini njia zote zimefeli.

I. Ninalazimika kukuwekea screen shots 3 (a, b, na c) kama rejea.

II. Bwana Mbusi umeandika kwangu mara mbili. Hii sasa ni ya tatu. Nakuwekea zote hapa ili ujiridhishe:

a) Post yako ya kwanza:

IMG_20240114_232427.jpg

b) Post yako ya pili:

IMG_20240114_232637.jpg

1. Swali unalodai kuniuliza kuhusu maridhiano ambalo nimeshindwa kukujibu liko wapi humo kwenye post yako ya kwanza au ya pili?

2. Swali lipi kwenye mabandiko yako hayo mawili, kuwa sijalijibu?

Sasa niambie, kwanini Mbowe ajiuzuru kisa tu mpango wake wa maridhiano umeshidwa kuzaa matunda?

Lakini tusiangalie package moja tu kwenye haya maridhiano, niambie tena, ni wanachadema wangapi wameachiwa huru toka mahabusu na magereza chini ya mpango huu wa maridhiano? Mnalalamikia maridhiano lakini hamtoi njia mbadala iliyopaswa kuchukuliwa na kutoa matokeo chanya.

3. Haya ya maridhiano umeyaokota wapi?

4. Hayo ya kujiuzulu umeyaokota wapi?

5. Zingatia mimi nilichoandika. Rejea post #4 kwenye uzi huu au popote pengine nilipoandika lolote:

c) Post (yangu) #4 kwenye uzi huu:

IMG_20240115_000602.jpg

6. Kulikoni kutaka kuniuliza lolote nje ya ninachokisimamia?

7. Tafadhali jikite kwenye nilichosema. Ya kwako yanihusu mimi au nani wapi ndugu?

8. Nitegemee majibu ya hayo yote 6 (bila kukosa) kama ni nia yako kujadili lolote nami tafadhali.

NB
: Nakuona una matatizo ya msingi sana na kumbu kumbu.
 
Binafsi Mbowe aliniudhi Sana Sana kwenye issue ya maridhiano na naamini bila chenga kuwa kuna sukari alilamba lamba kipindi hicho.si CCM wala chadema kwa muda mrefu walooongea lugha moja na sisi walalahoi. Ila kwa kuwa mbowe amerudi kwetu wananchi hatuna budi kumuunga mkono
 
Puppet ndio anaefaa kuachia ngazi mara moja,
maana jana ameinanga sana hotuba ya chairman kwakusema kwamba nothing new at all 🐒

Kuna Puppet zaidi ya Samiah. Maana yeye ndio anategemea wazungu wamkopeshe pesa. Usipende kuropoka.
 
Back
Top Bottom