Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Primary target ya ujasusi was Tanzania ilikua katiba mpya!na chadema ilipaswa kuwa sauti hiyo!

Wao wakazimishwa na nusu mkate yaani wakafika bei hii ikaleta hasira kali na kutokuaminika Kwa mbowe Toka Kwa wale jamaa wanaopigania katiba!!

Nadhani plan ya katiba kabla ya uchaguzi imefeli coz mwenyekiti was CCM ame was outsmart wale jamaa wa Dola!Sasa nadhani wata execute plan B:-

1.Uchaguzi 2025 uvurugike mabaka wakachukua Dola!

2.Damage ya kisiasa Kwa mtia Nia was urais mapema ambae no mwenyekiti was ccm,nadhani wamefanikiwa coz hakuna mwananchi was kawaida kabisa anaemkubali kihivyo has Hulu bara tumebaki sisi chawa wa mchongo tukiziimba nyimbo zake Ili kufurahia ugali na teuzi zake!!

Lengo ni kumuingiza mgombea mwingine 2025 na sie huyu !

3.Hii mbaya sana!I have a feeling ni kuwindana Hadi viwanja vya ndege ili apewe mwingine!!

Watumishi wanaomba mungu haha yasitokee!

Hoi inachagizwa na Ile "original plan in and out""!!!

Ngoja tuone!!!

Mbowe kafeli coz hajui no Dola ilishinikiza atolewe mahabusu Kwa kesi ile Ili apiganie katiba Sasa yeye kalamba asali plus nusu mkate!!!
Pia inawezekana no plan ya mbowe kurudisha Imani ya wanachama kwake baada ya kuvurunda,Kwa kuitisha maandamano!!


Ngoja nisubiri!!!
Inafikirisha sana !
Ngoja izidi kunyesha tuone panapovuja
Karma Karma Karma
Tunasubiri tuone
 
Kila jambo na wakati wake, kitabu kimesomeka kwa utulivu na kukielewa, namanisha kulitakiwa kutulia na kuusoma mchezo wa ccm, kwa kipindi kile kujitoa kwenye maridhiano hakukua na tija yoyote , ni mda sasa kusonga mbele mbwai mbwai ,hakuna sababu ya hoja yako

Uli
Yes, kila Jambo na wakati wake. Ni wakati wa Mbowe kustaafu. Let's get fresh brain. Ni aibu CHADEMA kuwa outsmarted na hiyo mama.
 
Sawa. Ila hoja yangu Ina mantiki.
Hakuna mkuu, kuna mambo ayahitaji mihemuko, safari ni mwendo au atua moja kwenda nyingine , Maridhiano ilikua sehem ya mwendo , so iyo phase imeisha twende na phase mpya sasa , Uongonzi wa Chadema mpaka sasa wapo sawa kabisa
 
Wana CCM watakupinga kwasaba Mbowe ni mtu muhimu sana kwa utawala wa CCM kwenye kulaghai wafuasi wake ili mambo yaende.

fikiria mwenyekiti wa chama angekua Lisu au Heche rasimu ya katiba ya Warioba wangeitilia mkazo na kingeeleweka.

Kweli kabisa. Mbowe alikuwa na golden chance akaichezea kwa kutaka kumfurahisha ye mama asiyekuwa na ukweli. Unakimbilia Ikulu kisa Nini? Kujitetea kwingi, mwishowe mama kapata kila kitu.
 
1. Ungekuwa sahihi kama tusingelikoroga mbeya.

2. Hatumjui adui yetu.

3. Hatuna msimamo, falsafa haijulikani.

4. Tunahitaji kwenda shule:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

5. Misimamo yetu haiwezi kuwa Kwa ku bet!
Chama kama taasisi, hakiwezi kuwa kinakurupuka na kucheza mdundiko wa kila anaepiga ngoma, hata ya Mbeya chama kilijipa mda wa kutafakari na kuja na mahamuzi waliokuja nayo,

Huwezi kubeba maiti usiejua amefia wapi kisa tu umeshirikishwa
 
Habari Wana JF. Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samiah.

Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe 21/1/2023, Mbowe alidai hatamsema vibaya mama Samiah , Leo inakuwaje ndio anashtuka muda umeenda? na kudai anajuta kumwamini Mama Samiah?.

Pia nakumbuka kwenye mkutano wake na diaspora wa Marekani tarehe 11/12/2022, Mh Mbowe alidai kuwa hatarudi nyuma kwenye mazungumzo, na kudai anaweka maslahi ya nchi mbele na sio CHADEMA, Leo inakuwaje anajutia kumwamini Rais Samiah.

Mh. Mbowe anajua yaliyotokea Zanzibar na alitakiwa kuchukua Kama fundisho. Kwamba pamoja na maridhiano, CCM wakaiweka CUF ya maalim kwenye mtego mpaka leo imekuwa historia. Mwishoni maalim ikabidi akimbilie ACT baada ya Msajili kutumika kumfustrate. Hii ilitosha kumfundisha Mbowe aache kujikomba kwa Mh Samiah na CCM yake. Ilitakiwa ajifunze kutoka kwa Maalim. Kwamba pamoja na Maalim kujishusha na kukubali maridhiano , CCM wakakivunja chama chake Cha CUF na pia kumfanyia unyama 2020.

Sasa Kutokana na kauli ya Mh Mbowe ya Jana, Naomba nishauri yafuatayo:

1. Kwakuwa Mh. Mbowe alilazimisha Maridhiano na yeye kujiweka mbele Kama kiongozi wa maridhiano, basi kwa kuwa maridhiano yameshindikana, nashauri aachie ngazi mara moja. Maana kashindwa kutimiza hayo maridhiano aliyo lazimisha.

2. Kwa kuwa Mh. Mbowe alidharau sauti za wanachama wa CHADEMA kumkataza kuendelea na hayo maridhiano, na kwa kuwa hakufanikiwa na hayo maridhiano aombe Radhi wanachama kwa maamuzi hayo ambayo hayakufanikiwa na yaliyoiweka CHADEMA rehani.

3. Kwa kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kutimiza approach yake ya diplomacy , itakuwa ujinga akiendelea kuongoza approach nyingine dhidi ya serikali au CCM maana haaminiki Tena. Hivyo ajiuzulu kupisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambaye atatumia approach nyingine kabisa kuliko ya Mbowe.

4. Kwamba, kwakuwa imeonekana maridhiano sio njia sahihi ya kutatua malalamiko ya CHADEMA kutokana na kiburi Cha CCM na serikali yake, nashauri CHADEMA waachane na approach ya maridhiano watafute approach nyingine.

5. Kwa kuwa inaonekana maoni ya CHADEMA kwenye mswada ya sheria yamekataliwa na Kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria, nashauri CHADEMA watangaze rasmi kutoshiriki chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Naomba kuwasilisha.
Umeombwa na nani ushauri? Mtu yeyote timamu hatoi ushauri hadi aombwe.

Pili anzisha chama chako ili ufanye hayo unayodhani ndiyo sahihi. Kwa nini mambo ya chama kingine yakuume?
 
Uli
Yes, kila Jambo na wakati wake. Ni wakati wa Mbowe kustaafu. Let's get fresh brain. Ni aibu CHADEMA kuwa outsmarted na hiyo mama.
Mwenyeki wa chama hajiteuwi mwenyewe, anachaguliwa pitia vikao halali vya chama, kwa kujinadi na kuomba kura ,siku ambapo hatapigiwa kura za kutosha basi atakoma kuwa mwenyekiti , mbona kitu simple tu
 
Chama kama taasisi, hakiwezi kuwa kinakurupuka na kucheza mdundiko wa kila anaepiga ngoma, hata ya Mbeya chama kilijipa mda wa kutafakari na kuja na mahamuzi waliokuja nayo,

Huwezi kubeba maiti usiejua amefia wapi kisa tu umeshirikishwa

1. Bila kuwa falsafa inayokubalika kukurupuka kunaepukwa vipi ndugu?

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

3. Adui ni adui, kwa mujibu wa falsafa, siyo kwa kuvizia.

4. Nendeni shule, misimamo haiwezi kuwa kwa ku bet!
 
Hakuna mkuu, kuna mambo ayahitaji mihemuko, safari ni mwendo au atua moja kwenda nyingine , Maridhiano ilikua sehem ya mwendo , so iyo phase imeisha twende na phase mpya sasa , Uongonzi wa Chadema mpaka sasa wapo sawa kabisa

Kwa upande wako sawa, ila kwangu Mimi wamefail. Approach ya maridhiano imefail. Kwanini tulilazimisha tukijua CCM hawaaminiki?. Katiba Mpya no, wabunge Nuksi no, mswada wa sheria za uchaguzi batili. Kwanini Kiongozi alazimishe kuamini watu ambao hawajawahi kuaminika?

Ok, Mimi nimesema yangu ila huko mbele tunapoelekea sijui. Mbowe atambue ni kiongozi wa chama na lazima chama kiwe na msimamo mmoja. Sio Leo mazungumzo, kesho maandamano, keshokutwa mazungumzo. All in all Mbowe kakidharilisha chama kwa kumuamini Samiah bila kujua ni mwanaccm.
 
Mwenyeki wa chama hajiteuwi mwenyewe, anachaguliwa pitia vikao halali vya chama, kwa kujinadi na kuomba kura ,siku ambapo hatapigiwa kura za kutosha basi atakoma kuwa mwenyekiti , mbona kitu simple tu
Sema hivi utaeleweka vizuri
Afrika hakuna utamaduni wa kujiuzulu ili kuwajibika kwa yale uliyoyavurunda
Just as simple as that
 
Kweli mkuu, Leo tunasema hivi kesho tunasema kingine.

1. Bila falsafa ya wazi tunayoiamini itakuwa ku bet.

2. Kwa falsafa ya wazi kina Mwabukusi na sauti ya Tanzania walikuwa wenzetu.

3. Tutakuwa wazi kuhusu Gaza, Ukraine, LGBTQ, tutapigania katiba mpya consistently nk.

4. Hapo #3 hatuta bet na lolote

5. Hapo #4, hatutapita kwenye embarrassments kama hizi.

6. Chawa chawa hawatakuwapo.

7. Hakutakuwa na uonja sumu.

8. Nk.
 
Back
Top Bottom