Mbowe Ni mwenyekiti makini
Kwenye msafara wa mamba, muhimu Kujua, kenge huwa kazini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbowe Ni mwenyekiti makini
Yeah ni kweli lakini huwa ana weakness ya kuwa outsmarted so easilyMbowe Ni mwenyekiti makini
Binafsi napendekeza mwenyekiti wa ccm ajiuzulu nafasi moja , achague kuwa Rais au mwenyekiti wa chama inawezekana vipi tumikia nafasi zote mbili kwamba ccm hakina watu wa kushika nafasi ya uwenyekiti, ndo mambo hayaendi
Habari Wana JF. Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samiah.
Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe 21/1/2023, Mbowe alidai hatamsema vibaya mama Samiah , Leo inakuwaje ndio anashtuka muda umeenda? na kudai anajuta kumwamini Mama Samiah?.
Pia nakumbuka kwenye mkutano wake na diaspora wa Marekani tarehe 11/12/2022, Mh Mbowe alidai kuwa hatarudi nyuma kwenye mazungumzo, na kudai anaweka maslahi ya nchi mbele na sio CHADEMA, Leo inakuwaje anajutia kumwamini Rais Samiah.
Mh. Mbowe anajua yaliyotokea Zanzibar na alitakiwa kuchukua Kama fundisho. Kwamba pamoja na maridhiano, CCM wakaiweka CUF ya maalim kwenye mtego mpaka leo imekuwa historia. Mwishoni maalim ikabidi akimbilie ACT baada ya Msajili kutumika kumfustrate. Hii ilitosha kumfundisha Mbowe aache kujikomba kwa Mh Samiah na CCM yake. Ilitakiwa ajifunze kutoka kwa Maalim. Kwamba pamoja na Maalim kujishusha na kukubali maridhiano , CCM wakakivunja chama chake Cha CUF na pia kumfanyia unyama 2020.
Sasa Kutokana na kauli ya Mh Mbowe ya Jana, Naomba nishauri yafuatayo:
1. Kwakuwa Mh. Mbowe alilazimisha Maridhiano na yeye kujiweka mbele Kama kiongozi wa maridhiano, basi kwa kuwa maridhiano yameshindikana, nashauri aachie ngazi mara moja. Maana kashindwa kutimiza hayo maridhiano aliyo lazimisha.
2. Kwa kuwa Mh. Mbowe alidharau sauti za wanachama wa CHADEMA kumkataza kuendelea na hayo maridhiano, na kwa kuwa hakufanikiwa na hayo maridhiano aombe Radhi wanachama kwa maamuzi hayo ambayo hayakufanikiwa na yaliyoiweka CHADEMA rehani.
3. Kwa kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kutimiza approach yake ya diplomacy , itakuwa ujinga akiendelea kuongoza approach nyingine dhidi ya serikali au CCM maana haaminiki Tena. Hivyo ajiuzulu kupisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambaye atatumia approach nyingine kabisa kuliko ya Mbowe.
4. Kwamba, kwakuwa imeonekana maridhiano sio njia sahihi ya kutatua malalamiko ya CHADEMA kutokana na kiburi Cha CCM na serikali yake, nashauri CHADEMA waachane na approach ya maridhiano watafute approach nyingine.
5. Kwa kuwa inaonekana maoni ya CHADEMA kwenye mswada ya sheria yamekataliwa na Kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria, nashauri CHADEMA watangaze rasmi kutoshiriki chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Naomba kuwasilisha.
😝😝😝Mbowe Ni mwenyekiti makini
Jana sio leo by the way who is Mange katika taifa hili, iweje linganisha Mange na taasisi kama chadema😂 😆
Muulize Da Mange anawajua wabongo !
Yaliyowapata Zuma and Thabo Mbeki SAWakifanya hivyo watapotea mazima. Maana Rais anaweza kupingana na mwenyekiti wake.
Jana sio leo by the way who is Mange katika taifa hili, iweje linganisha Mange na taasisi kama chadema
Huyo Mbowe Mimi Sina imani naye muda mrefu sana. Toka blunder ya kumpokea Lowassa kwa njia ya Voda fasta na kumpa nafasi ya kugombea urais, kisha hakufanikiwa kwenye jambo lile, kwa kiongozi muwajibikaji alipaswa kukaa pembeni. Lakini bila aibu akogombea tena uenyekiti ndani ya cdm uchaguzi uliopita. Kibaya zaidi alisema 2023 ataachia uenyekiti, lakini naona anajikausha tu!
Hayo mambo ya maridhiano toka mwanzo tulisema ni kupoteza muda. Tuliwapinga cdm hata walivyokwenda Mwanza kwenye sherehe za uhuru wakati wa Magufuli kutaka maridhiano, matokeo yake Magufuli akawwpuuza waziwazi. Ni kama Mbowe analazimisha yasiyowezekana ili asifiwe na ccm kuwa ana siasa za kistaarabu, na wakati huohuo kuwaburuza cdm kwa jambo ambalo wanaona kabisa haliwezekani. Huyo Mbowe hastahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm maana ni kama kapoteza muelekeo, sasa anataka kukipotezea chama mwelekeo.
Sasa kama rais anafanya mambo ya hovyo kwa nini chama kisipingane naye ili kuweka sawa, shida ni kufikili kwamba kumpinga rais ni dhambi, ccm ije na mwenyeki wa chama ,Rais abaki timiza majukum yake ya kitaifa , periodWakifanya hivyo watapotea mazima. Maana Rais anaweza kupingana na mwenyekiti wake.
Tulipokuwa tunawaambia Mbowe anapaswa kustaafu mlitutukana na kutuita CCM, ila kwa mwenye akili timamu Mbowe hana maarifa tena yakuisaidia na kuiongoza chadema kupata dola.
Na sababu hasa ya watu kushuka moral ni yeye pale alipodanganywa na Lowassa asitishe maandamano ya ukuta, eti akifanye cdm chama Cha siasa na sio chama Cha kiharakati. Sasa kaingizwa chaka kujifanya anafanya siasa, matokeo yake anakalishwa vikao vya hadaa viitwavyo maridhiano sijui upuuzi gani, lakini mapendekezo yote yanatupiliwa mbali.Kweli kabisa mkuu. Ni Kama anawapa nafasi CCM. Leo anahitisha maandamano wakati political heat imeshuka.
Kabisa, a good dancer knows when to leave a stage. Mbowe agomewe waziwazi aache wasiotaka mambo ya ccm wasonge mbele.Hakuna Cha uhafidhina. Ajiuzulu tu amefail.
Mfano halisi, Lowassa fisadi, kisha gia ikabadilishwa angani, mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani! Kama Kuna kosa kubwa la kiufundi lilifanyika ndani ya cdm ni lile. Namna pekee ya kuisafisha cdm nilishauri ni Mbowe atoke hadharani na kujiuzulu huku akikiri kosa like hadharani, tena ikibidi asema yeye ndio alitumia nafasi yake vibaya kumpokea mtu yule kimakosa. Kisha angeingia mwenyekiti mwingine, pale cdm ingekuwa imetakasika.Kweli mkuu, Leo tunasema hivi kesho tunasema kingine.