Nimesoma hii nikataka nipite tu ila nikaona niandike kitu; naona wengi mnataka Mbowe ajiuzulu na kuomba radhi, tena wengine mnakuja na sababu zilizotoka nje ya mada zisizo na msingi wowote.
- Kumpokea Lowassa, hili hakulifanya mwenyewe, yale yalikuwa ni maamuzi ya KK ya chama chao kumpokea Lowassa, ndio maana siku ilipofika, karibia nusu ya wajumbe wa KK walikuwepo pale kumpokea, sijui kama mnajua maana ya collective responsibility au ni mihemko tu.
- Maridhiano; hivi mmewahi kujiuliza kwanini alitaka maridhiano wakati ule, au mnapiga kelele tu?
Wakati ule wa Magufuli kwa mfano, na aina ya siasa alizokuwa akizifanya Magufuli, mlitegemea Mbowe aende sawa na Magufuli kwa namna ipi? ni ipi kwenu ilikuwa njia sahihi kwa Mbowe kufanya siasa wakati ule badala ya maridhiano? Itajeni hapa, au mlitaka ashindane nguvu na Magufuli ambaye kila mmoja alimjua kwa ukatili wake?
Mbowe kuja na wazo mbadala leo mnamuona mkosefu, mlitaka akachukue wapi jeshi la kumuwezesha kuandamana? mfano yale maandamano yao kule Kinondoni alipokoswa na risasi pamoja na wenzie, mlitaka ile ndio iwe njia yao ya kufanya siasa, wakati wewe una mdomo unashindana na mwenzio anayetumia risasi kuyazuia?
Ajabu Mbowe "kukosea" kama mnavyoona nyie kwa thinking yenu, not me; anatakiwa kujiuzulu, hivi ni malaika yupi atakayekuja kuiongoza Chadema ambaye hatakosea [kama kweli kosa litakuwepo sio haya makosa yenu ya mihemko]?
Nawashauri tu, kama Mbowe hamumtaki kuweni straight kusema hivyo, mtoe na sababu zenu zitakazomuhusu personally, kama mwingine alivyozoea kuimba kiongozi akikaa miaka kumi akili yake inachoka!, hata kama ni sababu ya kuchekesha lakini atleast ametoa sababu, sio kuja na sababu za jumla kama kumpokea Lowassa, mnazidi kujipoteza, au kumtaka ajiuzulu kisa "amekosea", huyo malaika yuko wapi aje apewe Chadema leo?!
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app