denoo JG
JF-Expert Member
- Oct 27, 2023
- 2,701
- 9,759
"Kesi" nimetumia kama msemo tu, nikiwa na maana kutofautiana mawazo.1. Wapi unapoisoma unayoiita kesi? Kulikoni kutokujikita kujibu hoja kwa hoja?
2. Wanaohusika ni kina nani ndugu? Aghalabu na sisi unaothubutu kutuita tusiohusika labda nasi pia ni nani?
3. Kwanini neno demokrasia kwenu ni shida? Kwanini mnaotaka kuleta vurugu msiwe ni ninyi?
4. Kwanini hudhani tuliompigia kura Mbowe ni sisi? Na pia kwanini mnataka kujimilikisha chama? Kwanini mnadhani mna haki zaidi kuliko wengine?
5. Kwanini hamdhani chamani tuna haki sawa? Kwanini hamuoni kuwa mnahangaika kupinga demokrasia tunayoipigania nchini na vyamani?
6. Umeandika mengi ambayo kwa hakika hayana msingi wowote!
7. Hakuna tunapolazimisha lolote wala popote, zaidi ya kuwa tunaona mnataka kutulazimisha misimamo yenu mipya isiyokuwapo. Kilichokuwa chama cha haki, uhuru na demokrasia leo kimekuwa na siasa za tombola.
8. Ustaarabu ni kuwa, kukitokea kukengeuka, demokrasia huchukua mkondo wake. Ni Hilo tu tunalolitaka kurejelewa sasa.
9. Tumesema huyu bwana ana uchaguzi mmoja, ku retreat kwenye misimamo ya chama inayoeleweka au kupumzika?
10. Kulikoni #9, ni chungu mno kwenu? Kwamba mnataka kutulazimisha na siasa za ku bet? Hiki chama ni cha umma, si mali binafsi.
11. Kulikoni ninyi kutaka kuleta vurugu hivi? Ni watu wa namna gani ninyi msioweza kuona wanachama wanataka nini?
12. Waziwazi siasa hizi za kulamba sumu hatuzitaki.
CHADEMA, ACT, CUF na wengine, na hofu ya kuonja sumu
13. Ninakazia:
hiyo #12 hatutaki
Maswali yako mengine kuyajibu naona kuchoshana, kama una hoja iweke kwa mtindo huo twende sawa, lakini sio maswali juu ya maswali...
Ajabu unasema nimeandika mengi yasiyo eleweka halafu unasema kwangu neno "demokrasia ni shida", wakati kwenye hayo maelezo yangu nimekuonesha na wenzako demokrasia ikoje kwa vitendo, na sio maneno kama haya unayoandika hapa.
- Hapo demokrasia ni shida kwangu au kwenu? au kwenu demokrasia simply mnamaanisha mnachokitaka nyie ndio lazima kiwe tofauti na wengine walivyoamua?! kutaka Mbowe aondoke mna maana ipi? ndio demokrasia yenu hiyo?! hata siwalewi na ndio maana hata mleta mada nae amepotea!.
All in all, muda wa Mbowe ukifika ataondoka, simple, kama hamumtaki muandaneni yule mumtakaye, lakini kupiga kelele zenu wakati huu ni kukivuruga chama kikiwa kwenye harakati zake nyingine.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app